HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 215257,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/215257/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Mswada huu wa sheria ya tumbaku. Kama alivyosema Waziri Msaidizi mwenzangu, hii ni hatua kubwa sana. Labda ni ya kwanza katika kaya hii yetu. Natumaini ya kwamba Wabunge wote, hasa Maj. Madoka, wataona haja ya kuunga mkono Mswada huu. Bw. Naibu Spika wa Muda, natumaini ya kwamba watu wetu wataweza kujua ya kwamba hakuna uungwana au uustarabu katika uvutaji wa sigara. Wengi wa wale ambao wanavuta sigara, hasa vijana, wavulana na wasichana wachanga, wanavuta sigara kwa sababu wanataka kuonekana kama waangwana wa aina ya kipekee. Ni rahisi sana vijana kushawishika kuvuta sigara ili waonekane \"wamefika\". Jambo hilo linafanyika kwa sababu vijana wetu hawajui hasara za kuvuta sigara. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna picha moja ambayo nimekuwa nikiiona katika majumba fulani. Picha hiyo inaonyesha magonjwa ambayo yanaletwa na uvutaji wa sigara. Mtu akiitazama picha hiyo, anatishika na kuogopa mara moja! Nimekuwa nikiwaza ni kwa nini picha hiyo haiwezi kusambazwa katika sehemu zote katika nchi hii, ili watu wakiiona waelewe vizuri hasara za kuvuta sigara. Utaona mapafu yamelika, mikono imeoza, meno iliisha zamani na hakuna mtu! Sijui ikiwa Wizara ya Afya inaweza kusambaza picha hiyo kila mahali, ili watu waone na waelewe. Wakati mwingine, watu wanaelewa picha zaidi ya maandiko au matamshi. Kinachosemwa na picha hiyo ni kwamba, hakuna cha kufaidi kwa kuvuta sigara. Ni magonjwa na hasara tupu! Bw. Naibu Spika wa Muda, sigara ni sumu. Ningeulizwa, tungechukua hatua kali kabisa, hata ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara. Ikiwa sigara ni sumu, kwa nini turuhusu watu wetu watumie sumu, eti kwa sababu ya zile pesa zinazopatikana kutokana na kilimo na biashara ya kuzalisha sumu? Sumu ni kitu cha kupigwa marufuku. Siyo kitu cha kubembelezwa. Isitoshe, ukiangalia hasara, na nimeelezwa na mtaalam mmoja--- Hasara ambayo nchi inapata kwa kugaramia matibabu ya wagojwa wa uvutaji sigara - wenye saratani, vifua vikuu na khadhalika--- Pesa ambazo zinatumika kuwatibu ni nyingi kuliko zile zinazopatikana kutokana na kilimo na biashara husika. Kama hivyo ndivyo kulivyo, ni kwa nini tuendele na jambo hilo? Ni kwa nini tusifanye hesabu na kama gharama ya kutibu magonjwa inazidi faida inayopatikana kutoka kilimo na biashara hiyo, jawabu ni kupiga marufuku uvtutaji wa sigara na kuachana na mambo hayo! Bw. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia, utaona ya kwamba nchi zingine zimefanya vile nimesema. Utakuta nchi zilizoendelea--- Sidhani zinalima tumbako tena. Uvutaji wa sigara umepunguka kwa kiasi kikubwa hivi kwamba kampuni ambazo zinafanya biashara ya sigara zimehamia katika nchi zinazoendelea. Zimehama Ulaya na Marekani. Kampuni hizo zimekuja huku. Huku ndiko tumbaku inalimwa na ndiko sigara zinatengenezewa. Ukiona mzungu ameachana na jambo, ni afadhali uonyeke mapema. Kama biashara hiyo ingekuwa na faida, mzungu hangeiwachia nchi zinazoendelea. Lakini ameelewa ya kwamba hasara ndiyo kubwa na July 5, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2329 ameachana na kazi hiyo. Amewaachia wajinga. Unajua wajinga ndio waliwao. Mswahili alisema. Lazima tujifunze kutoka kwao. Ndio walianzisha mambo hayo na wameachana nayo. Sijui ni kwani nini tuendelee. Eti kwa sababu sisi ni maskini sana, chochote ambacho kinaweza kuajiri watu kazi, hata kama kazi hizo hazina faida kubwa, bado tunakishikilia. Bw. Naibu Spika wa Muda, nilishangaa wakati Bw. Kimunya alisema kwamba sigara ambazo zinavutwa na wananchi wa kawaida zisiwekewe kodi. Hiyo ni kumaliza watu! Ningeulizwa, sigara zote zingewekewa kodi kwa kiasi ambacho watu hawangeweza kuzinunua. Lakini sasa, kuwaachia maskini hohe hahe sigara zao--- Hata mtu akipata shida kidogo au kuumwa na kichwa, anakimbilila sigara. Hao watu wataisha! Wataisha kabisa kwa sababu watavuta sigara, watajaa kifua kikuu, wataliwa na saratani, watagonjeka na washindwe kusomesha watoto wao na mwishowe, watakufa! Kile kilichofanywa na Bw. Kimunya katika Bajeti kitaletea nchi hii hasara kubwa. Labda, hasara hiyo haitaoneka wakati huu. Itaonekana baada ya miaka kama mitano hivi. Wakati huo ndiyo tutaanza kutibu magonjwa ya wananchi wa kawaida yanayotokana na uvutaji wa sigara. Sijui ikiwa wananchi walifurahia kwa sababu sigara zao hazikuwekewa kodi. Wangekuwa wajuzi, wangejua ya kwamba walikuwa wanasukumiwa sumu. Sio kwamba walikuwa wanapakwa mafuta. Hakuna jambo jema pale! Ni hasara tupu na ni makosa yaliyofanyika! Lakini, tuachane na yaliyopita na tugange yajayo. Sijui tutayagangaje kwa sababu hasara yaja! Itakuja ikiwa hasara kubwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumbaku ina ulevi ambao ni sawa au unakaribiana sana na ulevi wa mihadarati. Ukitaka kujua ya kwamba wanaovuta sigara wanalewa kama watumizi wa madawa hayo ya mihadarati, kwenda jela! Katika jela, kuna watu ambao watafanya chochote kupata sigara. Sigara ndizo pesa za jela. Ukiwa nazo, hakuna kitu huwezi kupata. Utapata wale"
}