GET /api/v0.1/hansard/entries/219026/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 219026,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/219026/?format=api",
"text_counter": 336,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Ndile",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Tourism and Wildlife",
"speaker": {
"id": 272,
"legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
"slug": "kalembe-ndile"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, ninasema kwamba hata kama sijaona jina la Mkamba hapa, naamini Kenya ni kubwa na tuko na makabila mengi sana. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaosema kwamba: \"Kinyozi hajinyoi.\" Yale matatizo ambayo tuko nayo hapa Bungeni, ambapo watu wanasema kwamba hawakuwekewa majina waliotarajia, ni wao walitaka kujinyoa kwa sababu tulianza na wao na wakadanganyana, wakasema kwamba huu ni mchezo wa mpira. Walifikira kwamba siasa ni mchezo wa mpira. Ningependa kusema kwamba hakuna jina la Mkamba katika orodha hii, kwa sababu mtu mmoja aliwadanganya Wakamba wetu na wakaenda upande ule. Wangekuwa upande huu, tungekuwa na jina moja la Mkamba katika orodha hii. Ningependa kusema kwamba, katika hili Bunge, nimegundua kwamba ukiona wengine wanaongea hapa, hawaongei wakimuogopa Mungu. Wengine wanataka marafiki wao au ndugu zao. Hao wanachezea akili ya Wakenya. Katika orodha hii hakuna jina la skwota ama mtu mlemavu. Hakuna mnenanaji yeyote ambaye amewatetea watu wa aina hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, hii shughuli ya kuvuruga vyama, wao ndio walioanza na sasa wako upande ule. Inafaa wakae kimya ili tumalize hii shughuli ya leo na tuanze shughuli nyingine. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}