GET /api/v0.1/hansard/entries/220667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 220667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/220667/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assitant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, jambo lingine ni kwamba, wafanyakazi katika mashamba ya makonge wanafanya kazi hatari. Wanashinda katika maji ya makonge katika karakana ambazo zinatengeneza majani ya makonge. Maji hayo yamejaa sumu. Wafanyakazi wanalazimika kuingia katika maji hayo bila viatu na mipira ya mikono. Bw. Boit alisema ya kwamba wafanyakazi wanaokata mikonge, mikono yao imepindika inaka kama hii--- Huwezi kuamini! Mtu hawezi kukunjua vidole vyake vikakunjuka kwa sababu amevikunja miaka nenda, miaka rudi, mpaka maumbile ya mkono wake 1510 PARLIAMENTARY DEBATES May 22, 2007 yamebadilika. Hakuna fidia wanayolipwa. Hata mishahara wananyimwa. Unashindwa hao tunaoambiwa ni wakaguzi wa wafanyakazi wanafanya kazi gani? Hawazunguki katika karakana hizo kuona hali ya hatari inayowakumba wafanyakazi wakairekebisha. Kazi yao ni kuketi ofisini tuu! Zamani walikuwa wanavaa mavasi rasmi. Siku hizi hawana sare! Wanakaa tu kama--- Sitaki kusema kama wahuni! Wanakaa kama raia! Zamani, walikuwa na sare zao ambazo ziliwapa nguvu ya kufanya kazi. Sasa, wanakaa hivi hivi! Unaweza ukasema, bila uoga wa jambo hili kukanushwa ya kwamba, wakaguzi wa wafanyakazi hawafanyi kazi! Katika hii sheria, lazima tuone vile tutailazimisha idara ya wakaguzi wa wafanyakazi ifanye kazi yake, au iwaachie watu wengine ambao wako tayari zaidi kufanya kazi hiyo. Bw. Naibu Spika, kwa nini matajiri wanakaa kama miungu? Kwa nini hakuna wa kuwaambia: \"Fanyeni hiki?\" Ni kwa nini tunawafanya waajiri wakae kama miungu? Ni kwa sababu wana ngozi nyeupe, pesa nyingi au ni kwa sababu tunawaogopa? Hili ni jambo la kutisha. Wafanyakazi wanakaa kama watumwa. Hali yao ni ya kitumwa kabisa. Sitaki kusema ya kwamba namtolea yeyote changa moto, lakini ukitembelea mashamba yanayokuza maua katika sehemu za Naivasha, utashangazwa na namna wafanyakazi wetu wanavyowekwa katika hali mbaya. Ukiangalia uso wa mfanyakazi ambaye analipwa mshahara na uulinganishe uso huo na mtu ambaye anangoja mlangoni kuajiriwa kazi katika shamba hilo, utakuta ya kwamba uso wa anayengoja kuajiriwa kazi una afya zaidi kuliko aliyeajiriwa. Sura ya aliyeajiriwa imechunjuka na kukaa vibaya kwa sababu ya kemikali ambazo wanatumia. Wanashinda wakinusa kemikali hizo na hawapewi chakula wanachofaa kupewa - kwa mfano, maziwa. Pia, hawalishwi vizuri. Wakiugua, hakuna matibabu. Unashindwa ni kwa nini Waziri hajachukua jukumu la kutembelea mashamba hayo na kutazama vile wafanyakazi wanavyokaa, na kutafuta suluhisho la matatizo yao. Mtu anayefanya kazi anastahili kuonekana kama mtu anayekula vizuri. Mtu hawezi kuwa anafanya kazi na sura yake inazidi kuwa mbaya. Sura yake inachunjuka mpaka unadhani amekatwakatwa uso au amekwaruzwa uso na kitu fulani. Ni lazima Waziri aelewe ya kwamba haitoishi kumpatia nguvu za kisheria, ikiwa hatakuwa tayari kutekeleza sheria hii. Mpaka sasa, tunaweza kusema ya kwamba zile sheria ambazo tumekuwa nazo, hakuzifanyisha kazi. Swali ni: Atatekeleza sheria hii au ataendelea kulala? Nasema \"kulala\" kwa sababu mambo hayo hayana msuluhishi. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya kazi ya Waziri! Kazi aliyopewa ni yeye tu pekee anayeweza kuifanya. Lazima aamke na aamke na Wizara yake, ateremke kule kunapofanyiwa kazi na awapatie wafanyakazi wetu ulinzi. Wanastahili ulinzi. Ni haki yao!"
}