HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 216988,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/216988/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Moroto",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of Vice-President and Ministry of Home Affairs",
"speaker": {
"id": 318,
"legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
"slug": "samuel-moroto"
},
"content": "Hata hivyo, Bw. Naibu Spika wa Muda, mshangao wangu, na nataka Waziri anayehusika 2116 PARLIAMENTARY DEBATES June 27, 2007 na wale wengine ambao wako hapa wajue. Wakati Mhe. Rais anakuja na watu wanamuuliza, anawajibu kwa kuwapatia matakwa yao. Lakini wale ambao wanahusika na kuwasaidia watu kwa karibu wanaenda mwendo wa kinyonga. Bw. Naibu Spika wa Muda, hali ya barabara katika wilaya hizo mbili, yaani Pokot North na West Pokot, kuna sehemu ambayo tangu dunia iundwe, ama Kenya ipate uhuru hadi sasa, haijui kitu inayoitwa barabara. Hata watoto wakiona gari--- Hata sio watoto! Hata watu wazima! Hata hawajui kitu kinachoitwa Serikali. Wanajua tu vile wanakaa na vile wanaishi. Mshangao wangu ni kwamba, ukiangalia makadirio ya mwaka huu, pesa ambazo zimepeanwa na Wizara ya Barabara kushughulikia sehemu hizo ni ndogo mno. Hiyo ni kama kutuambia: \"Nyinyi katika sehemu hizo hamstahili kuwa katika Kenya.\" Wamepeana Kshs22 million. Hata hiyo Kshs22 million imegawa kwa wilaya mbili. Zimegawa tena kwa barabara ambazo hata ukipeleka gari lako huko, halitaweza kupita. Viongozi wamekaa kupitia kwa DDC na wametuma mapendekezo ya sehemu hizo. Nilishangaa jana wakati Waziri alijibu Swali hapa akasema kwamba zile pesa mumenipa--- Hata unaweza kumhurumia huyo Waziri. Kwa hivyo, lazima Wizari wa Fedha na yule wa mipango watuambie wana malengo gani ambayo yanawafanya wasahau sehemu hizo. Wakati mwingi, unapata kwamba wale watu au Wanakenya ambao wanaishi katika sehemu kavu ni watu ambao wanapigana na majirani wao mara nyingi. Hata katika eneo la Pokot, wakati mwingi, tunaingia Trans Nzoia na kwingine. Mapigano hayo yanasababishwa na ukosefu wa maji. Sisi ni wafugaji na ng'ombe wetu wanahitaji maji. Wakati mwingi, tunahama ili wanyama wetu wasitaabike. Hata mwaka uliopiata, tulipewa Kshs59,500,000. Lakini mpaka sasa, hakuna kitu kilifanyika. Hata Waziri alifika na akazunguka huku na tukamshukuru. Hata aligombana kidogo lakini alipotoka--- Mimi sijui! Ni kama watu wake walikuwa wanasema: \"Wewe enda! Sisi tutanyorosha kazi nyuma.\" Mpaka sasa, hakuna kitu kimefanyika. Jambo kama hilo linaharibu sifa ya serikali. Wakati tunasema Serikali inajaribu kufanya hivi, watu wanasema: \"Imefanya nini?\" Mwito wangu mwaka huu ni kwamba, Mawaziri ambao wanahusika wajaribu kufanya bidii. Nasema kwamba Rais amejaribu. Wakati alienda sehemu hizo, watu waliuliza na akakubali kuwasaidia. Lakini wale ambao wanamsaidia ndio wako na shida. Ni lazima tuketi kuona tutafanya nini. Hata hivyo, ukiangalia katika makadirio ya mwaka huu, utaona kuna ukosefu wa kupeana mali kwa usawa. Sehemu zingine bado zinapata kuliko zingine. Na utaona sehemu hizo ni zile ambazo zimeendelea. Kwa hivyo, nasema kwamba Mawaziri ambao wapepewa jukumu la kuona kwamba Wakenya wamehudumiwa vilivyo wachukue nafasi hiyo, wazunguke kila mahali ili watu wajue kuna Serikali. Nikimalizia, vile nchi inaendelea, kuna mambo ya usalama. Hivi majuzi, kuna ng'ombe walichukuliwa na wakapelekwa Uganda. Mpaka sasa--- Na Waziri alisimama hapa na akasema aliongea na mwenzake--- Mimi sasa sijui tunalisha mali na kupeleka nchi nyingine! Wakati watu wetu wanaruka na kwenda upande ule mwingine, wanakaziwa na wanarudishiwa. Tukiangalia mambo ya usalama na haya mambo ya Mungiki, hatujui ni nini inaendelea. Kwa sababu watu wanachinjwa hata mchana na hakuna kitu ambacho kinafanyika. Nataka kufananisha kwa sababu jambo likifanyika sehemu nyingine, kwa mfano pahali mimi natoka, hata mbuzi mmoja akiibiwa, jeshi linatumwa kwenda kumtafuta huyo mbuzi mmoja ambaye amepotea! Lakini hivi majuzi, maisha ya mwanadamu--- Watu wanachinjwa mchana na usiku! Hali hiyo inakaa namna gani? Hatuwezi kusema ni Serikali peke yake. Hata upande ule mwingine. Lazima tutie bidii kama Waheshimiwa na kuona kwamba watu wamepata ujumbe wa kuweka usalama. Kwa sababu huenda ikawa sasa hivi, ni mambo ya siasa inaendelea. Huenda ikawa Serikali inafanya bidii, na wengine wanaenda kichini chini. Sasa, huwezi kujua hiyo kitu inaishia wapi. Inashinda mawazo ya wengine. Jambo linafanyika na hakuna kitu kinaendelea. Hata leo huko Naivasha, gari la polisi linapigwa mchana June 27, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2117 saa saba! Kwa hivyo, lazima watu waketi waone namna wanaweza kusaidiana, ili usalama urudi na watu waendelee kwa njia mzuri. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}