HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 217636,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/217636/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Shakombo",
"speaker_title": "The Minister of State for National Heritage",
"speaker": {
"id": 244,
"legal_name": "Rashid Suleiman Shakombo",
"slug": "rashid-shakombo"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi pia nasimama hapa kuunga mkono Bajeti ya mwaka huu unaoanza Julai tarehe moja. Naunga mkono Bajeti hii kwa sababu ya mambo kadhaa. Kwanza, naangalia upande wa elimu. Elimu ilikuwa ni tatizo kubwa kwa watu wengi wa Kenya kwa sababu ya hali yao ya umaskini. Lakini, kwa imani ya Serikali hii inayoongozwa na Rais Kibaki, Waziri wetu wa Fedha ametilia maanani sana elimu. Mwaka unaokuja, ametenga zaidi ya Kshs100 bilioni kuhudumia mambo ya shule za msingi na za upili. Pia, nikiwa bado juu ya elimu, nataka kuongezea kwamba sisi Wapwani, kwa zaidi ya miaka 40 tangu Kenya ilipopata Uhuru, tumekuwa tukiomba chuo kikuu. Tumelia sana mpaka mwaka huu, ndio tumepata. Hatukupata chuo kimoja bali tumepata viwili. Hata Vice-Chancellor wa Chuo cha Taita ameshaandikwa kazi jana. Tunatarijia yule wa kule Kilifi pia ataandikwa kazi. Kwa hivyo sisi, kwa niaba ya watu wa Pwani, tunasema asante sana kwa Serikali hii kwa kuangalia mambo ya elimu upande wa kwetu. Jambo lingine ambalo ningependa kutaja linahusu wazee waliostaafu. Kwa mara ya kwanza, wazee hao wamesaidika kwa kusahemewa kutolipa kodi juu ya pesa kidogo wanazozipata. Najua wazee wengine hivi sasa ambao hawapati hata shillingi moja kwa sababu walisahau kujaza zile fomu. Walifikiria wako na pesa nyingi zaidi lakini hata zile kidogo wanazozipata, zinachukuliwa na watu wa Income Tax. Hali ya wazee hao ni mbaya sana. Nataka kuchuka nafasi hii kuuliza Waziri wa Fedha awaongezee pesa kidogo mwaka ujao. Kila ghali. Kuwaondolea kodi peke yake haitoshi. Tungeomba waongozewe hata ikiwa ni asilimia 20, 30 au 40 ya mshahara wanaopata sasa, maanake wazee hao si wengi. Wale wachache walioko yafaa waongezewe kwa sababu hao ndio walishikilia punde tu tulipopata Uhuru. Tusidharau juhudi zao zilizotufikisha hapa tulipo na tukawa tunaendelea na nchi nzuri. Jambo la tatu ambalo limenifanya pia nizidi kuunga mkono Bajeti hii ni ile hali ya kuwaangalia maskwota. Mkoa wa Pwani kwa jumla una maskwota wengi kuliko pahali pengine popote. Huko kwingine ni kidogo tu. Ni wale ambao wanalima msituni. Lakini sisi, katika ile miji tunayoishi, wengi wa watu wetu wanalazimika kulipa kodi za nyumba zile ndogo wanamoishi. Asipolipa kodi hiyo, nyumba hizo zinauzwa. Mzee huyo wakati ule alipokuwa kazini, angeweza kujenga nyumba nzuri. Na kwa vile amestaafu na ni mzee skwota, kile kidogo alichonacho kikiuzwa huwa ni hasara na mateso makubwa. Kwa hivyo, nasema asante sana kwa hii Bajeti ya kuongeza Kshs1.3 bilioni kuwapa maskwota makao. Kitu ambacho kinasikitisha ni kwamba, katika pesa zilizotengwa kuwapatia makao maskwota mwaka jana, hata shillingi moja haikutumiwa huko Pwana. Pesa zote zilitumiwa kununua mashamba upcountry . Safari hii, tunauliza Waziri anayehusika asifanye makosa hayo; Kshs1.3 billioni tena zimalizikie huko huko ilhali sisi tunaendelea kungoja. Unajua tukingojangoja, tutapata mwana sio wetu. Pesa hizo zigawiwe kila mkoa, haswa kule kwenye maskwota wengi. Vile vile, ningependa kupongeza Bajeti hii kwa sababu ya vile pesa nyingi zimetengewa barabara zetu. Barabara pia zimeangaliwa na zimepewa kiwango cha juu. Tulikuwa na shida kubwa sana ya barabara kutoka Likoni Ferry hadi katika mpaka wa Tanzania. Mpaka sasa, kandarasi zimetolewa na kazi ya kukarabati barabara hiyo imeanza. Itatuunganisa na nchi jirani ya Tanzania. Lakini kuna sehemu ndogo ambayo tunaita \"no man's land\". Hiyo sehemu haina lami ukifika Lunga Lunga. Ni muhimu sehemu hiyo iangaliwe pia. Jambo lingine ambalo limenifanya niunge mkono kabisa Bajeti hii ni kule kuanzishwa kwa Women Enterprise Development Fund. Akina mama walikuwa wakitatizika sana. Tunaambiwa pesa za CDF tunazopewa tusizitumie kwa vikundi vya akina mama. Tunaambiwa tuzitumie kwa miradi ya community au society . Lakini, community ni nani? Mimi nafikiria community inaanza na mimi, mke wangu na watoto, ndugu zangu, majirani, halafu Kenya nzima. Kwa hivyo, tukianza kubagua eti kikundi hiki hakistahili siyo vizuri. Sasa, akina mama wataunga mkono vilivyo 1960 PARLIAMENTARY DEBATES June 20, 2007 mapendekezo yaliofanywa na Wizara ya Fedha. Juu ya elimu vile vile, Serikali imesema itawaajiri walimu 11,000. Hii ni kwa sababu sasa tuna elimu ya bure na tumejenga shule nyingi. Shule hizo zina ukosefu wa waalimu. Kwa hivyo, tukiwaajiri walimu 11,000 na wagawanywe katika Kenya nzima kisawa, tutaongeza thamani ya elimu ya bure ambayo Serikali yetu imepeana. Jambo la saba ni usambazaji wa nguvu za umeme. Baadhi yetu tumekota sehemu za miji. Lakini kuna sehemu zingine ambazo, hata kama zinaitwa miji, ziko mashambani kuliko hata sehemu nyingi za mashambani. Katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni, kuna sehemu nyingine tunayoita Mwanagala. Ukifika huko, hutakubali iko Mombasa. Lakini, ramani inaonyesha iko katika Wilaya ya Mombasa. Tulikiwa na shida kwa sababu manispaa zetu hazina fedha za kueneza nguvu za umeme. Hatukujua tufanye nini. Lakini Wizara ya Kawi imetuhurumia. Naweza kusema kwa furaha kwamba sehemu zote za sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni zina nguvu za umeme. Tuna pesa za kutosha na kila mtu anajua kweli kuna Serikali ya vitendo kuliko maneno. Bw. Naibu Spika wa Muda, la mwisho kukicha, gharama ya maisha inazidi kuwakwetu sisi kama wakulima ambao wanafanya ukulima ndogo ndogo kwa sababu sisi ni vyongozi na kila mara tunasikia vilio kutoka sehemu mbali mbali, huwa tunauliza Serikali yetu kwa sababu tunataka kila mmoja afurahie haya matunda na uzuri wa hii Serikali ya Bw. Kibaki. Basi wale ambao wamenyimwa pesa kwa siku nyingi ama wana madeni yao ambayo wanangoja kutoka kwa Serikali, wapewe. Nasema hivyo kwa furaha kwa sababu Waziri wa Fedha aliona ni jambo nzuri wakulima wetu wa pareto walipwe hizo pesa. Jambo hilo lishachukuliwa, na wakulima hao watapata malipo yao na hiyo ni shukrani. Ni matumaini yangu kwamba wale wote ambao hawaoni uzuri huu wamuone kwa vitendo vyake. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}