GET /api/v0.1/hansard/entries/218952/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 218952,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/218952/?format=api",
"text_counter": 262,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, swala la kuhesabu vyama si swala la Bunge hili mbali ni la Msajili wa Vyama. Juzi Bunge liliketi na kupitisha sheria kuhusu namna ya kuwachagua waakilishi wa Kenya katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashiriki. Ni matumaini yangu, kuambatana na sheria hiyo, ikiwa mhe. Bunge, alitaka kuikosoa, basi alikuwa na fursa na nafasi ya kutosha kuhakikisha vyama fulani na watu binafsi watapata fursa katika uwakilishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashiriki. Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge hili. Hatuwezi kuibatilisha sheria! Kenya imechelewesha shughuli za Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashiriki kwa sababu ya mvurtano wetu. Mvurugano wetu wa kisiasa usivuruge Jumuyia Afrika Mashariki. Maslahi yetu ya vyama yasivuruge Afrika Mashariki. Kwa mara ya kwanza, mengi ya majina haya yanawakilisha sehemu kubwa ya nchi ya Kenya. Wale ambao wasingekuwa na fursa ya kuwakilishwa katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia wamepata fursa leo. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa mfano, chama cha LDP kimewakilishwa na mhe. Mbunge mmoja. Kifungu cha 4 cha sheria hiyo, kinasema Katibu wa Bunge agawanye nafasi hizo kwa vyama vinavyowakilishwa hapa Bungeni. Je, chama cha LDP kitapata nafasi ngapi? Kwa hivyo, tusivuruge shughuli za Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hebu sheria hii ifanye kazi ili Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashiriki iweze kufanya kazi yake. Kwa hayo machache, ninaunga Hoja hii mkono."
}