GET /api/v0.1/hansard/entries/220663/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 220663,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/220663/?format=api",
"text_counter": 299,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili nichangie machache kuhusu Mswada huu ambao utasimamia usalama pamoja na afya ya wafanyakazi. Najua swala la njaa halijatiliwa maanani May 22, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1509 katika Mswada huu. Lakini naamini kwamba shibe au njaa ya wafanyakazi ni swala muhimu sana kuhusu afya yao. Nasema hivyo kwa sababu utakuta wafanyakazi wengi ambao wamefanya kazi hata miaka kumi bila kulipwa mishahara yao. Ukikutana na wafanyakazi hao, ni watu wa kuombaomba. Wanaomba chakula cha msaada. Wanafanya hivyo kwa sababu hawalipwi mishahara yao. Utawezaje kuongea juu ya afya ya mfanyakazi ambaye anashinda kazini na ifikapo mwisho wa mwezi, mwajiri wake hamlipi mshahara? Atahifadhi afya yake namna gani? Itawezekanaje? Nikisema hivyo, nafikiria zaidi juu ya wafanyakazi katika mashamba ya makonge katika Wilaya ya Nakuru na sehemu za Pwani. Katika mashamba ya Banita, Majani Mingi, Alfega, Wakamundu na mengine mengi, Waziri ana habari ya kwamba wafanyakazi hao wanawadai waajiri wao Kshs150 milioni. Pesa hizo hazijalipwa kwa zaidi ya miaka kumi. Tumeongea na Waziri juu ya swala hilo mara nyingi. Nimemwomba na kumpigia magoti afanye kila kitu kusuluhisha swala hilo. Lakini kila mara, ni kama anasahau. Sasa, tunampatia nguvu zaidi za kuweza kuitisha mishahara hiyo. Sijui kama atazitumia nguvu hizo au atakuwa mlegevu tena. Ukweli wa mambo ni kwamba, ikiwa Serikali hii itamaliza kipindi chake na iondoke kabla ya wafanyakazi hao kulipwa mishahara yao, sijui tutapata wapi kura. Bw. Waziri, kura hazitapatikana! Wafanyakazi hao wana uchungu mwingi. Siyo eti wanasingizia. Wanasema ukweli! Hawajalipwa mishahara yao! Sasa wanadai Kshs150 milioni. Mzungu na Mgiriki wameruhusiwa kukaa na pesa hizo kwa miaka kumi. Utashangaa ya kwamba miaka mitatu iliyopita, Mhe. Raisi mwenyewe aliamrisha wafanyakazi hao wawe wakilipwa mishahara yao. Miaka mitatu baadaye, hakuna kitu kimefanyika. Tunashindwa ikiwa kuna Wizara au sheria za kumlinda mfanyakazi au hakuna. Ikiwa Wizara haiwezi kumtetea mfanyakazi, atatetewa na nani mwingine? Vyama vya wafanyakazi viko. Ijapokuwa tunamskia Bw. Atwoli akiwaka moto, ameshindwa kuwasaidia wafanyakazi wapate mishahara yao. Kwa hivyo, hatuwezi kusimama hapa kuongea juu ya afya na usalama wa wafanyakazi na tunajua kuna wafanyakazi ambao wamenyimwa mishahara yao na hatufanyi chochote. Bw. Naibu Spika, swala hili linagusia heshima ya Mhe. Rais. Ikiwa aliamuru mishahara hiyo ilipwe, sioni ni nani anaweza kukaidi amri hiyo. Ikiwa kuna mtu amekaidi amri ya Mhe. Rais, mtu anayestahili kumtetea Mhe. Rais ni Waziri. Waziri anatakiwa kusimama aseme: \"Mhe. Rais aliamurisha mishahara ilipwe! Nataka ilipwe mara moja!\" Ikiwa watu hawawezi kuamini ya kwamba Mhe. Rais akisema jambo litafanyika, wataamini nani mwingine mwenye uwezo?"
}