HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 217912,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/217912/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami nichangie Hoja hii kuhusu Bajeti. Ningependa kufungua kwa kusema kwamba Bajeti hii ni muhimu sana kwa sababu ndiyo Bajeti inayofunga kipindi cha utawala wa NARC. Inadhihirisha mambo ambayo Serikali iko tayari kufanya na yale mambo ambayo haiko tayari kufanya. Bw. Naibu Spika, kuna jambo moja ambalo lilininitia wasiwasi na likanifanya nione uchungu. Kama mmoja wa wale walioteswa wakati wa utawala wa Serikali ya KANU, nilidhani na kuomba kwamba Serikali hii ingeiwezesha nchi hii kuwa na Tume ya Kweli, Haki na Maridhiano ili tuweze kusameheana; wale tulioteswa na wale waliotutesa. Kama tungelifanya hivyo, June 19, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1883 tungeiletea nchi hii amani ambayo yaonekana itakuwa ngumu kupata na tutaendelea kuchukiana, kudharauliana. Sijui ni kwa nini Serikali haikuruhusu tuwe na Tume ya Uhuru, Haki na Maridhiano. Pili, ningependa kusema kwamba kulingana na yote tuliyosomewa na Mhe. Kimunya, ni wazi ya kwamba vita dhidi ya ufisadi vimedorora na sioni kama vitaendelea. Nimesema hivyo kwa sababu huwezi kupigana na ufisadi kama huna ujasiri wa kuwashika wafisadi na kuwafunga. Sikusikia juu ya juhudi za kuwashika wafisadi na kuwaweka ndani. Tulichosikia ni mambo ya kuunda taasisi na sheria za kuzuia ufisadi. Namna pekee ya kukomesha ufisadi ni kushika wafisadi, kuwafanyia kesi na kuwafunga. Bw. Naibu Spika, mtu wa pekee ambaye amewahi kufungwa jela kwa sababu ya ufisadi; mtu mkubwa katika nchi hii sasa inabaki ni yule mama, Dr. Gachara. Wengine wote wameponyoka, na hawa ndio sasa wanatafuta uongozi wa nchi hii. Naomba kusema ya kwamba, tukishindwa kupigana na ufisadi, tusijidai kwamba tutaweza kupigana na umaskini katika nchi hii, kwa sababu, kitu kinachokuza umaskini kwa namna kubwa sana ni kitu kinachoitwa ufisadi. Bw. Naibu Spika, kitu kingineAmbacho nataka sema na kilichonisikitisha ni kwamba, tunataka kuuza makampuni ya umma ili tuweze kupata pesa kiasi Kshs36 bilioni. Nataka kusema ya kwamba, kiitikadi, mimi sikubaliani na falsafa ya kwamba, ni lazima makampuni yapewe watu binafsi ndio yaweze kustawi. Naamini kwamba hata makampuni ya Kiserikali na umma yanaweza kusimamiwa kwa namna isiyo na ufisadi na yakastawi. Hili wazo la kusema kuwa ni lazima makampuni ya umma yote yapewe watu binafsi ni juhudi na njama ya kuhakikisha kwamba utajiri wa nchi unapewa watu wachache. Sikubaliani na jambo hili. Kama tunapigana na ufisadi, sio lazima tuwauzie watu binafsi makampuni yetu yote. Haya ni makampuni yaliyojengwa na juhudi na jasho ya walio wengi. Kwa hivyo, kurudi kuwapatia watu wachache makampuni hayo ni kuwakosea walio wengi. Bw. Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningetaka kugusia ni kuhusu Ruwaza ya 2030, yaani \"Vision 2030\" . Tumeambiwa kuwa hii ndio itakayotufikisha huko Canaan. Maoni yangu ni kwamba hii \"Vision 2030 \" haiwezi kutupeleka kokote. Ninasema hivyo kwa sababu tumeandikiwa hii \"Vision 2030\" na wageni. Watu ambao hawawezi kujiandikia ndoto yao; hawawezi kujichorea ruwaza hawajui--- Lazima wawaite wageni wawaonyeshe njia ya kufika kule watakapokwenda, watu aina hio hawawezi kupata maendeleo. Wengi watabisha, lakini naona hakuna wanaobisha, kwa sababu wanajua kwamba hii ruwaza tuliandikiwa na wageni; kampuni inayoitwa Mackenzie & Company. Nashindwa, kwani sisi hatuna wataalam ambao wanaweza kuandika ruwaza yetu, mpaka tumeenda Afrika Kusini. Tunakwenda kwa makampuni ya Waingereza kuwaambia watutilie mwanamke mimba ndio tuweze kupata mtoto. Sisi tumekuwa tasa! Ukipata bibi ushindwe kuzaa naye na umpatie bwana mwingine akutilie huyo bibi mimba, ujuwe kwamba mtoto atakayepatikana pale sio mtoto wako. Sisi tunaonyesha kwamba hatujiamini hata kidogo. Eti ni lazima tuende kwa wazungu. Kitu kibaya zaidi ni kwamba wazungu hawa wanawachukua watu wetu, wanawapa kazi ya kuandika haya, lakini moyo unakuwa ni ule wao. Ni kama tumesahau ya kwamba vita kati ya nchi bado zinaendelea. Vita vya kiuchumi kati yetu na nchi za magharibi vipo na vitaendelea kuwepo. Hatuwezi kusema ya kwamba tunakwenda kwa wageni ndio watuonyeshe namna ya kushinda vita hivyo. Bw. Naibu Spika, \"Vision 2030\" ni usalata mtupu. Haifai kuandikiwa ruwaza hii na watu wa nje. Tuna akili na uzoefu wa kutosha, sisi ndio wenye taabu, sisi ndio tunatafuta uokovu, kwa nini turudi tena kwa mzungu? Kwa nini? Natumai kwamba Bw. Kenneth, kwa sababu yuko hapa, atatujibu swali hili. Kwa nini wakaenda kwa wazungu kuwauliza wawaandikie? Waliwalipa pesa ngapi ndio watuandikie ruwaza hii? Ningetaka kujua tulitumia pesa hizo kwa nini. Je, ni kwa sababu hatuna wasomi, wazalendo au fikra? Kwa nini tulifanya hivyo? Hayo ni maswali muhimu. 1884 PARLIAMENTARY DEBATES June 19, 2007 Bw. Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka kutaja ni kwamba, zile Kshs1 bilioni ambazo zilitengwa kwa minajili ya kuwatafutia mashamba wale wasio na mashamba, hazitoshi. Tuna mamilioni ya maskwota ambao hawawezi kutafutiwa mashamba na makao na Kshs1 bilioni. Pesa hizi hazitoshi. Mashamba yamejaa hapa. Tunamwona Bw. Delamere ambaye ana mashamba kutoka Naivasha hadi Nakuru. Kule Laikipia, Wamaasai wanakosa pahali pa kulisha mifugo wao kwa sababu wazungu wamekalia malaki na malaki ya mashamba yetu. Aidha tuna haja ya kuendeleza nchi hii au hatuna. Lakini hatuwezi kundeleza nchi hii kama watu wachache wataendelea kumiliki malaki ya mashamba na mamilioni ya watu wetu wanabaki maskwota. Hawana pahali pa kuishi na hata pahali pa kuzikwa au kulima mboga. Hii Kshs1 bilioni haitoshi chochote; ni tone katika bahari. Bw. Naibu Spika, natumai kwamba Bw. Kimunya hajasahau kwamba kuna watu waliofukuzwa kutoka kwa mashamba yao, ambayo waliahidiwa na Serikali hii kwamba watatafutiwa ardhi ingine na mpaka sasa tunaendelea kumaliza kipindi hiki na watu hawa hawajapatiwa chochote. Bajeti hii, kama ilivyosemekana, ni Bajeti ya kutafuta kura, basi ni lazima Serikali ijue kwamba hata wale waliofukuzwa kutoka kwa mashamba yao wana kura. Serikali hii haitapewa kura tu kwa kuahidi kwamba wako na Kshs1 bilioni, ambazo hatujui zitatumiwa kwa namna gani. Nakubaliana na profesa mmoja ambaye nilimsikia akiongea hivi majuzi, akisema kwamba, kama hatuna mabadiliko ya namna ya mfumo wa kumiliki ardhi, hakuna wakati tutafikia maendeleo yaliyofikiwa na nchi kama Malaysia, Singapore na nchi zingine. Ninakubaliana na wazo hilo kwa sababu kuna watu wanapenda sana kuhepa swala la umiliki wa ardhi kwa sababu wao ni mojawapo wa wanyakuzi wa mashamba haya na wanataka tuamini kwamba nchi inaweza kuendelea wakati mashamba yanamilikiwa na wachache. Hilo halitawezekana daima, na hatusemi kwamba lazima kila mtu apate shamba ili nchi iendelee, lakini kabla ya sisi kujaribu kuaminisha watu ya kwamba wategemee viwanda ndio waweze kuishi, kwanza, ni lazima mashamba tuliyo nayo na hayafanyiwi kazi yapewe wale hawana mashamba. Bw. Naibu Spika, tena kuna miji ya mabanda; Kibera, Mathare, Korogocho na miji mingine. Unastahili kwenda Mathare na Kibera ndio uone umaskini uliokithiri pale. Ni umaskini mbaya kuliko umaskini ulio jehanamu. Na hakuna pesa zozote ambazo tumetenga za kupigana na umaskini ulioko kule. Unashindwa, Serikali--- Namuomba Bw. Kimunya asafiri au afanye matembezi huko Kibera ili aone ule umaskini aliousahau. Aende Mathare, Korogocho na kwingineko. Labda mwaka ujao, kama atakuwa na bahati ya kurudi Bunge, hatasahau miji hii. Lakini naona kana kwamba hatarudi Bunge. Akirudi, itakuwa ni bahati. Kwa haya machache, naomba kuunga mkono."
}