GET /api/v0.1/hansard/entries/219361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 219361,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/219361/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Bw. Naibu wa Spika, ninamuomba Waziri wa Ardhi na Makao atoe taarifa na kueleza ni kwa nini wakazi wa Marereni na Kanagoni walioko katika maeneo ya chumvi wanahangaishwa musimu huu wa kilimo. Wakazi hao wametayarisha mashamba yao kwa kutumia matingatinga na kupanda mahindi, lakini, hivi majuzi, walivamiwa na askari, wakabebwa na kuwekwa korokoroni kinyume cha sheria. Ningependa Waziri pia aeleze kinaganaga jinsi mashamba hayo yalivyotolewa kwa wawekezaji wa kibinafsi, ikifahamika kwamba kuna watu ambao wameyaimarisha mashamba hayo ya kilimo kwa muda wa zaidi ya miaka 12. Kufikia sasa, zaidi ya miaka 30 imepita tangu wakati wakazi hao walipoyabuni na kuyahifadhi mashamba hayo. Ni jambo la kutatiza kwamba, mpaka sasa, watu wanahangaishwa ilhali Serikali ya Rais Kibaki imejitolea muhanga kuangamiza uskwota. Pia ningependa Waziri aeleze ana mipango gani kuhakikisha kwamba mashamba hayo, ambayo hayakuzi chumvi, yamerejeshewa wenyewe ili waweze kuendelea na shughuli zao bila ya kutatizwa na mtu yeyote. Bw. Naibu wa Spika, ningependa kumuomba Waziri achukue hatua ya dharura kulitatua jambo hilo, kwa sababu hali ya amani katika sehemu hiyo imo hatarini. Lolote laweza kutokea kuanzia sasa."
}