GET /api/v0.1/hansard/entries/217635/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 217635,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/217635/?format=api",
    "text_counter": 272,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Ndile",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Tourism and Wildlife",
    "speaker": {
        "id": 272,
        "legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
        "slug": "kalembe-ndile"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii fursa ili nami nitoe maoni yangu. Ningependa kusema kwamba Bajeti ya mwaka huu ilikuwa nzuri zaidi ikilinganishwa na ile ya miaka iliyopita. Kwanza, Bajeti hiyo imewapa akina mama pesa. Ukimpa mama pesa, kwa mfano, yule anayeuza tomato, itamsaidia. Si rahisi kwa akina mama kufanya biashara zao zianguke. Wao ndio wametusomesha kwa kutumia pesa zile kidogo ambazo wamepata. Pia, wamesomesha hata mabwana na watoto wao. Sijasema kuwa vijana wasipewe pesa lakini ninashukuru kwa kuwa wanawake wamepewa pesa ili wajue kufanya biashara. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lilonifurahisha zaidi ni kuwa Bajeti hii imemlenga maskini. Hii ni mara ya kwanza kuona Bajeti ikizungumzia mambo ya maskwota. Hili ni jambo ambalo limenifurahisha sana. Jambo ningemuuliza Waziri ni kuhakikisha kuwa amezitumia pesa ambazo zimetengewa maskwota vizuri. Kuna watu ambao walifukuzwa kule Molo na pale kuna shida ya maskwota. Sehemu nyingi zina shida ya maskwota. Pesa hizi zilizotengwa mwaka huu zikitumiwa vizuri, na mashamba hayo yasije kutolewa kwa matajiri, uchumi wa nchi hii utaimarika zaidi. Hata ugonjwa wa UKIMWI utapungua kwa sababu watoto ambao wamezaliwa katika jamii ya maskwota; wasichana na wavulana, ambao mwishowe hawana kazi ni kama wametengwa. Ndio sababu unaona wanafanya vituko ili wapate riziki. Lakini wakipewa pesa na shamba, maisha yao yatabadilika. Ukiangalia mambo ya Wizara ya Utawala na Usalama, tunataka kuona polisi wakiwa macho kabisa. Tujiulize, sisi kama viongozi, \"ni nini mbaya?\" Kuna wakati polisi walikuwa wakipewa magari aina ya Mahindra. Wananchi walikuwa wakisema mtaani kuwa gari aina ya Mahindra halingeweza kumkimbiza mwizi. Gari hilo likianza safari na mwizi aanze baadaye, yule mwizi angeweza kulipita gari hilo. Leo polisi wana magari ambayo hayajawahi kuonekana. Wanatumia Toyota Rav4 na Toyota Land Cruisers. Tunataka kuona kazi ikifanyika na uhalifu ukipungua. Bw. Naibu Spika wa Muda, nafikiria kuna shida mahali. Wakati wananchi walitupatia uongozi, tukiongozwa na Mhe. Rais, kulikuwa kuzuri sana kwa miezi sita ya kwanza. Polisi walikuwa hawachukui hongo. Leo kutoka hapa hadi Kibwezi kwangu, kuna road blocks karibu kumi ama 20. Ni kitu gani wanafanya? Ukiangalia, utaona matatu zinasimamishwa, lakini zinapita tu! Malori pia yanasimamishwa halafu yanapita na hayaandikiwi kesi. Basi tujiulize swali moja: Ikiwa hakuna kesi wanazoandikiwa, si polisi wa trafiki wapewe kazi ile nyingine ya kawaida ya kuwakimbiza wezi? Ikiwa kutakuwa na ajali, ni jukumu la manusura kupiga ripoti katika kituo cha polisi halafu polisi waende wakapime na warudi kituoni. Tusipofanya hivyo, tunawaharibu polisi na watu wetu. Hilo ni jambo ambalo tunafaa kuangalia. Nimeambiwa hadithi moja na nimewauliza, Wabunge wa Uganda, ambao waliniambia kuwa hali ilikuwa kama hii iliyoko Kenya. Lakini Bw. Museveni alichukua hatua na kuwaambia: \"Polisi, hamuandiki kesi na magari hayaandikiwi makosa. Basi haina haja mkae hapa!\" Akawaondoa barabarani na siku hizi hawako tena. Walikuwa wabaya zaidi kuliko polisi wa Kenya. Sasa wamekuwa watu wazuri. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni lazima tujuilize ni kwa nini tumeachwa nyuma. Tulipochukua Uhuru, tulikuwa na Kicomi na Thika Textiles - ijapokuwa hatutaki kurudi huko - na Kenya Co-opertative Creameries (KCC). Serikali yetu imeanza kufufua hivyo viwanda na hiyo ni hatua moja ambayo tunapiga. Lakini tunaweza kupiga hatua zaidi ikiwa sisi sote tutaweka nchi yetu mbele. Katika Bajeti hii kuna kitu kidogo ambacho Waziri hakukifikiria - ijapokuwa natumaini atafikiria zaidi - na ni juu ya magari makuukuu. Je, ni nani ana magari kuukuu? Ni masikini Ndile; ni skwota mwenzangu, kama ana bahati, na yule maskini mwingine. Ni nani ana magari mapya? Labda uwe Mbunge kama mimi! Lakini ikiwa tunataka uchumi wetu uimarike na mwananchi wa 1958 PARLIAMENTARY DEBATES June 20, 2007 kawaida anufaike na kujisikia kuwa Mkenya, tungeongeza bei ya magari mapya na ya magari kuukuu iachwe angalau hata maskini akifa, awe ameendesha gari hata kama ni kuukuu! Kodi ya magari makuukuu imeongezwa. Nataka pia kusema kuwa gari la masikini linatumiwa mitaani kwa kutumia spare parts ambazo tumetoa kwa magari mengine makuukuu na hatuharibu barabara. Wanaoharibu barabara ni wenye malori makubwa na ambao ni matajiri. Waziri amejaribu, lakini wakati mwingine yafaa azingatie jambo hilo. Bw. Naibu Spika wa Muda, majaji wanalipwa pesa nyingi na wanafika ofisini saa nne na huwezi kuwajibu. Ikifika saa tano, wanaenda kunywa chai na kesi zimejaa kortini ilhali wanapata mshahara mkubwa. Kuna mzee wa kijiji ambaye anaamua kesi ambazo hata hazifiki kortini. Anakaa katika kikao kimoja mpaka saa kumi. Kesho yake anaamkia pale pale kutatua kesi zingine. La sivyo, tungekuwa na vijiji ambamo watu wanapigana. Lakini wazee wa vijiji wanafanya kazi ngumu sana. Nataraji kuwa wakati mwingine Waziri atafikiria kuwalipa wazee wa vijiji. Hata kama ni Kshs2,000 kwa mwezi, wazee hao watafurahia kazi yao. Uchumi wetu ukiendelea kuimarika, kwa sababu naamini Serikali hii itarudi tena, na tutapigania irudi tena, kwa sababu wale wengine wanaoyumbayumba hapa, ni watu waliokuwa katika ile Serikali nyingine. Wengine wanajifanya eti wataleta elimu ya bure na wao walikuwa Mawaziri wa elimu. Nakumbuka kuwa waalimu walikuwa wakigoma wakitaka mshahara wa mwezi uliopita, hata si nyongeza. Lakini, leo wanalipwa na kuongezewa! Hiyo ni hatua moja Serikali hii imepiga na ndio sababu naiunga mkono. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunasema ni lazima sote tuwajibike. Nimewasikia wengine wakilalamika kwa sababu tunakaa bila kazi ofisini. Kwa nini Ndile awe Waziri Msaidizi na kazi yake ni kukaa ofisini kusoma magazeti? Tunataka tugawanye kazi! Tunataka tupate habari ili tujue ni kitu gani kinaendelea katika Wizara lakini si kuitwa hapa kuja kujibu Maswali. Hili ndilo jambo linalotufanya kusema hatuna kazi. Hiyo ni kuharibu pesa za umma. Ikiwa ni mimi niko katika Wizara ya Utalii na Wanyama Pori, nataka kujua ni wapi watu wamewauwa na ndovu kwa siku na ikiwa hawakuuwa watu, wameingia shamba la nani. Ninataka kupata ripoti hiyo ili niweze kujua. Lakini kama sijui halafu niambiwe nijibu Swali--- Nasema hivyo kwa sababu habari hizo zinatolewa kwa Waziri. Wakati mwingine siwezi kumlaumu kwa sababu labda ana kazi nyingi sana na mimi sina habari. Nasikia watu wakinipigia simu na kuniuliza kama nimesikia jambo fulani. Sitaki kusikia kitu fulani! Tunataka wale wanaohusika kwamba wajue hatupendezwi na jambo hili kwa sababu tunataka kufanya kazi. Jambo lingine muhimu sana katika Wizara ya Utalii na Wanyama Pori, nadhani katika Serikali hii tuna mchango mkubwa kama Wizara na imefaulu sana. Lakini inaweza kufaulu zaidi tukifanya bidii. Inafaa tupige hatua! Ile hatua tutapiga si rahisi; ni lazima tuangalie wenzetu wamefanya nini. Juzi nilikuwa Mauritius na walisema kuwa kwao wamewakaribisha watalii. Ikiwa una pesa zako na unasikia kule kuna baridi nyingi na umezeeka, ukienda kule kwao, watakupatia hata shamba bure. Wanawakaribisha watu kutoka sehemu mbalimbali kwenda kuishi kwao. Hivyo ndivyo wamesema kule kwao. Wamesema pia si lazima mtalii akae katika hoteli kubwa. Wamewaambia watu wajenge nyumba za wageni. Ikiwa ni mzungu ambaye amekwenda kule na kutaka kukaa mashambani, anaruhusiwa. Kwa kufanya hivyo, wamepata pesa nyingi. Lakini ukirudi Kenya, utakuta mtu akisema: \"Hapa Bonde la Ufa ni kwetu, sisi ni Wamaasai! Nyinyi mlale kama bahasha\" Imekusaidia na nini kama ni kwenu? Ni nchi kubwa na haisaidii kwa chochote! Wanapigana kwa sababu ya ukabila. Nawauliza Wakenya swali moja. Mwanamke akienda kufanya kazi katika mashamba ya majani huko Kericho na kwa bahati mbaya apate mimba huko na afukuzwe mwezi huo, atarudi na mimba hiyo Ukambani na azae. Je, atakuwa amezaa Mkamba ama Mkericho? Ni nani atajua mama yake alimtoa wapi? Sisi wote ni Wakenya na ukabila ni lazima uishe. Kwa hayo machache, ijapokuwa ningependa kuongezewa muda zaidi, naomba kuiunga June 20, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1959 mkono Hoja hii."
}