GET /api/v0.1/hansard/entries/221249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 221249,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/221249/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Raila",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 195,
"legal_name": "Raila Amolo Odinga",
"slug": "raila-odinga"
},
"content": "iliundwa kutoka juu ikaletwa chini. Baada ya miaka mingi ambapo nchi zote zilikuwa na shida za kibiashara na mawasiliano, baadaye iliamuliwa kwamba tuanze tena upya na ikasemekana kuwa mara hii, tutaanza chini tukielekea juu; yaani kumaanisha kwamba tutajumuika kama wananchi kushauriana ili shirikisho hili likiundwa, litakuwa lenye msingi wa kudumu. Hii ndiyo sababu Katiba hii mpya ilipoandikwa, iliwekwa kuwa ni lazima ipitishwe na bunge za nchi 1358 PARLIAMENTARY DEBATES May 16, 2007 hizi zote. Sisi katika Bunge hili, nakumbuka kwamba tulijadiliana sana kuhusu katiba hii mpya na tukaipitisha yote bila kupingwa. Ndiyo baadaye ikapelekwa, ikawekwa sahihi na ikawa sheria. Bw. Naibu Spika, kama kulikuwa na shida, mimi nataka kusema kwamba Fungu la 150 linasema kwamba lazima kama kuna mabadiliko, yaidhinishwe na nchi hizi zote tatu. Serikali yetu hii ina viungo vitatu: Kuna Bunge, Serikali kuu na Mahakama. Bunge ndio limepewa wadhifa wa kipekee katika sheria ya nchi hii kupitisha Katiba kama hii ya Afrika Mashariki; sio Cabinet au Baraza la Mawaziri. Kwa hivyo, mimi naweza kusema kwamba ni ukiukaji mkubwa wa sheria kwa Mkuu wa Sheria kwenda kupotosha Baraza la Mawaziri kwa kuwaambia kwamba wanaweza kuidhinisha, kuweka sahihi na kupeleka Arusha. Halafu ukienda Arusha, inawekwa kule kwamba Kenya tayari imeshabadilisha hiyo sheria, na sahihi iliyoko kule ni ya Bw. Tuju! Bw. Tuju ni Mjumbe wa Bunge hili, na yeye ana haki ya kuja hapa na kujadiliana na Wajumbe hapa. Bw. Naibu Spika, hili Baraza la Mawaziri na Serikali hii ni Serikali ambayo ina ulafi mkubwa, maanake shida ni juu ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ambayo inatakikana iwe kule. Ni wao wenyewe ambao wanataka kuchukua nafasi hizi peke yao! Shida sana ni juu ya wawakilishi wa chama cha National Rainbow Coalition (NARC). Hiyo ndiyo shida hapa! Bw. Naibu Spika, tulienda kuwinda wanyama pamoja. Tulipomuua huyu mnyama, wenzetu upande ule wakawa sasa wachoyo na walafi. Wanataka kuchukua miguu, mikono, shingo, kichwa, hata matumbo yote ndani, na hata ngozi! Wanachukua yote peke yao!"
}