HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 215236,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/215236/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu. Kwanza nataka kuwashukuru waheshimiwa Wabunge wote waliochangia mjadala kuhusu Mswada huu. Tulisikiza kwa makini maoni yao yote. Tutakapoingia katika Kamati ya Bunge nzima, ni matumaini yangu ya kwamba Wabunge wataleta maoni yao kama marekebisho, ili tuweze kuboresha sheria hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna mengine ambayo yalisemwa kwa nia ya kuwafurahisha waandishi wa habari. Ni vigumu sana kuyajibu hayo kwa sababu hayawezi kujibika. Wabunge hao walikuwa wanajua kwamba wamepoteza mjadala. Kitu ambacho walikuwa na haja nacho ni kuwajulisha waandishi wa habari kwamba wako upande mmoja. Lakini sote tuko upande mmoja. Bw. Naibu Spika wa Muda, katika kuuandaa Mswada huu, Wizara ingependa kulijulisha Bunge kwamba tulijumuisha maoni na mapendekezo ya washikadau wote. Mhe. Bi. Ndung'u alipokuwa akichangia mjadala juu ya Mswada huu, alionyesha hofu na kutaka kujua kama tumepata maoni kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya habari. Ningependa kulijulisha Bunge kwamba ni kweli tumekuwa na mikutano na semina kadhaa na wamiliki wa vyombo vya habari. Wametoa mapendekezo yao ambayo tutayaleta tukiingia kwenye kipindi kingine cha mjadala kuhusu Mswada huu. Wakati Bunge litakapokaa ili kupokea mapendekezo, mojawapo ya mapendekezo ambayo yataletwa yametoka kwa wamiliki wa vyombo vya habari. Kwa hivyo, haileweki ni kwa nini kwa upande mmoja wamiliki wa vyombo vya habari wanatuletea mapendekezo na kwa upande mwingine, wanaendelea kuonyesha hofu kwamba sheria hii inaundwa ili kuwakandamiza. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo ambalo tunafanya si geni. Kama alivyosema Waziri, ni July 5, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2323 jambo ambalo limefanyika katika nchi zingine. Watu wamekuwa wakiandika sheria kama hii, kwa sababu wanataka kuimarisha demokrasia wala sio kuibomoa. Ni lazima Kenya iende na wakati. Nchi zingine zinafanya yale ambayo yatasaidia demokrasia. Kwa hivyo, sisi pia ni lazima tufanye vivyo hivyo. Hatuwezi kubaki pahali pamoja hadi nyumba yetu ibomoke ndipo tuanze kulia. Sheria hii hailengi kuvunja demokrasia. Lengo lake kubwa ni kuhifadhi demokrasia kwa kulinda masilahi ya wote. Maana ya demokrasia sio kuhifadhi maslahi ya wachache tu bali ya kila mtu. Hilo ndilo lengo kubwa la Mswada huu. Bw. Naibu Spika wa Muda, lengo la kwanza la Mswada huu wa vyombo vya habari ni kuhifadhi uhuru wa habari. Ukisoma Mswada huu, utaona kipengee kinachosema hivyo. Lakini wakati tunahifadhi uhuru wa habari, lazima tuhakikishe ya kwamba uhuru huo hautumiwi kuhujumu maslahi ya watu wengine. Ni lazima kila mmoja katika nchi yetu awajibike katika kutumia uhuru. Vyombo vya habari ndivyo vya kwanza kudai ya kwamba kila mtu lazima awajibike. Kwa hivyo, vile wanavyotaka watu wengine wawajibike, ni lazima nao pia wakubali kuajibika. Bw. Naibu Spika wa Muda, hakuna mtu, hata Mheshimiwa Rais, aliyepewa na Katiba haki au uhuru usiokuwa na mipaka. Hapa tunaambiwa ya kwamba vyombo vya habari vinastahili uhuru usiokuwa na mipaka. Wanadai ya kwamba tusipofanya hivyo, tunavunja Katiba ya nchi hii. Katiba inawekea kila mtu mipaka ya kutekeleza haki na uhuru. Kama nilivyosema jana, mtu haruhusiwi na Katiba kwenda katika majengo ya sinema na kusema moto na ilhali hakuna moto. Jambo kama hilo linaweza kuwafanya watu wauane bure wakikimbilia usalama wao. Mtu wa aina hiyo atakuwa amevunja sheria na Katiba pia. Kwa hivyo, Katiba yetu imeweka mipaka. Mswada huu pia hauvunji haki za wanahabari hata kidogo. Kwa kusema kweli, lengo ni kuhifadhi haki hizo. Katiba yetu haipi vyombo vya habari au mtu yeyote uhuru wa kuingilia haki za mtu mwingine. Bw. Naibu Spika wa Muda, jana tuliambiwa na mhe. M. Kilonzo ya kwamba lengo la Mswada huu ni kuvunja haki za Katiba za vyombo vya habari. Na pia akasema ya kwamba ili tusiwavunjie haki zao za kikatiba, basi waruhusiwe kuandika na kusema chochote. Hilo haliwezekani. Katiba haimpi mtu yeyote uhuru na uwezo huo wa kuvurugia wengine maslahi na haki. Ni kweli Katiba inahifadhi haki ya kila mtu katika nchi hii. Lakini haimpi mtu uhuru wa kusema na kuandika chochote anachofikiria. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni maoni yetu ya kwamba vyombo vya habari vinadai uhuru ambao hauna mipaka. Tunaweza kusema ya kwamba wanachotafuta ni udikteta. Tunakumbuka vizuri ya kwamba vyombo vya habari vimekuwa katika mstari wa mbele vikisema ya kwamba Serikali lazima isiwe ya kidikteta. Ni lazima Bunge hili lisiwe na nguvu za kidikteta. Ni lazima mahakama yasiwe na udikteta. Hicho ndicho tunachouliza vyombo vya habari pia, visiwe na nguvu za kidikteta. Vyombo hivi vina nguvu na uwezo mwingi. Ikiwa uwezo huo utatumiwa vibaya, basi nchi hii itapata hasara kubwa sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia kufuata maadili ya uwandishi sikuvunja Katiba. Jana, nilishangaa sana kusikia ya kwamba hata kutafuta tafsiri ya mwanahabari kuhusu jambo fulani utakuwa unaivunja sheria. Hilo haliwezekani. Mswada huu hauruhusu vyombo vya habari kushambuliwa na mtu yeyote. Baadhi ya waheshimiwa Wabunge jana walizungumza kama kwamba Mswada huu unatoa kibali cha vyombo hivyo kushambuliwa. Yeyote ambaye amesoma vizuri Mswada huu na hataki kupotosha maana yake, atakubaliana nami hakuna jambo kama hilo. Kwa hivyo, vyombo hivi havina haja kuwa na hofu kwa sababu Mswada huu unavilinda na kuvitetea. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumeleta Mswada huu kwa sababu vyombo hivi vimeshindwa kujidhibiti chini ya Baraza la Wanahabari. Sisi katika Wizara mara nyingi tunawauliza: \"Kwa nini vyombo vya habari havijidhibiti?\" Baraza la Wanahabari hudai kuwa wameshindwa kuvidhibiti vyombo hivi kwa sababu hawana sheria. Wanataka sheria ambayo itawapa meno. Lengo la 2324 PARLIAMENTARY DEBATES July 5, 2007 Mswada huu ni kulipa Baraza la Wanahabari meno ili iweze kudhibiti vyombo hivi. Hata kama wengine wetu wanasema vyombo hivi vinaweza kujidhibiti vyenyewe, jambo hili haliwezekani kama hakuna sheria ambayo itasaidia Baraza la Wanahabari kuweza kuchukua hatua dhidi ya yeyote ambaye anavunja maadili au atakosa kufanya kazi inavyotakikana. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna ushahidi chungu nzima ya kwamba vyombo hivi vilishindwa kujidhibiti. Kuna mambo mengi yanayoweza kusemwa lakini la muhimu zaidi ni kwamba vyombo hivi haviwezi kuhurusiwa kuchochea ukabila na chuki katika nchi."
}