GET /api/v0.1/hansard/entries/219471/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 219471,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/219471/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Capt. Nakitare",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja hii ambayo inahusu maisha ya watu. Ripoti hii ambayo imeletwa Bungeni na kuungwa mkono na mhe. Syongo, ina maana sana. Mikutano mingi hufanyika kule Uingereza na nchi 1634 PARLIAMENTARY DEBATES May 24, 2007 zingine za Ulaya kuhusu watoto yatima walioko hapa nchini Kenya. Serikali inafaa kuzingatia maslahi ya watoto yatima. Maisha yaliokuweko kati ya mwaka wa 1980 na 1990 yalikuwa mazuri sana. Watu walikuwa na afya nzuri na pia adabu. Maafa yaliotokea kufuatia kuibuka kwa ugonjwa wa UKIMWI hushangaza watu ulimwenguni. Ugonjwa huu umewauwa watu wengi sana na kuwaacha watoto yatima. Inashagaza sana kwamba ukitembelea boma nyingi utawapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka 20 wakijitegemea wenyewe baada ya wazazi wao kufariki. Serikali inaweza kutenga kiasi fulani cha pesa ili kuangalia maslahi ya watoto yatima. Hata hivyo, watoto yatima sio wale watoto waliofiwa na wazazi wao tu, hata akina mama wajane wako katika hali ya uyatima, ihlali wao ndio wanajukumu la kuwatunza watoto wao. Siku hizi katika boma nyingi, utapata kwamba nyanya mkongwe ndiye kiongozi wa watoto karibu 12. Haya mambo ni ya kushangaza. Serikali hii inayoongozwa na Rais Kibaki imeleta maendeleo mengi nchini. Hata magereza yetu yamefanyiwa mabadiliko mengi. Kwa mfano, wafungwa wanaishi katika mazingira mazuri. Haya ni maongozi ambayo yanafaa kuangaziwa na kusifiwa. Serikali hii inafaa kupewa muda ili iweze kuendeleza mambo haya. Serikali haiwezi kumaliza mipango yake yote kwa mda mfupi, kwa sababu nchi haitakwisha kesho. Ni miaka zaidi ya kumi tangu siasa za vyama vingi zilianza. Watu waliuawa kwa sababu ya siasa na tamaa ya uongozi. Watoto wengi waliachwa mayatima kwa sababu ya ghasia hizo. Wazazi wao waliuawa kwa kukatwakatwa au kupigwa risasi. Wengi wao sasa wanakaa kando ya barabara wakiombaomba. Baada ya wazazi wao kuuawa wengi wao walikimbilia usalama mjini. Kwa kuwa hawana watu wa kuangalia maslahi yao huko mjini, waliitwa chokora, ilhali walikimbilia usalama na kutafuta usaidizi. Haya ni mambo ambayo yanataka kuangaziwa. Hoja hii inataja mambo muhimu. Inataja mikutano na mipango ambayo imefanywa nje ya nchi hii. Hata hivyo, hakuna kipengele kimoja katika Ripoti hii ambacho kinazungumza juu ya upangaji wa uzazi. Je, tutaendelea kuzaa kwa kiwango gani? Watu wengi wanaishia katika mazingira duni kutokana na kutopanga uzazi. Mfano mzuri ni wale watu wanaoishi kule Kibera na Mathare. Sehemu hizi hazina upangaji mzuri wa ujenzi wa nyumba. Watu wanaishi kama mifugo. Hiki ndicho chanzo cha usherati. Serikali imekuwa ikiwasaka wale ambao wanarandaranda mjini usiku, lakini huo sio usherati pekee. Kuna ule usherati unaotokana na ulevi. Juzi Serikali ilihalalisha unywaji wa busaa na chang'aa. Watu watakunywa chang'aa kwa wingi kwa sababu imehalalishwa. Lakini matokeo yake mwishowe yatakuwa nini? Utamkuta mzee mkongwe, kwa mfano akisema: \"Mimi sina chakula wala boma, lakini nikinywa vikombe viwili vya busaa hii, itakuwa blanketi yangu. Nikienda kulala sitahisi baridi wala njaa. Nitajua mambo ya kesho nikiamka.\" Ni lazima tuzingatie mambo ya upangaji wa uzazi. Ni lazima tupange uzazi kama vile inavyofanyika katika nchi zingine ambazo hualika nchi za Afrika mara kwa mara. Wewe una watoto 12 na huna mahali pa kujenga nyumba wala shamba. Labda ulienda mjini kutafuta kazi na ukastaafu kule. Hata nauli ya kurudi nyumbani imekushinda kupata na uko kule na watoto chungu nzima. Watoto wanapokosa mahitaji, tamaa inawafanya kuingia kwa usherati na kuambukizwa na ukimwi. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine katika nchi yetu ya Afrika - nimetaja miaka ya 1970 hadi 1990 - ni jambo ambalo limesambaza UKIMWI ni mambo ya vita. Wanajeshi walipokuwa wakipindua serikali kama ya Uganda, waliwaasi na kufanya chochote walichotaka. Walizaa watoto na mshangao wa sasa ni Zaire. Ukienda DRC Congo utapata watoto kabila nyingi na wa rangi tofauti ambao hakuna mtu anawaangazia. Mtoto wa miaka 12 amezaa. Ni nani alimpatia mimba isipokuwa ni mtu aliyekomaa? Ule uume wake ulimfanya yule mtoto wa miaka 12 azae. Yeye akizaa, yule jamaa anapata aibu na anaona haya ya kusema kuwa yule ni mkewe. Amempa kisonono na mtoto haendi hospitalini, kwa hivyo hapati matibabu. Tayari UKIMWI May 24, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1635 umempata yule mtoto na anazaa mtoto ambaye ana UKIMWI tayari. Kwa nini tusiwe na mwongozo katika Kenya? Nchi yetu haipanuki! Mashamba hayapanuki! Hata sasa Kenya imeshindwa na namna ya kuangazia mambo ya watu wasio na mashamba. Inabidi sasa Kenya itafute njia yoyote ya kuijenga kwenda juu badala ya kwenda kwa upana kwa sababu hakuna nafasi ya kupanua. Ukiangalia hii njia ya Nakuru, utashangaa. Ni kama biashara na ni aibu! Kwanzia Jumatano hadi Ijumaa, Nairobi, jeneza ziko kwa matatu na magari ya kubeba maiti zikielekea Magharibi mwa Kenya. Hiyo sehemu ikijaa makaburi, watalima, watalala na kujenga wapi? Ni lazima Serikali iweke mguu wake chini dhidi ya mambo haya. Ni lazima tuwe na upangaji wa uzazi. Sheria itungwe hapa ya kuwalazimisha watu kuwacha kuoa wake wengi na kuzaana kwa wingi. Inatakikana mtu awe na watoto watano ambao anaweza kulea. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo la pili ni kwamba ni mshangao kwa sababu mtu akiwa amestaafu na yule mtoto wa kitinda mimba ana miezi sita, akianza kusoma, babake atakuwa wapi? Kwa hivyo, hakuna mpango wowote tunaoweza kusema ya kwamba tunaangazia haya mambo. Ndio sababu hii Hoja ya Wabunge waliokwenda kwa huo mkutano, walienda kutafuta mambo na kuonyeshwa vile nchi zingine zilivyo. Kwa nini sisi tusiige nchi kama Uchina? Ukizaa zaidi ya watoto wawili, Serikali inakuhukumu. Itakupatia ulinzi wa mtoto wa kwanza na wa pili itakuwa ni gharama yako. Ukitaka kazi nzuri, inafaa uwe umezaa mtoto mmoja na unapewa huduma nzuri na Serikali. Kwa nini sisi tusifanye hivyo? Tusiwe tunawalazimisha ama kuwaacha watu wetu kuzaana wanavyopenda. Mkijaza Kenya mtakaa wapi? Mtakaa wapi watu wa Kenya, nawauliza? Ni lazima kuwe na kiwango! Hata matibabu ambayo mnalilia mkisema mnataka matibabu ya HIV/AIDS--- Lakini kuzuia ni bora kuliko kutibu. Mwingereza anasema: \" Prevention is better thancure !\" Ni kweli na ni lazima tuanzie kwa nyumba. Hakuna sehemu hata moja nimeona kwa hii Hoja inayosema kuwa ni lazima tuwe na mwongozo katika uzazi wa kinyumba. Tena inatakikana tuwe na kipengele ambapo wale watu ambao wamezeeka, wanaoitwa \" senior citizens \", pia wawe wanaangaliwa. Hii ni kwa sababu yule mtu alihudumia Kenya, akastaafu, akaenda nyumbani, hana mapato mengine na ni yeye alijenga Kenya. Yeye ndiye alianzisha na kupigania hii Kenya. Leo anaangaliwa kama mawe yaliyoko chini ya mto; mto ukipita, jiwe halisongi na ukilikanyaga, unateleza. Bw. Naibu Spika wa Muda, inafaa tungazie mambo ambayo Mzee Kenyatta alisema. Alikuwa mwanzilishi wa hii nchi. Inafaa tuangazie yale mambo ambayo Mwalimu Nyerere alisema akituhutubia. Inafaa tuangazie yale mambo ambayo Nkrumah alisema akiangazia Afrika 50 yearsbefore he was born . Kwa nini tusiangazie hayo mambo?"
}