GET /api/v0.1/hansard/entries/216986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 216986,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/216986/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Moroto",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of Vice-President and Ministry of Home Affairs",
"speaker": {
"id": 318,
"legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
"slug": "samuel-moroto"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza, nataka kuanza kwa kushukuru kazi ambayo imefanywa na Serikali kwa muda mdogo uliopita. Ningetaka kuanza na wilaya mpya ambayo tumepata kama watu wa Pokot. Bw. Naibu Spika, imekuwa ni njia moja ya kuleta utawala karibu na watu. Sasa, tuna Wilaya ya Pokot North ambayo imekuwa sehemu ya Uganda kwa muda mrefu. Katika mwaka wa 1970, sehemu hiyo ilitolewa Uganda na ikawa sehemu ya Kenya. Ni sehemu ambayo ilikuwa imesahaulika kimaendeleo. Eneo la West Pokot kwa jumla ni sehemu ambayo, kwa muda mrefu, imebaki nyuma kimaendeleo. Watu katika sehemu hiyo wamekuwa wakiuliza, miaka nenda, miaka rudi, misaada ya chakula. Tunajua huenda ikawa jambo ambalo limefanyika linaweza kuwapa wale watu matumaini kwamba mafanikio yanaweza kuwafikia."
}