GET /api/v0.1/hansard/entries/217182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 217182,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/217182/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Karume",
    "speaker_title": "The Minister of State for Defence",
    "speaker": {
        "id": 234,
        "legal_name": "Njenga Karume",
        "slug": "njenga-karume"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili niseme machache kuhusu Bajeti ya mwaka huu. Namshukuru Waziri wa Fedha kwa kutusomea Bajeti ya maana sana. Hii ni Bajeti ya maana kwa sababu imewasaidia watu wasio na uwezo, na hiyo ndio maoni na upendo wa Serikali hii inayoongozwa na Rais, Mhe. Mwai Kibaki. Vile vile, namshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa hii kazi ya maana aliyofanya kwa muda mfupi. Nasema \"kwa muda mfupi\" kwa sababu alipochukua usukani, kila mtu aliye hapa katika nchi ya Kenya anajua mambo yalikuwa namna gani; tunajua barabara zilikuwa namna gani. Wakati huo, hakuna barabara ilikuwa inatengezwa na kuwekwa lami na zile zilizokuwa na lami hapo mbeleni, zilikuwa zimekwisha kabisa na zikawa za mchanga na murram . Lakini kutoka Serikali hii ichukue uongozi, ikiongozwa na Mhe. Kibaki, tumeona kuwa katika karibu kila wilaya kuna barabara moja au mbili zinatengenezwa na kuwekwa lami. Hii ni kuonyesha vile Serikali inafanya kazi ya maana. Bw. Naibu Spika, nikikumbuka, kama ni mambo ya health, hapo mbeleni kama ungalienda katika hospitali ya rural area, hata huko kwetu Kiambu, hungepata dawa. Hata kama pengine umetakiwa ulale kwa hospitali hata blanket haikuwa. Na ukitakiwa uwe na karatasi ya kuandikiwa dawa, ilikuwa mpaka uende kununua karatasi yako mwenyewe uje nayo uandikiwe dawa kwa sababu hakuwa na chochote. Hii inaonyesha vile Serikali hii imefanya kazi. Ukiangalia mambo ya maji wakati huu, hata ukienda West Pokot au North Eastern, utakuta Serikali inachimba boreholes, dams na mambo mengine kama hayo. Hii ndio sababu hata hii Bajeti unaona ikienda namna hiyo kwa sababu ya uongozi tulionao wakati huu. Ukiangalia mambo ya ukulima, yalikuwa yameharibika sana wakati huo. Hata kahawa ilikuwa imekwisha, mahindi yalikuwa yakikuzwa na kununuliwa kwa bei ya chini na wakiyauza hata hawakulipwa hapo hapo. Wakati huu inanunuliwa kwa bei ya juu na wanalipwa. Hata KCC ilikuwa imekwisha na ikanunuliwa tena na Serikali; sasa ni ya wakulima, na watu wale walio na ng'ombe wananunuliwa maziwa kwa njia bora. Hiyo ni kuonyesha vile Serikali imefanya kazi, ndio sababu hata tunasema mambo ya Bajeti yanaendelea sawa sawa. Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, mimi kwangu ninashukuru Serikali hii kwa kazi bora ambayo imefanya, na kwa sababu haikukuta kitu hata kidogo. Kwa hakika, ingawa tunajua kuna watu wengi sana ambao hawana kazi, especially younger people, lakini Serikali imejaribu na watu wengi wamepata kazi. Ukiangalia upande wa utalii, ulikuwa umekwisha. Watu walikuwa wanafutwa kazi, mikahawa ilikuwa imefungwa kule Pwani, na sasa mahoteli yamefunguliwa tena na yameandika wale watu ambao walikuwa hawana kazi, na mengine yanajengwa wakati huu kwa sababu ya vile Serikali inafanya kazi na vile inaendelea. Kwa hivyo, tunasema ni vizuri na tunajua hata wananchi hayo ndiyo maoni yao. Tungeombea hii Serikali irudi tena miaka mingine mitano ili mambo yatengenezwe sawa sawa. Tunaona kwa kweli, hata wageni wameanza kurudi hapa kuleta investments zao, kwa sababu wanaona vile Serikali inafanya; ni Serikali ya haki na wanaona vile mambo yanaendelea. Hii ndiyo sababu watu wameanza ku-invest pesa katika Kenya. Hayo ndiyo mambo tunayofikiria, na tunataka kuendelea na Serikali kwa sababu tunaona vile imeangalia watu wote. Vile vile, Serikali hii ilianzisha Wizara mpya, ya youth, ya kusaidia vijana, kwa sababu vijana wetu wengi hawana kazi. Hawawezi kufanya biashara kwa sababu hawawezi kupata mikopo kwa benki, kwa sababu hawana security ; hawana title deeds za mashamba au za nyumba ili wajaribu kuomba loans kutoka banks . Hii ndiyo sababu Serikali imeanzisha hii Wizara mpya ya kusaidia wananchi., Ni vizuri tufikirie young people katika nchi hii ili tuone wamepata kazi, kwa sababu walikuwa hawapati kazi kwa sababu viwanda vile vilikuwa vimekwisha, na bila viwanda si rahisi kazi kupatikana. Bw. Naibu Spika, ningetaka kusema machache kuhusu mambo tunayozungumza kuhusu Katiba kila wakati. Ningesema kwa maoni yangu tumejaribu kupata Katiba karibu miaka 15. 2028 PARLIAMENTARY DEBATES June 26, 2007 Tumejaribu kwa muda mrefu, tunajaribu, wananchi, wakati mwingine, wanaikataa. Kwa mfano, mwaka wa 2005, tulijaribu tukazunguka nchi hii kuzungumza na wananchi wakati wa referendum tukiwauliza wananchi wakubali tu-change Katiba ili tuwe na Katiba mpya. Wananchi walikataa; walisema hawakutaka mambo ya Katiba. Hata hawakutupatia ruhusa tukirudi kwa Bunge kuwa na"
}