GET /api/v0.1/hansard/entries/218259/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 218259,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/218259/?format=api",
    "text_counter": 191,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu Hoja hii. Ninaomba kufanya hivyo kwanza kwa kumpongeza Mbunge kwa kuleta Hoja hii Bungeni, ambayo inaomba ruhusa ya kutayarisha Mswada wa sheria juu ya habari na mawasiliano. Bw. Naibu Spika wa Muda, pamoja na kumpongeza Mbunge, ningetaka kumtahadharisha kwamba ni kama juhudi zake kidogo zimechelewa kwa sababu hata yeye ana habari kwamba tayari Wizara imetayarisha Mswada wa sheria juu ya habari na mawasiliano, Mswada ambao tutauwasilisha Bungeni leo alasiri au kesho alasiri. Kwa hivyo, sidhani tungekuwa na sababu yoyote ya kuchukuwa msimamo kinyume na matakwa ya Hoja hii. Tunaiunga mkono, lakini tutasaidia kufanya lile ambalo Hoja inaomba. Nina hakika kwamba Mbunge atashukuru kuona kwamba tumechukuwa mzigo aliokuwa tayari kuubeba kwa niaba yake na nchi nzima. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni wazi kwamba teknolojia, habari na mawasiliano ndizo zimekuwa kiini cha maendeleo yote ya nchi yetu, na maendeleo yote ya dunia. Kesho itakuwa siku ya kusomewa Bajeti, na maombi yangu ni kwamba Bajeti hiyo ya kesho itaipatia Wizara ya Habari na Mawasiliano kiasi cha pesa tutakazokuwa tumeomba, kwa sababu hii ndio Wizara ambayo inategemewa na nchi nzima kwa maendeleo."
}