GET /api/v0.1/hansard/entries/220683/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 220683,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/220683/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ninashangaa kwa nini mheshimiwa anaogopa Mswada huu. Tuko hapa kuongea na hiyo ndio kazi yetu. Dunia nzima inalia ya kwamba tunalipwa mishahara mikubwa sana halafu tena tuogope kuongea? Tutashitakiwa kwa ufisadi. Tunakuja hapa tunakula pesa na 1512 PARLIAMENTARY DEBATES May 22, 2007 wakati wa kuongea, hatupatikani. Bw. Naibu Spika, sitaongea zaidi. Kuna makampuni ambayo yamekuwa na sifa mbaya kwa muda mrefu sana. Hii ni sifa ya kutojali afya na usalama wa wafanyakazi wao. Mfano ni kampuni ya Eveready. Nakumbuka zamani sana kama miaka 20 iliyopita nilipokuwa mhe. Mbunge hapa, nilikuwa nalia juu ya wafanyakazi wanaolazimika kupuliza kemikali wakati wakufanya kazi katika kiwanda hicho. Wanapougua unakuta kampuni badala ya kuchukua jukumu la kuwasaidia inaajiri wakili ili aseme wafanyakazi hao hawakupata ugonjwa hapo kiwandani. Si vizuri kuona mfanyakazi hawezi akasaidiwa na madawa au matibabu mpaka ashitaki kampuni. Jambo mbaya zaidi ni kwamba waajiri wengi huepa kuwasaidia wafanyakazi kupata matibabu kwa kuwatimua kazini wanapokuwa wagonjwa. Wakiwa kule nje, hawana nguvu za kushitaki makampuni au waajiri wao. Utamkuta anakimbia kwa waheshimiwa Wabunge, diwani au anatamauka na kungojea kifo. Hii sheria lazima ioneyeshe wazi ya kwamba mwaajiri hatakuwa na haki ya kumfukuza mfanyakazi kazini kwa sababu ameugua ugonjwa. Hakuna mfanyakazi anayeugua kwa mapenzi yake. Hakuna mfanyakazi angetaka kuwa mgonjwa. Ni makosa makubwa kama vile tunavyosema hata waliougua ugonjwa wa UKIMWI, hawawezi wakafutwa kazi kwa sababu ya ungonjwa huu. Wale wengine ambao afya yao inadhoofika wakiwa kazini, ni lazima sheria iwalinde. Sheria hii inatakiwa ilazimishe matibabu kwa mfanya kazi aliyepata ugonjwa akiwa kazini. Inafaa iseme kwamba mtu akipata ugonjwa kazini, atatibiwa mpaka apone. Hilo lifanyike kama haki, si kama kitu ambacho unapata mwajiri akipenda na hupati kama hapendi. Ni lazima iwe kuwa mtu akiugua akiwa kazini hawezi kufutwa kazi, na atashughulikiwa kimatibabu mpaka apone bila ya kukatwa mshahara au kusumbuliwa kwa namna nyingine, kwa sababu hivyo ndivyo kuwasaidia wafanyakazi kufanya kazi katika hali ambayo ni ya usalama na afya. Bw. Naibu Spika, nitamalizia kwa kumkumbusha Waziri lile nililoongea kuhusu namna wafanyakazi hawawezi kuhifadhi afya yao kama hawana mshahara. Ningemkumbusha Waziri kwamba wafanyakazi wa mashamba ya Banita, Alfega na Majani Mingi sasa wamekaa miaka kumi wakimdai mwajiri wao, ambaye Waziri anamjua vizuri, zaidi ya Kshs150 million ambazo hazijalipwa. Ninamwomba Waziri, ili aonyeshe kwamba atakuwa mfanyakazi tofauti, kwa sababu yeye pia ni mfanyakazi. Namwomba atafute nafasi mwishoni mwa wiki au mwanzoni mwa wiki ijayo, atembelee mashamba yale ili ahakikishe kwamba mwajiri yule amewapa wafanyakazi wake mishahara yao. Si haki mheshimiwa Waziri. Si haki. Wewe mzigo huu utaubeba kwa dhamira na pia kwa mabega yako. Tunakubebesha mzigo huu kwa sababu wewe ndiye mwenye nguvu. Unatazamwa na wafanyakazi hawa. Serikali inakutazama wewe. Usipotimiza hili, utakosa kuingia Mbinguni. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}