GET /api/v0.1/hansard/entries/221251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 221251,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/221251/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Raila",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 195,
        "legal_name": "Raila Amolo Odinga",
        "slug": "raila-odinga"
    },
    "content": "Hii ndio sababu Afrika Mashariki inakuwa na shida, juu ya ulafi wa hawa ndugu zetu. Hakuna shida nyingine! Maanake, ukichukua huu mseto wetu wa NARC, tulipokwenda kule, ndugu mkubwa alikuwa ni Liberal Democratic Party (LDP). Kati ya Wabunge 126 ambao NARC ilipata, 62 ilikuwa kutoka upande wa LDP. Democratic Party (DP) ilipata viti 38, FORD(K) ikapata viti 20 na National Alliance Party of Kenya (NAK) ikapata viti Sita. Kwa hivyo, yule ndugu mkubwa katika mseto wa NARC ni LDP! Walipokwenda kule kuteua Baraza la Mawaziri, DP ilipata Mawaziri tisa na LDP ikapewa Mawaziri saba. Baadaye, wanasema kuwa NARC imekufa kwa sababu wao ni kama fisi; wanakula peke yao. Bw. Naibu Spika, sisi tunasema kuwa tunataka tugawe sawa. Hii ndio imefanya kazi yote ya Afrika Mashariki kusimama. Uganda na Tanzania hawana shida. Ni Wakenya ndio wana shida. Walipokwenda kule na kusema kuwa wanataka sheria ibadilishwe, Watanzania wakawa wangwana na wakapeleka katika Bunge lao na ikapitishwa. Hao wamekataa kuleta katika Bunge hili maanake wanajua wakileta hapa watashindwa. Ndio kwa sababu wanataka kuchukua ile njia nyingine. Tunajua ya kwamba chui hawezi kubadilisha madoadoa yake. Lakini nataka kuwaambia ndugu zetu ya kwamba wakati utawadia. Leo ni wewe na kesho itakuwa ni mimi! Tuelewane sawa sawa. Tuilete hiyo sheria hapa ibadilishwe. Lakini jambo la muhimu zaidi ni tukubadiliane tuwachague wale Wabunge wa Afrika Mashariki tukikubaliana. Wachukue na pia watuachie sisi vile vile kama LDP. Nafasi ni tano lakini tunasema wachukue nafasi tatu, ingawaje sisi ni wengi zaidi, watuachie nafasi mbili peke yake. Nafasi mbili peke yake! Najua tutashikana tena miereka na wao hata kama watajaribu kuiba kama ambavyo wameiba kule Magarini, shauri yao. Sisi tuna hakika kuwa wakati utafika na ukweli utajulikana. Waswahili wanasema ukweli ukidhihiri, uongo hujitenga. Kwa hivyo, nasema katika Hoja hii tukubaliane bila pingamizi yoyote eti ni jukumu na haki ya Bunge hili, kisheria na Kikatiba, kubadilisha hio sheria ili tupitishe hii Hoja kwa kauli moja. Bw. Naibu Spika, vile vile tuendelee na tukubaliane maanake KANU haina shida. Wameteua bila shida! FORD(P) pia hawana shida. Wameteua bila shida yoyote! Shida ipo katika May 16, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1359 mseto wetu wa NARC. Waziri ambaye anahusika na mambo ya Afrika Mashariki, kwa bahati nzuri, ni wa KANU; ingawaje sasa anakula upande mwingine."
}