GET /api/v0.1/hansard/entries/216690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 216690,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/216690/?format=api",
    "text_counter": 98,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Hoja hii muhimu ya Bajeti. Tangu mwanzo kitu ambacho kimenipendeza zaidi katika hii Bajeti ni kwamba inategemea kidogo sana pesa kutoka kwa wafadhili. Nafikiri tukiwa na huo mwenendo wa kuhakikisha kwamba Bajeti yetu inategemea rasilmali zetu za ndani, nafikiri hapo tutakuwa tunaendelea vizuri sana kwa sababu uchumi wetu hauwezi kuyumbishwa yumbishwa na siasa kutoka kwa wafadhili kutoka nchi za nje. Ni muhimu kwa Serikali, Bunge na Wakenya kwa jumla kutoa sauti kali kabisa kwamba hili deni kubwa ambalo tunabebeshwa na wabeberu iondoke. Serikali yoyote ya Magharibi ambayo inasema kwamba ni marafiki ya Wakenya haiwezi kuendelea kusema kwamba ina urafiki na Kenya wakati ambapo nchi yetu inabebeshwa deni kubwa sana ambalo tunalipa. Kama deni hilo lingekuwa limeondolewa, nafikiri Bajeti hii yetu ingekuwa inaendelea vizuri zaidi. Kwa vile sasa tuna Kamati ya Bajeti ya Bunge, ni muhimu katika siku za usoni Bunge lihusishwe, kutoka mwanzo, katika kuandika Bajeti. Haitoshi tuje hapa kupiga debe na kusifu Bajeti na tunajua kwamba hatuwezi kubadilisha chochote ndani ya Bajeti. Kwa hivyo, tunajua kwamba katika siku za usoni, ambazo zinaweza kuja, tunatarajia kwamba Bunge itahusishwa kutoka mwanzo katika kuandika na kuadhiri swala la Bajeti. Hofu yangu ni kwamba tunasema kuwa tunakusanya kodi nyingi zaidi na tunatengeneza Bajeti na pia mojawapo za hela tutazipata kutoka kwa kubinafsisha mashirika ya umma kama posta na huduma nyingine za simu. Uchumi wa kimataifa umefanywa na wasomi, wazalendo Wafrika na wale ambao wanaingilia mambo ya kiuchumi kwa undani. Sijui kama Mawaziri wa mipango na fedha wanasoma. Lakini, tunafanya yale makosa ambayo wengine wanarekebisha. Tukiangilia huko America ya Kusini imekuwa ni uwazi. Uchumi utaendelea ikiwa sekta ya fedha itapewa kipaumbele. Tukisema kwamba tutauza kila kitu na kubinafsisha--- Tukibinafsisha, tunawanufaisha matajiri wa ndani na vile vile wabeberu kutoka nje. Uchumi hauwezi kukua. Bajeti haiwezi kukua. Ni muhimu kwa Bajeti kukua kwa sababu kuna mipango halisi ya kiuchumi. Lakini mipango ya kiuchumi ambayo inafanya uchumi wa nchi yetu utawaliwe na watu kutoka nje au matajiri walioko huko juu na pesa haziwafikii watu maskini, hiyo haiwezi kutuokoa. Watu kutoka Latin America walijifunza kutoka hayo na sasa, badala ya kubinafsisha mashirika yao, wanayafanya kuwa mikononi mwa Serikali na wananchi. Lakini huku kwetu, tunafanya kinyume. 2058 PARLIAMENTARY DEBATES June 27, 2007 Tunaendelea kubinafsisha na kufanya yale makosa ambayo wengine walifanya zamani. Tunarudisha makosa hayo hapa. Sidhani kwamba nchi hii itaendelea kuongeza nafasi za kazi, kuongeza ajira, kupunguza umaskini, kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini ikiwa itaendelea na hizi sera za kiuchumi za kipebari na ubinafsishaji. Kufanya hivyo hakuwezi kutupeleka mbele. Bw. Naibu Spika wa Muda, China iliendelea mbele kwa sababu ya kuweka misingi imara ya kiuchumi ya kisoshelisti. Na hivi sasa, ndio wamegundua na kuuhurisha uchumi wao. Lakini miundo msingi yote ya kiuchumi iko mikononi mwa watu wa China ambao wameidhibiti kabisa. Sasa hivi, nchi za Kusini Mashariki mwa Asia zina misingi kama hiyo. Misingi yao ya dola ilikuwa ni muhimu sana katika kuchangia uchumi wa nchi hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunasema kwamba Bajeti imesifiwa sana. Ilikuwa Bajeti wa kuwaangalia maskini na kuwasaidia watu wengi. Lakini la muhimu zaidi ni utekelezaji. Mimi nimeona, miaka nenda, miaka rudi, tunafanaya Bajeti. Lakini mitaa ya mabanda huko Kibera, Korogocho na Mathare inazidi na inaendelea kuwa ile ile. Nitakiangalia kipimo cha hii Bajeti. Wananchi watapima na waulize: \"Je, baada ya kutengeneza hii Bajeti, mitaa ya mabanda imepungua ama imeongezeka? Pengo kati ya matajiri na maskini limepanuka zaidi ama limepungua zaidi?\" Nasema hivyo kwa sababu hii Bajeti imewekwa katika msingi wa mipango ya kiuchumi ya kipebari. Nafikiri hata tukiambiwa uchumi umekua, utaendela kukua kwa wale wachache ambao wako juu, yaani wale matajiri. Ile sehemu nyingine ya wananchi haiwezi kufikiwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, utekelezaji wa hii Bajeti ni lazima uangalie haki katika nchi. Tunazungumza kwamba Bajeti imetengenezwa kuboresha maji. Lakini huku ndani, hatujaona mpango wa Serikali wa maji hata kidogo. Karibu miradi yote ya maji ambayo inatekelezwa katika Wilaya ya Taita-Taveta inatumia pesa za Constituencies Development Fund (CDF). Hakuna mradi wa maji kutoka Wizara ya Maji katika Wudanyi. Kumekuwa na ubaguzi mkubwa sana. Sehemu nyingine za nchi zinapewa Kshs500 milioni kwa wilaya mzima. Sehemu nyingine zinapewa Kshs400 milioni. Wilaya ya Taita-Taveta imepewa Kshs5 milioni kutoka Wizara ya Maji. Hiyo Kshs5 milioni ni ya wilaya yote na sehenu nne za uwakilishi Bungeni! Hizo pesa hazitoshi kutekeleza miradi ya maji. Ufisadi ambao unaendelea katika Wizara ya Maji, hasa katika ngazi ya wilaya ni pingamizi kubwa ambayo inazuia maendeleo. Kwa hivyo, lazima kuwe na haki. Haiwezekani kwamba Mkoa wa Pwani unatoa karibu Kshs60 bilioni za kodi kila mwaka, lakini hatuoni chochote. Hatuoni chuo kikuu. Hatuoni miradi ya maji ikiendelea na mambo mengine yanafanywa huko nje. Ni lazima kuwe na haki. Ndio tunasema sisi watu wa Pwani tunangojea Katiba mpya nyenye msingi wa Bomas, ambapo kutakuwa na usambazaji wa mamlaka na mipango ambayo itagawa nchi yetu kimajimbo. Bw. Naibu Spika wa Muda, na wakati huo huo, tukizungumzia uchaguzi unaokuja, ni muhimu kuwe na mabadiliko maalumu muhimu ya Katiba. Haswa, ili mtu awe Rais, ni lazima apate zaidi ya asilimia 51. Sijui ni kwa nini watu wanaogopa jambo hilo. Hata kusema Bunge litahairishwa ni kujaribu kuhujumu juhudi za wale watu ambao wanataka kuleta mabadiliko ya kimsingi ya Kikatiba. Nasema kwamba, ili nchi iendelee vizuri, hayo mabadiliko ya kimsingi ni lazima yawepo mwaka huu. Bunge hili litakuwa limechangia hayo. Hata ikiwa uchaguzi utahairishwa, ni sawa. Muhimu zaidi ni mabadiliko ya kimsingi ya Kikatiba yatokee, hasa kile kifungu kinachosema kwamba ili mtu awe Rais, ni lazima apate zaidi ya asilimia 51 ya kura zote. Bw. Naibu Spika wa Muda, usalama ni jambo muhimu. Lakini Waziri wa Usalama asitumie ofisi yake kupambana na watu ambao anawaona ni maadui wake. Sioni ni kwa nini watu wengine wanyang'anywe ulinzi wa polisi wakati tunajua mtu ambaye ameongoza maandamano ya mungiki hapa katika nchi yetu. Halafu, inasemekana watu wengine wamenyang'anywa ulinzi. Na wale watu ambao wanafanya hiyo wanajulikana. Watu ambao wamekula kiapo wamesemwa hapa. June 27, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2059 Halafu wanachaguliwa wengine wachache kutelekeza visasi vya kibinafsi. Halafu wananyang'anywa ulinzi huo. Ndiyo nasema hapa kwamba njama hizo sisielewi. Ukiwa Waziri, ni lazima Bajeti itengenezwe ya kuangalia usalama wa kila mtu. Sio kuangalia usalama wako mwenyewe na marafiki zako, na kuuondoa usalama kutoka kwa wengine ambao hukubaliani nao. Vile vile, wakati tunaangalia usalama, lazima tuhakikishe kwamba kuna usawa wa kisheria. Lazima tuhakikishe kwamba hatuvunji haki za kibinadamu. Hakuna mtu anataka kuvunjwa kwa sheria. Hakuna mtu ambaye hataki usalama wa wananchi. Lakini yule ambaye analenga maskini katika mitaa ya Mathare na Korogocho, eti anapambana na umaskini huku anakanyanga akina mama--- Na huku unavunja nyumba za watu na kuwauwa bila kuwapeleka mahakamani au kujua ikiwa kweli ni wahaalifu--- Nafikiri huo hautakuwa mfano mzuri katika nchi yetu ya Kenya. Kuwa ujumla, wakati nazungumzia swala la uchaguzi wa mwaka ujao---"
}