GET /api/v0.1/hansard/entries/221258/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 221258,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/221258/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Raila",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 195,
        "legal_name": "Raila Amolo Odinga",
        "slug": "raila-odinga"
    },
    "content": "Mr. Deputy Speaker, Sir, I do not want it! I do not need information. He will have a chance to speak! Atakuwa na fursa ya kuongea na atasema yote anayopenda kusema. Ninayosema ni kwamba mambo ya uhusiano baina ya Afrika Mashariki ni muhimu zaidi. Ukienda Rwanda ndio utajua umuhimu wa uhusiano huu. Watu wa Rwanda wanalia kuwa wanataka kuingia kwa dhati hapo ndani. Burundi vile vile! Tutatengeneza soko kubwa zaidi. Wakati huu ndio mazungumzo ambayo yanaendelea. Bw. Waziri amenialika niende kwa Kenya Broadcasting Corporation (KBC) nizungumze na Wakenya juu ya umuhimu wa huu uhusiano. Kwa hivyo, tunatengeneza! Tutatengeneza shirikisho kubwa ambalo litaheshimika ulimwengu mzima. Hii ni kwa sababu litakuwa soko kubwa la zaidi ya watu milioni 100. Tunataka tushirikiane na tutembee pamoja bila pingamizi lolote kama ndugu na kama tumeelewana. Tuonyeshe, kama Kenya, kuwa sisi tuko mstari wa mbele, ili ndugu zetu watakuja pamoja na sisi. Tusiwe tunapigana hapa Kenya juu ya mambo yasiyokuwa na msingi. Ningependa kumsihi Bw. Waziri apige moyo wake konde mara tatu. Kwanza, yeye ni mtu wa Afrika Mashariki. Pili, yeye ni mzalendo wa Afrika Mashiriki. Tatu, anataka kuona kama wananchi wote wa Afrika Mashariki wameungana pamoja. Ikiwa yeye na mimi ndio tukiungana pamoja, najua yeye hatakuwa na jibu lingine ijapokuwa kuunga mkono, kwa kauli moja Hoja hii ili tutembee pamoja. Aachane na wale walafi wachache. Yeye hajui siasa ya ndani na NARC kwa sababu yeye si mwanachama wa NARC. Awaache watu wa NARC wapigane wenyewe. Yeye kama mwanachama wa KANU yafaa akae kama mwanachama wa KANU na aunge mkono haya mambo ili tuweze kupitisha kwa kauli moja Hoja hii, ili Serikali ya Afrika Mashariki iweze kufanya kazi. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, naunga mkono."
}