GET /api/v0.1/hansard/entries/215261/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 215261,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/215261/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": "ni walipa kodi kama watu wa sehemu nyingine katika nchi hii. Mhe. G.G. Karikui hapa anatosha kuwa Waziri. Ijapokuwa alikuwa Waziri kwa muda mrefu sana. Nadhani sasa ingekuwa ni wakati wa kuwaachia watu kama sisi. Lakini tunachosema ni kwamba, hata kama hatutakalia viti hivyo, tunyimwe kwa sababu hatuna sifa, na siyo kwa sababu tunatoka Nakuru. Kuna wengi ambao wametunukiwa nyadhifa kubwa sana, na ni wavutaji wakubwa wa sigara. Tunauliza nchi ifuate nyayo za Nakuru katika kupiga marafuku uvutaji wa sigara. Hivyo, hivyo, tunauliza ya kwamba watu wa Nakuru, Laikipa na wakaazi wa Mkoa wa Bonde la Ufa ambao hawahesabiwi kama wakaazi wa pale--- Hatupati rasilmali zilizotengewa mikoa mingine kama vile Mkoa wa Kati. Hatupati kile ambacho kimetengewa wakazi wa Bonde La Ufa. Tunataka na sisi itambulike ya kwamba--- Ieleweke kwamba sisi ni raia sawa na wengine. Tunatoa kodi sawa. Hakuna kitu ambacho kimefanyika katika nchi hii ambacho sisi hatukufanya. Kuwa hivyo, wakati wa kugawa rasilmali na makazi makubwa, ni lazima sisi tupewe haki yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}