HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 215646,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/215646/?format=api",
"text_counter": 349,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo ni muhimu. Inahusu walemavu katika nchi yetu na hasa watoto walemavu. Nikianza, ningetaka kusema ni imani yangu kwamba jukumu la kuwaelimisha watoto walemave, na hata wale wazima, ni la Serikali. Wengine, kama makanisa na wafadhili, wanaweza tu kusaidia. Lakini jukumu lenyewe ni la Serikali. Serikali ina uwezo huo. Ni vyema Serikali itumie pesa za kodi kuhakikisha kwamba wale ambao hawana nguvu wanafaidika kutokana na pesa hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni jambo wazi kwamba kwa bahati mbaya jamii yetu haionekani kuwaheshimu walemavu ya kutosha. Ukiwa mlemavu, mara nyingi utaonekana kama wewe si mtu. Ni rahisi sana kwa watu kukubagua, kukutukana na kukutupa kando. Walemavu wanaonewa sana! Wanachukuliwa kama si watu, wananchi wakamilifu au kama si walipakodi. Ukweli ni kwamba hata walemavu wanalipa kodi na ni haki yao kurudishiwa hiyo kodi kwa njia ya huduma kutoka kwa Serikali. Hizo huduma ni kama elimu na nyinginezo. Kuna wakati tulikuwa na shule nzuri sana zilizokuwa zinashughulikia elimu ya walemavu. Lakini viwango vya shule hizo vimekuwa vikishuka hivi majuzi. Sijui tatizo ni nini. Wakati Prof. Olweny alipokuwa akitoa Hoja hii, nilidhani labda angetuambia ni kwa nini viwango vya shule hizo za walemavu vimekuwa vikishuka. Labda ni kwa kukosa pesa au kudhaminiwa vya kutosha. Ukiangalia shule tulizo nazo za walemavu wakati huu, na uzilinganishe na zile zilizokuwako miaka 20 au 30 iliyopita, utaona tofauti kubwa sana. Nahisi sana sana ni kwa sababu ya kukosa July 4, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2241 pesa za kuzisimamia. Bw. Naibu Spika wa Muda, hivi majuzi nilikuwa na mkutano wa walemavu hapa mjini, na nilikuwa nikiwashawishi wajiunge na Chama cha Mwananchi. Katika mkutano huo, walinieleza matatizo yao mengi. Waliniambia kwamba wakisoma, wanakuwa ndio wa mwisho kupata kazi, au mara nyingi hawapati kazi kabisa. Wamesoma, wana ujuzi wa aina moja au nyingine, lakini hawapati kazi. Waliniambia kwamba wakisafiri, kwa sababu ya viti vyao, wanatozwa nauli mara mbili ya nauli ambazo zinatozwa watu wengine. Nilishangaa kabisa, eti wakati watu wazima wanatozwa, kwa mfano, Kshs40 kutoka sehemu moja hadi nyingine, mlemavu, yule ambaye angestahili kueleweka na kusaidiwa zaidi, anatozwa Kshs80 kwa safari ile ile. Huu ni ubaguzi ambao haueleweki! Ungefikiri kwamba kama kuna kubagua, ni kubagua ili umsaidie mnyonge. Lakini hapa mlemavu anabaguliwa na kulazimishwa kutoa pesa zaidi anaposafiri. Sikujua hilo jambo, lakini ni tatizo kubwa linalostahili kushughulikiwa, si tu na Serikali lakini pia na wale ambao wanamiliki magari ya usafiri. Ni lazima waache kuwabagua walemavu. Jambo lingine ni kwamba katika Jiji hili letu utakuta kwamba, kwa sababu walemavu hawawezi kupata kazi afisini--- Walisema kwa kweli wakijaribu kwenda afisini mwa mtu kuomba kazi, wakati mwingine hata hufukuzwa. Wanaambiwa: \"Nyinyi si watu wa wakuja hapa afisini. Tokeni!\" Kwa hivyo, ili wapate riziki yao, wengi wao wanajishughulisha na kazi ya uchuuzi. Wengi wao ni wachuuzi wa bidhaa hapa mjini, lakini kwa bahati mbaya wakipatikana wakichuuza, badala ya kusaidiwa na askari, wananyang'anywa hata viti vyao na kuwekwa korokoroni. Sasa wewe waza: Wewe unatembea kwa kiti cha magurudumu, halafu unakinyang'anywa na askari, utarudije nyumbani? Ukienda kwenye kituo cha polisi cha Central, utakuta mlima wa mikongojo iliyonyang'anywa walemavu wakati wa hekaheka za kuwatoa mitaani wasichuuze. Unakuta viti viko pale ambavyo vimenyag'anywa walemavu. Ukimnyang'anya mlemavu kiti, atapata wapi pesa za kununua kiti kingine? Ni kama unataka wafe kwa sababu hawezi kutoka nyumbani. Hana namna ya kutembea. Hili ni jambo ambalo silielewi. Sijui ni kwa nini askari wetu hawafunzwi kwamba kuna tofauti kati ya walemavu na watu wazima. Huwezi kumnyang'nya mlemavu kiti chake au mkongojo wake na wakati huo useme kwamba unamsaidia. Watu hawa wangeruhusiwa kuuza bidhaa zao bila kusumbuliwa. Wakati watu wazima wanafukuzwa, walemavu wanafaa kueleweka vizuri. Lakini badala ya kusaidiwa, wanasukumwa vile nilivyoeleza. Kwa bahati mbaya, mhe. Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Nyumbani ameondoka. Nilikuwa nikitaka kusema kwamba walemavu wanafaa kuwa na jela zao kwa sababu wakiwekwa katika jela moja na watu wazima - kule ni jehanamu. Kila mtu na lake - hawawezi kuwa na amani. Watasumbuliwa na wafungwa walio na nguvu. Hataweza kutoka katika jela hilo kwa sababu utakuwa umempa hukumu ya kifo. Kwa hivyo, natumai kwamba Makamu wa Rais atalifikiria jambo hilo na kuona vile anaweza kujenga magereza maalum ya wafungwa walemavu. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni ajabu kwamba kuna wanaume ambao hufanya mapenzi na walemavu ambao huomba katika miji yetu na kuwatia mimba, kisha wanawaacha. Utakuta mlemavu ambaye anatembea na kiti ana watoto. Ukimuuliza alivyopata watoto hao, utapata kujua kwamba wengine walinajisiwa na waliofanya kazi hiyo mbovu hawawasaidii. Nadhani kuna umuhimu wa kufundisha wanaume wa nchi hii utu ili waache kufanya vitendo ambavyo matokeo yake ni mabaya sana. Ningetaka kushukuru mashirika ya kimataifa ambayo yanawanunulia walemavu viti, mikongojo na vifaa vingine ambavyo wanahitaji. Hilo ni jukumu ambalo Serikali ingejitwika badala ya kungojea watu wa nje waje kuwanunulia walemavu wetu viti na vitu vingine vya kutembelea. Kusema kweli, hiyo ni aibu kwetu. Jambo lingine ambalo ningetaka kuomba ni kwamba, Serikali, katika kutatua matatizo ya walemavu, ifikirie sana kuhusu kutembelea nchi zile za Scandinavian ambapo walemavu wanatunzwa vizuri. Niliishi huko na nilishangaa kabisa kwa sababu haungepata mlemavu ambaye 2242 PARLIAMENTARY DEBATES July 4, 2007 amekosa elimu. Walemavu wanashughulikiwa kwanza kabla ya watu wengine. Huwezi kupata mlemavu asiye na kazi katika nchi ya Norway. Niliishi huko miaka mingi na sikuona mlemavu hata mmoja akitafuta kazi. Walipomaliza masomo yao, walikuwa wakipata wametengewa kazi tayari, na kazi yao ilikuwa kuifanya tu. Walemavu wanaposafiri pale, wao hutozwa nauli ambayo ni nusu ya ile watu wazima wanatozwa. Mahali kwingi, wao husafiri bila kutozwa nauli kwa sababu hali yao inaeleweka. Huwezi kukutana na mlemavu akiomba. Nimezunguka nchi hiyo na sikukutana na mlemavu yeyote akiomba chakula au pesa mitaani. Wote wameshughulikiwa ili wapate kazi na kila kitu. Naomba kuunga mkono."
}