GET /api/v0.1/hansard/entries/219014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 219014,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/219014/?format=api",
    "text_counter": 324,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kombe",
    "speaker_title": "The Member for Magarini",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Nilikuwa ninasema kuwa pia ninavipongeza vyama vilivyo kwenda kushiriki kwa sababu vilidhihirisha kwamba Kenya ina demokrasia licha ya kwamba tulikuwa marafiki, bali waliweza kusimamisha wagombea wao na pia wakaja wakashuhudia kushindwa kwao. Hilo lilikuwa ni jambo jema kwa demokrasia nchini Kenya! Pia vile vile, ningependa kuthibitisha kwamba miradi ambayo inaendelea na ambayo ingefikiriwa kuwa ni miradi ya kampeini, ni miradi ambayo tulijadiliana na Mhe. Rais, tarehe 4 Januari, 2007 na ilianza hata kabla ya uchaguzi kuharamishwa. Hivyo basi, Serikali ilikuwa inaendeleza miradi yake kwa wananchi wake na siyo kwa minajili ya uchaguzi wa Magarini. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kumalizia, pia miradi ya barabara ilianza hata kabla ya uchaguzi kuharamishwa. Kwa hivyo, haikuwa haki kwa wengine kusimama na kusema kwamba hali hiyo ilitumika kwa niaba ya uchaguzi wa Magarini."
}