GET /api/v0.1/hansard/entries/221265/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 221265,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/221265/?format=api",
    "text_counter": 216,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Capt. Nakitare",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kuchangia Hoja hii ya Muungano wa Afrika Mashariki. Ni muhimu kuelewa chanzo cha muungano huu. Bunge hili lina uwezo kama bunge zingine tatu kubadili mwongozo wa nchi tatu za Afrika Mashariki. Kifungu 150 katika Katiba ya muungano wa Afrika Mashariki ni kipengele ambacho kinaongoza vichwa vya watu wote. Sasa ni miaka minne tangu Rais watatu wa nchi za Afrika Mashariki wakae pamoja ili kuangazia mambo yanayohusika katika kuanzisha muungano wa Afrika Mashariki. Nikiwa mmoja wa wale watu ambao walifanya kazi chini ya muungano wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa na Bw. Nyerere, Bw. Obote na Bw. Kenyatta, ilikuwa mshangao mkubwa kwetu wakati maangamio yalitokea na huu ushirikiano ukafupishwa kwa sababu ya mzozo wa kikatiba na fedha. Mzozo ambao unatokea, chanzo chake ni hapa. Ikiwa Mawaziri wana uwezo wa kupindua sheria za nchi tatu kwa niaba ya watu wa Kenya, na ilhali Bunge halina fahamu kwamba kuna mikutano ya Mawaziri ambao una lengo la kubadili mwendo wa ushujaa wa nchi yetu, inatatanisha. Bw. Naibu Spika, swali langu ni hili: Iwapo hili Bunge lina uwezo wa kujielekeza na mambo yake kibinafsi, Mawaziri wangelikuwa na uwezo wa kubadilisha mambo ya Bunge? Ikiwa Mawaziri wangelikuwa wanachaguliwa nje ya Bunge kama nchi zingine ambapo si lazima Waziri awe Mbunge. Bunge lina uwezo. Ni kifunguo cha sheria. Kulikuwa na mikataba mingi katika Afrika Mashariki ambayo ilikuwa inaangazia masuala ya Shirika la Reli, bandari, East African Airways, masomo na kadhalika. Haya mambo yote yalikuwa na lengo la kuambatanisha watu wa Afrika Mashariki. Itakuwa vigumu sana kwa sisi wenyewe kama hatupewi uwezo katika hili Bunge kujadiliana na kurekebisha matatizo ya mikataba kama hiyo, tuwe tunawaachia waliochaguliwa kama Mawaziri nchini mwetu. Tutakuwa kama tunaongozwa na vipofu. Kwa sababu Waziri wa Afrika Mashariki angelikuwa anaishi Arusha, kwa sababu yeye ni Waziri wa Afrika Mashariki. Yeye na msaidizi wake wanatakikana May 16, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1363 kukaa Arusha na sio kwamba wanakaa hapa Kenya na wanafanya kazi Arusha. Wale Wabunge walioteuliwa na ambao wanatakikana kukaa Arusha hawana hata nafasi katika Bunge hili ili kuangazia mambo ambayo yanaendelea katika nchi yao. Hivi sasa, hata hao Wabunge wenyewe hawajui tunazungumza juu ya Muungano wa Afrika Mashariki. Labda lengo lao lilikuwa kutuletea mawaidha ama shida ambazo wanapata Arusha. Mswahili alisema: \"Usipokuwepo na lako halipo.\" Hao watu ambao hawapo, ndio waliochaguliwa kwenda katika kikao cha Bunge la Afrika Mashariki. Wanatakikana kuwa wanatengeneza sheria za nchi hizo zote. Kuna upungufu hapa, ambapo ni lazima tuangazie. Bunge pekee ndilo lina uwezo wa kubadilisha sheria, kwa sababu ni hilo Bunge ambalo linatunga hizo sheria. Mawaziri hawana uwezo wa kurekebisha sheria. Ni lazima tuangazie hayo mambo."
}