HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 218261,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/218261/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Ni kweli, Bw. Naibu Spika wa Muda. Labda, ninaishangilia Bajeti, lakini nachukua tahadhari yako. Hata hivyo, ningependa kusema kwamba Wizara hii hapo nyuma, haikudhaminiwa ya kutosha. Kusema kweli, ilikuwa imeorodheshwa kama ya pili kutoka mwisho. Lakini sasa naiona kama Wizara ambayo itakuwa ya kwanza miongoni mwa Wizara zote tulizo nazo nchini. Bw. Naibu Spika wa Muda, nilimsikia mhe. Ochilo-Ayacko akisema ya kwamba ni muhimu kwa Wizara ya Habari na Mawasiliano iunde hazina ambayo itagharamia usambazaji wa tekinolojia katika maeneo yote ya nchi. Mswada ambao umetayarishwa na Wizara unashughulikia jambo hilo kikamilifu. Kuna hazina ambayo itagharamia usambazaji wa tekinolojia katika maeneo yote ya nchi. Ni matarajio ya Mswada huu kwamba pesa zilizotengwa katika hazina hii zitatumiwa na Serikali kuhakikisha ya kwamba kila eneo la uakilishi Bungeni litakuwa na kijiji cha tekinolojia ya kitalakimu ambacho kwa lugha ya Kiingereza kinaitwa digital village. Natumai ya kwamba hili ni jambo ambalo litasaidia sana kuwepo kwa tekinolojia katika kila eneo. June 13, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1767 Mbali na hivyo vijiji, kutakuwepo na vijiji vingine pia vya tekinolojia kwa sababu ni imani ya Serikali ya kwamba bila tekinojia hii na ujuzi wake kusambazwa, Wakenya haiweza kuwa washiriki katika maendeleo ya kisasa. Bw. Naibu Spika wa Muda, labda mheshimiwa Mbunge aliyeleta Hoja hii ameona mitaro ambayo imechimbwa kutoka Mombasa hadi Kisumu. Mitaro hiyo itakwenda hadi kwenye mpaka wetu na nchi ya Sudan. Lengo la uchimbaji huu ni kusambaza nyaya za optic. Sijui neno \" optic\" linajulikanaaje kwa lugha ya Kiswahili. Lakini la muhimu ni kwamba waheshimiwa Wabunge wanaelewa kile ninachoongea juu yake. Baada ya kusambazia nchi nzima nyaya za optic, patakuwa na uwezekano mkubwa wa tekinolojia kila pahali nchini. Pamoja na nyaya hizo za optic, pia ni wazi ya kwamba simu za mkono zimefika katika pembe nyingi nchini. Hiyo ni sehemu mojawapo ya tekinolojia ya habari na mawasiliano. Bw. Naibu Spika wa Muda, Serikali inaelewa vizuri ya kwamba bila tekinolojia ya mawasiliano na habari, Kenya itabaki nyuma kimaendeleo kama vile Bara la Afrika lilivyobaki nyuma likilinganishwa na bara zingine. Maendeleo duniani yameorodheshwa katika enzi nne. Kuna enzi ya kwanza ambayo ilikuwa ni enzi ya mapinduzi ya kimawazo, yaani renaisance. Baada ya hiyo, dunia iliingia katika enzi ya nguvu za bunduki, baada ya Marcopolo kutembelea Uchina na kupata gun powder na kurudi nayo Uropa. Wazungu walitumia nguvu za poda hiyo kutengenezea bunduki na wakatumia bunduki hizo kuenda katika pembe nyingi duniani na kunyaka mali ambayo waliitumia kuongezea maendeleo yao. Baada ya nguvu za bunduki, dunia iliingia katika enzi ya mtambo wa kutumia nguvu za mvuke. Wazungu walitumia mtambo huu kuunda meli ambazo ziliwasaidia kuzunguka dunia zikiteka koloni na malighafi ambayo yalipopelekwa kwao yalitumika kuundia viwanda na kutawalia dunia. Sasa, dunia imeingia katika enzi ya nne ya maendeleo ambayo ni enzi ya tekinolojia ya habari na mawasiliano. Huu ndio msingi wa kile kinachoitwa utandawazi. Katika enzi hii ya utandawazi, ni wazi ya kwamba hatuwezi kushiriki katika biashara ya kimataifa kama hatuna ujuzi wa tekinolojia ya habari na mawasiliano. Tekinolojia hii ni muhimu kama vile hewa. Hivi karibuni, bila tekinolojia, hutaweza kuenda popote. Utakuwa umo katika enzi ya nyuma ambayo imepitwa na wakati. Hutaweza hata kujilinda kutokana na dunia ikiamua kukushambulia. Mhe. Weya ameongea kuhusu umuhimu wa kutoa leseni ya kufanya biashara inayohusu tekinolojia ya habari na mawasiliano, bila ya kufanyiwa ubaguzi wowote wa kisiasa. Ningependa kumhakikishia ya kwamba leseni zinatolewa kwa msingi wa usawa na uwezo wa wanaoomba leseni ili kufanya kazi hii. Sidhani ya kwamba mhe. Weya ana ushahidi ya kwamba kumekuweko na ubaguzi wa aina hiyo. Kama umekuwepo, nadhani utashughulikiwa vilivyo. La muhimu ni kwamba muongozo wa Serikali hautambui ubaguzi huo na utataka kuhakikisha ya kwamba watakaopewa leseni ni wale wote ambao wanauwezo wa kifedha wa kuweza kufanya biashara hii. Hii ni kwa sababu biashara haijui siasa. Yeyote ambaye anaweza kuiletea nchi hii maendeleo atakuwa mzalendo halisi. Kwa hivyo, ni lazima apewe kila aina ya msaada ili kumuwezesha kufanya kazi yake. Mhe. Weya pia aliongea juu ya ukiritiba wa biashara wa vyombo vya habari. Alitoa hofu ya kwamba kukiwa na wachache ambao wataruhusiwa kumiliki vyombo vya habari tofauti, watu hao watakuwa na nguvu zaidi za kisiasa. Huo ni ukweli mtupu, lakini ningependa kumuambia ya kwamba kuna sheria ambayo inashughulikia swala la ukiritiba au monopoly . Ikiwa sheria hiyo haifanyi kazi kikamilifu kwa maoni yake, anaweza kuleta mapendekezo ya kurekebisha Mswada huu tutakapoingia katika Kamati ya Bunge Nzima. Nadhani marekebisho yake yanaweza yakawekwa kwenye Mswada wenyewe ili sheria ya habari na mawasiliano iweze kushughulikia vilivyo swala hilo la ukiritiba. Bw. Naibu Spika wa Muda, mhe. Weya aliongea pia kuhusu hofu au haja ya kushughulikia tatizo la usambazaji au ukosefu wa maadili miongoni mwa vyombo vya habari, hasa katika kuwaonyesha watu wetu filamu za ngono katika saa ambazo hata watoto wetu hawajalala. Hili ni 1768 PARLIAMENTARY DEBATES June 13, 2007 swala nyeti kwa sababu lishatolewa uamuzi na mahakama wakati gazeti moja liliishitaki Serikali ili kupata maelekezo kuhusu filamu gani zinaweza kuonyeshwa kwa wakati gani. Lakini hofu ya mhe. Weya inaeleweka. Ni hofu ambayo ina umuhimu mkubwa kwa sababu kwa kweli, si sawa kwa vyombo vyetu vya habari, hasa runinga zetu, kuonyesha filamu za ngono, kwa mfano, saa mbili za usiku, wakati bado tuko mezani na watoto wetu. Hata unashindwa kutazama filamu ya aina hiyo. Sijui kama jamii nyingine hufanya ngono masaa hayo. Lakini kiafrika nadhani ngono huja baada ya watu kula, kusikiliza habari na kulala. Isitoshe, mimi hata sijaelewa ni kwa nini mtu atazame filamu ya ngono ili aweze kufanya kazi hiyo. Mambo haya yanaweza kufanyika bila kutazama filamu hizi. Sioni umuhimu wa wazo hilo. Kuna nyimbo nyingine ambazo zinajulikana kwa jina maarufu la \"rap.\" Nyimbo hizi zimejaa ushawishi wa kingono. Ukiangalia runinga zetu saa kumi jioni utakuta nyimbo hizo zinaonyeshwa. Ajabu ni kwamba hakuna mtu ambaye haelewi lugha za nyimbo hizo. Ni lugha ya kutatanisha kwa sababu ni mapema sana. Saa kumi jioni watoto huwa bado wako shuleni na wengine huwa nyumbani wakitazama namna zinavyochezwa. Ni vibaya sana kuona nyimbo hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna video za ngono ambazo hutengenezewa hapa nchini. Ni kweli kuna studio za kutengenezea video. Baadaye video huuzwa katika nchi za nje kama bidhaa za kutoka nchini mwetu. Ni video mbaya. Zinatuharibia jina na maadili yetu kimataifa. Ninaamini ya kwamba ulevi wa kiponographia umekuwa mbaya hata kuliko ulevi wa mihadarati. Ukikutana na mlevi wa kiponographia, hasa ukiwa wewe ni mama, ni afadhali ukimbilie usalama wako kwa sababu panakuwa na hatari kubwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna waheshimiwa Wabunge ambao walizungumza juu ya uhusiano kati ya teknolojia ya habari na mawasiliano na swala la usalama. Huu ni uhusiano halali kabisa kwa sababu vita vya kisasa havitegemei sana uwezo wa bunduki. Vinategemea umilikiaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Hata vitu vingi ambavyo vinahusu vita vya kisasa, karibu vyote vinategemea teknolojia hii ya habari. Si ajabu ya kwamba mtambo wa internet uligunduliwa na jeshi la Marekani. Kwa hivyo, watu wasidhani ya kwamba wanaweza kuutumia mtambo huu wafikirie wamekuwa na ujuzi sana. Ukweli ni kwamba ni lazima tujue zaidi ya kutumia komputa kwa sababu dakika ya mwisho yule ambaye anamiliki teknolojia hiyo ndiye mwenye nguvu zote. Hii ni kwa sababu mtu akitaka kukufungia internet hiyo atakufungia. Wale ambao wataweza kujihami katika teknolojia hii ni wale ambao wataweza kutumia komputa na kujua inavyofanya kazi, ilivyoundwa na ufundi wake. Kuna watu wana ujuzi wa kuweza kuitumia bila ya kutegemea wengine. Kwa sasa, bado tuko mbali sana. Tunaweza hata tukasema sisi ni kama shule ya chekechea tukilinganishwa na wengine kwa sababu wao wamefika chuo kikuu kiteknolojia. Tuna safari ndefu sana ya kusafiri ili tuweze kufikia ndugu zetu kiteknolojia. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna maswala mengine ambayo yamegusiwa na waheshimiwa Wabunge. La muhimu hapa ni kusema ya kwamba tutauleta Mswada leo au kesho alasiri kama nilivyosema hapo awali. Mswada huu utazambaziwa waheshimiwa Wabunge wote ili wapate nafasi ya kuusoma. Iwapo wataona haja ya kuufanyia marekebisho, basi watapendekeza kabla ya sisi kuujadili katika Kamati ya Bunge Nzima. Mapendekezo yao yatajadiliwa na Kamati hiyo ya Bunge Nzima. Hii itakuwa ni sheria mpya ya habari na mawasiliano. Ninachosema ni kwamba sisi hatuipingi Hoja hii. Ni furaha yetu ya kwamba tayari tuna Mswada huu ambayo unapendekezwa na Hoja hii. Tunaweza kusema ya kwamba sasa mpira wa Mswada huu umo upande wa Bunge hili. Ikiwa Bunge hili litapitisha Mswada huu, basi nchi hii itakuwa na sheria juu ya habari na mawasiliano. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo mengi au machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}