GET /api/v0.1/hansard/entries/215259/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 215259,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/215259/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": "- wale ambao wamekolea katika jela mpaka wamekuwa kama wafalme kiasi kwamba hakuna kitu hawawezi kuingiza katika jela--- Wale matrustee wakiwa na sigara zao, utakuta watu wanapanga laini wakati kunapeanwa nyama. Nyama inapeanwa vipande vidogo sana mara tatu kwa wiki. Vile nyama ni nadra, hakuna mtu ambaye hangetaka kula nyama hiyo. Lakini utakuta ya kwamba tamaa ya kuvuta sigara ni kubwa kuliko ile tamaa ya kula nyama. Unakuta watu wamepanga laini. Mtu anapewa sigara avute mara moja tu na kisha anairusha nyama yake kwenye bakuli. Mpaka unawahurumia watu hawa. Watu hawa hawapati nyama kwa miezi mingi na wakiipata wako tayari kuipeana kwa sababu ya kiu cha sigara. Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikutana na mtu mmoja pale gerezani ambaye alikuwa akipata maziwa kwa sababu ya ugonjwa wa kifua kikuu. Lakini maziwa yale ambayo yangemsaidia kuponyesha ugonjwa huo, aliyapeana ili apate sigara. Muuzaji sigara alipata maziwa kwa kubadilishana na sigara. Huyu mtu mwingine aliachana na dawa na akaendelea kuvuta sigara. Tulimwambia akiendelea na tabia hiyo atakufa. Akatuambia, \"kwani uhai wangu ni wenu? Nyinyi mnajali nini? Pilipili isiokuwa mdomoni mwako inakuwashia nini?\" Na unajua, hatukukaa wiki tatu, mtu huyo akafa. Katika jela watu wengi wemekufa na wengi wameharibiwa maisha yao kwa sababu ya sigara. Inaonekana kama ni vigumu na haiwezekani kusimamisha biashara ya sigara katika jela. Kama mhe. Makamu wa Rais angekuwa hapa, ningemuuliza kama amefaulu kukomesha uvutaji wa sigara katika jela. Bw. Naibu Spika wa Muda, sijui kama umesikia tatizo la ushoga. Tatizo hili katika jela zetu linachochewa na uvutaji wa sigara. Walevi wa sigara wako tayari kufanywa wake na waume wengine ili wapate sigara wavute. Hili ni jambo la uchungu sana. Hebu waza; kwa bahati mbaya kijana wako akafungwe jela kwa sababu amefanya kosa dogo sana halafu miaka miwili baadaye, huyo kijana wako anaachiliwa akiwa shoga. Utalia machozi! Hili si jambo ambalo linalotokea kwa wachache. Ni jambo linalotokea kwa wengi. Ni lazima kutafutwe njia ya kuhakikisha sigara haziingii katika jela au wasimamizi wa jela wafanye vile wakoloni walivyofanya. Wakoloni waliruhusu watu wavute sigara. Sigara zilikuwa zinauzwa katika duka za jela. Kwa vile ilikuwa 2330 PARLIAMENTARY DEBATES July 5, 2007 rahisi kuzipata, ilikuwa ni vigumu kumfanya yeyote ajigeuze mwanamke au mwanaume ili aweze kupata sigara kutoka kwa mwingine. Ni muhimu kwa sisi kuwafikiria vizuri wale watu ambao kwa bahati mbaya wameingia katika jela. Tufikirie ni kitu gani kinaweza kuhakikisha kwamba ulevi huu wa sigara haitumiwi kuharibia wengine maisha kabisa katika magereza. Aidha, watu waruhusiwe kuvuta sigara kama vile siku hizi wanaruhusiwa kuona runinga na vitu vingine; hata kutembelewa na wake zao. Bw. Naibu Spika wa Mda, hili ni jambo moja ninaloliunga mkono sana. Mtu aliyewekwa jela aruhusiwe kutembelewa na mwenzake. Kama ni bibi, aruhusiwe kukutana na mume wake. Kama ni mume, aruhusiwe kukutana na bibi yake. Hii ni kwa sababu lengo la kifungo si kuharibu nyumba, ni kurekebisha mtu. Lakini kama utatoka jela ukute bibi yako alikimbia kwa sababu muda huo wote hamuruhusiwi kukutana naye, mwenye kuadhibiwa ni mfungwa wala si wale wako nje. Lakini bibi anakuwa amefungwa wakati anakatazwa kuonana na bwana wake au hata kupata watoto. Kwa hivyo, waliofungwa, waadhibiwe wao lakini nyumba zao zihifadhiwe kwa namna moja au nyingine. Hii ni imani yangu. Na wale ambao hawajaingia katika jela wakaonja maisha ya huko, basi waombe sana wasiingie! Kule ni kubaya. Lakini ni vizuri wakati mwingine kwa sababu kunaelimisha mtu. Kunakufanya uelewe ya kwamba hata mfungwa bado ni binadamu. Si vizuri kumunyima haki zake mwenyewe pamoja na haki za familia yake. Ni lazima kuwe na tofauti kati ya familia na mfungwa. Tusiwaadhibu watoto na bibi yake. Jambo hilo halifai. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunapofikiria namna ya kumaliza au kupunguza uvutaji wa sigara, ni lazima tujue kwamba kuna wale ambao wanategemea kilimo cha tumbaku. Kuna wale ambao wanategemea biashara za tumbaku. Hawa watatusikia tunaongea lugha mbaya tukisema kwamba tunataka kumaliza kilimo na biashara hii kama hatujawatafutia kazi nyingine. Kama tutasema wasiajiriwe kazi na makampuni ya kuuza sigara, lazima tutafute mbinu au namna ya kuwatafutia ajira tofauti. Tusipofanya hivyo, tutakuwa tunakosa. Sijui kama kwa Bw. Ojaamong wanalima tumbaku. Lakini ninatumai ataelewa tunatoka wapi. Hatusemi watu wako wasiendelee kulima, tunachosema ni kwamba watafutiwe kazi nyingine. Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kufanya watu wapate riziki badala ya kulima au kufanya biashara ya tumbaku. Bw. Naibu Spika wa Muda, nikimaliza, ningetaka kupongeza Baraza la Mji wa Nakuru kwa kuwa mji wa kwanza kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo yanayotumiwa na umma. Katika ofisi za Serikali, maeneo ya hospitali na shule, wamesema ukipatikana ukivuta sigara, utaonyeshwa kilicho mfanya punda asimee pembe. Bw. Naibu Spika wa Muda, kitendo hiki cha Baraza la Mji wa Nakuru kinastahili kuigwa na miji mingine, na hasa jiji la Nairobi. Tumefikia uamuzi kwamba sigara ni mbaya, inaletea watu madhara. Kwa nini basi turuhusu watu wanapovuta sigara walazimishe wengine kuvuta sigara hiyo? Unapovuta sigara palipo na watu wengine, pale pakaingia mtu ambaye hataki kuhusiana na sigara, utakuwa unamvutisha sigara hiyo kupitia kwa moshi unaopuliza. Nimesikia wataalamu wanasema wakati mwingine, kwa kukaa tu palipo wavutaji sigara, utajikuta kwamba umevuta sigara kiasi cha asilimia 50 au 60. Kule Uropa, utakuta kwamba kuna sehemu katika mikahawa ambayo imetengewa wavutaji na nyingine ambayo imetengewa wasiovuta. Ukiingia sehemu ambayo imetengewa wavutaji, mara moja unaugua homa. Hii ni kwa sababu moshi ulioko pale ni wa ajabu. Ukiingia pale kwa bahati mbaya, inakuwa umelazimishwa kuvuta sigara bila kupenda. Dawa ni kuhakikisha ya kwamba popote pale palipotengewa watumizi wa umma, pasiruhusiwe uvutaji wa sigara. Sisi watu wa Nakuru tumeongoza nchi hii kwa mambo mengi, lakini wakati wa kugawa kwa rasilimali na makazi, tunasahaulika. Ni ajabu kwa ni Mji wa Nakuru ambapo hatuna Mawaziri, DCs, PCs, PSs, wakurugenzi wa makampuni na mabalozi. Tunataka ubaguzi huu uishe! Bw. Naibu Spika wa Muda, nikiongea juu ya Waziri, siongei juu ya Waziri nusu! Naongea juu ya Waziri mkamilifu. Waziri ambaye anaweza kufanya mambo muhimu. Si mtu wa kutumwa July 5, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2331 hapa na pale, au kuja hapa Bungeni kuyajibu maswali au kumwakilisha Waziri katika jambo fulani. Tunataka Waziri kamili! Tunataka kuwa Mawaziri wakamilifu kwa sababu tunatosha. Sasa, tunaongoza katika kupigana vita na tumbaku. Tuliongoza katika kuchagua Serikali hii. Hakuna wilaya ambayo ina watu wengi katika nchi hii kuliko wilaya ya Nakuru. Lakini, unakuta ya kwamba wakati wa kugawa rasilmali, tunatengwa. Tunatengwa eti kwa sababu sisi siyo kutoka kabila hili. Tunachosema ni kwamba sijui ni kitu gani kinangojewa. Wakaazi wenye wako"
}