GET /api/v0.1/hansard/entries/219006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 219006,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/219006/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kombe",
    "speaker_title": "The Member for Magarini",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": " Asante Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, kabla sijachangia kwa mjadala huu, ningetaka kurudisha shukrani zangu kwa watu wa Magarini kwa vile walivyokuwa imara na kuwathibitishia Wakenya kwamba mwaka wa 2002, walipiga ndipo kwa sababu palikuwa ndipo na wakarudia kupiga ndipo. Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, walithibitisha ya kwamba si watu wakuhaingishwa na fedha maana fedha nyingi zilimwagwa. Pia walithibitisha si watu wa kuhangaishwa na magari makubwa makubwa na mengi. Pia walithibitisha kwamba maji katika bahari ya Magarini ni maji yaliyo na kina kirefu ambacho hakiwezi kamwe - viumbe wa majini kama vile mamba na viboko - hawawezi kamwe kuvidhiti kina hicho ila papa peke yake. Vile vile, mashindano au hali ya demokrasia iliweza kudhihirika Magarini kwa vile vyama vingine vyote vilivyoweza kwenda kushiriki katika demokrasia."
}