GET /api/v0.1/hansard/entries/220680/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 220680,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/220680/?format=api",
"text_counter": 316,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Haya, Bw. Naibu Spika. Lakini tunaelekea kule. Tutakapompa sheria hiyo basi aamke pamoja na maofisa wake. Anasema ukosefu wa sheria ulifanya walale kazini. Tukipitisha Mswada huu sioni sababu ya wao kuendelea kulala. Ni lazima waamke na kuwatetea wafanyakazi. Hakuna Wizara muhimu kuliko hii katika maisha ya wafanyakazi. Ninakumbuka vizuri Wizara hii ilikuwa maarufu sana ilipokuwa ikisimamiwa na marehemu Tom Mboya. Umuhimu wake umekuwa ukididimia. Ni lazima Waziri awatetea wafanyakazi, hasa wale wanyonge. Kwa sababu yeye ndiye mwenye uwezo, ni lazima afanye kazi zaidi."
}