GET /api/v0.1/hansard/entries/215585/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 215585,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/215585/?format=api",
"text_counter": 288,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Wiki jana, Wizara yangu iliwasiliana na mheshimiwa Weya katika semina moja kule Naivasha na tulimfahamisha kwamba Wizara imetayarisha Mswada kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Kwa hivyo, jambo ambalo linatafutwa katika Hoja hii limeshughulikiwa vya kutosha katika Mswada huo. Mswada huo unaeleza kwa kikamilifu namna Serikali imeunda mfuko wa pesa ambazo zitatumika kusambaza teknolojia ya habari na mawasiliano katika kila pahali nchini. Serikali imeunda mpango maalum wa kuhakikisha kwamba kuna kijiji cha teknolojia ya tarakimu au digital village katika kila eneo la uwakilishi Bungeni. Kwa hivyo, ni wazi kwamba kinachotafutwa na Hoja hii kimeshughulikiwa na Mswada ambao Serikali inataka kuleta Bungeni, pengine wiki hii. Kwa hivyo, hatuna sababu yoyote ya kupinga Hoja hii. Ninatumai kwamba mheshimiwa Weya, labda, atakubali kuondoa Hoja hii kwa sababu inashughulikiwa na Mswada ambao Serikali imetunga na ambao utakuwa sheria ya habari na mawasiliano ukipitishwa na Bunge hili. Mswada huu utaletwa hapa Bunge hivi karibuni, pengine wiki hii. Shukrani, Bw. Naibu Spika wa Muda."
}