GET /api/v0.1/hansard/entries/216068/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 216068,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/216068/?format=api",
"text_counter": 419,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kusema ya kwamba kuhusiana na jambo la nidhamu la Bw. M. Kilonzo, yale maoni yote ambayo yametolewa hapa, ni maoni ambayo yangetolewa katika mjadala. Kusema ukweli, wale waliongea walikuwa wanajadili Mswada huu. Hawana jambo ambalo kwa kweli ni tatizo la kikatiba. Isitoshe, Wizara yetu, wakati wa kutayarisha Mswada huu, ilipata ushauri kutoka kwa Mkuu wa Sheria kuonyesha ya kwamba hakuna chochote kilichomo katika Mswada huu ambacho ni kinyume cha Katiba. Kwa hivyo, mwanasheria mwingine akisimama hapa abishane na huo ushauri, basi nadhani jibu ni watu kufikishana mahakamani, lakini sio kuzuia mjadala uendele. Sioni ni kwa nini maoni ya Bw. M. Kilonzo yawe ni muhimu kuliko yale ya Mkuu wa Sheria, na wote wawili ni mawakili. Kukiwa na ubishi na kutofahamiana kati ya maoni yao, uamuzi utakuwa wa mahakama. Lakini sio sisi wenyewe kwa wenyewe tubishane. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukweli ni kwamba hakuna uhuru usiokuwa na mipaka. Hata Katiba yetu haisemi ya kwamba kuna aina za uhuru ambazo hazina mipaka hata kidogo. Tumeambiwa na wataalamu wa kidemokrasia kwamba huwezi ukasimama katika sinema ukasema, \"kuna moto\", na hakuna moto! Ukifanya hivyo, utakuwa unaingilia haki za watu wengine. Lazima tuelewe ya kwamba Katiba inatoa haki kwa kila mtu. Lakini hakuna mtu ambaye haki zake zinaweza kutekelezwa huku zikiathiri haki za mwingine. Bw. Naibu Spika wa Muda, yale waliongea ni maoni. Msimamo wetu ni kwamba ni afadhali waombe nafasi ya kutoa maoni hayo wakati tunajadili. Lakini sio kujaribu kusimamisha mjadala wenyewe au kupitishwa kwa Mswada."
}