GET /api/v0.1/hansard/entries/216704/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 216704,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/216704/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Chiaba",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Livestock and Fisheries Development",
"speaker": {
"id": 3,
"legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
"slug": "abu-chiaba"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi niungane na wenzangu ili niweze kuichangia Hoja juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Pesa za Serikali ya mwaka wa 2007/2008. Kwa kawaida Serikali husoma Makadirio hayo, lakini kitu muhimu cha kutilia mkazo ni kuhakikisha kwamba sehemu zote za uwakilishi Bungeni humu nchini zimepata maendeleo ya kisawasawa. Ijapokuwa sisi watu wa Lamu tumeweza kupiga hatua na kupata maendeleo ya kutosha katika kipindi hiki cha uwakilishi Bungeni, bado kuna mambo mengi ambayo tunayatarajia. Kwa mfano, masuala ya maji hayajazingatiwa kikamilifu katika Makadirio haya na Makadirio yaliyopita. Kuna sehemu nzuri za kuanzisha miradi ya maji ili maji yaweze kupatikana kwa matumizi ya watu wa Lamu Mashariki. June 27, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2067 Watu wa Lamu Mashariki hutumia maji ya mvua. Maji ya mvua yakikosekana, huwalazimu wakazi wa sehemu hiyo kwenda kutafuta maji Kisiwani Lamu, mwendo ambao huchukua masaa sita kusafiri kwa mashua. Kwa hivyo, ninataka kuisisitizia Wizara inayohusika, pamoja na Wizara ya Fedha, itenge pesa za kutosha ili watu wa sehemu hiyo, ambao wanapenda amani, waweze kupata maji. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa muda wa miaka 43 tumekuwa tukizungumzia suala la barabara ya kwenda Lamu. Wakati umefika. Mvua iliyonyesha katika sehemu hiyo hivi majuzi imeharibu barabara zote, na watu hawawezi kusafiri kwa usalama unaostahili. Nikizungumzia usalama humu nchini, inaonekana kwamba kila tukikaribia wakati wa uchaguzi, makabila fulani huwa yako tayari kutumia mabavu, au kutumia mbinu zisizoambatana na sheria, ili kuwaogopesha watu wanaoishi katika sehemu nyingine. Mfano ni yale mapigano ya kikabila yaliyotokea katika sehemu kadhaa humu nchini katika miaka ya 1992 na 1997. Kwa hivyo, tunaiomba Serikali iwe macho ili huu muda uliobakia kabla ya uchaguzi mwakani, kusitokee mambo kama hayo. Mambo kama hayo huiletea nchi hii sifa mbaya, na kuwafanya watu wanaotaka kuleta raslimali humu nchini washuku kwamba raslimali zao hazitaweza kulindwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo ningependa kuongezea linahusu Mswada juu ya marekebisho kiasi ya Katiba, ambao tunautarajia Bungeni. Mimi sioni kwamba ni sawa kwamba eti kwa sababu tunataka kufanya marekebisho kiasi ya Katiba, ni lazima kipindi cha Bunge hili kiongezwe hadi mwaka ujao. Ninaamini kwamba katika miezi hii mitano iliyosalia, tunaweza kupitisha sheria zote kuhusu marekebisho hayo na kura ipigwe katika mwezi wa Desemba au kabla ya Desemba ili tuweze kuingia katika hicho kipindi kingine kama kawaida. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}