GET /api/v0.1/hansard/entries/221267/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 221267,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/221267/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Capt. Nakitare",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Muite alituarifu kwamba kipengee 152 kina tatizo kwa sababu hakifuatwi. Mtu amewacha njia ambayo ni pana na inatuelekeza katika Afrika Mashariki ili tulete watu wetu katikati na tuwe tunazungumzia mambo haya. Tumepotea kwa sababu tunajaribu kuwachia watu ambao hawafai kubadilisha mwendo wa sheria ili kutuongoza. Bw. Naibu Spika wa Muda, uwezo wa Bunge ni nini? Kama hiki kipengee kingalikuwa kimetengenezwa na watu wa Bunge wenyewe, wangeshauriana na Wabunge wenzao kutoka nchi hizi zingine. Nimekuwa na mazungumzo na hao Wabunge wa Afrika Mashariki na wana ugumu. Hata wale ambao walichaguliwa hapa, hawana uwezo wa kutembelea Ikulu ya Kenya tangu wachaguliwa. Ni Waziri pekee ndiye ana uwezo wa kuzungumza na Rais wa Kenya. Je, hao watu walipelekwa huko kama senema? Je, hili Bunge linajua kwamba hao Wabunge wana shida kama hiyo? Mishahara yao inajadiliwa na nani? Tungalikuwa na kipengee ambacho kinaweza kurekebisha mambo hayo yote. Shughuli za Secretariat zimekwama kwa sababu hatusikizani. Ijapokuwa wanasema Customs Treaty ambayo itakuwa ndiyo njia pekee ya kupata pesa ya kugawia hizo nchi nne, je kama nchi moja itakosa kutoa pesa ili waletwe katika kile kikao, itakuwaje? Huo Muungano wa Afrika Mashariki utaanguka kama ule wa kwanza. Je, na kama Nchi moja itakosa kutoa pesa ili ziwekwe katika kile kikapu, itakuaje? Si hii Jumuia ya Afrika Mashariki itaanguka vile ile ya kwanza ilivyoanguka? Ya kwanza ilianguka kwa sababu ya kutosikizana na kuchangiana. Nchi moja ikisema haina pesa, nchi mbili zinasema kama nchi hii imekataa kutoa pesa, basi hakuna mishahara kwa watu. Sisi hatungependa kuona kwamba Afrika Mashariki inaongozwa na watu wachache. Isitoshe, hii nyumba ilijengwa kutoka juu. Sasa itakuwa ngumu kufundisha wananchi kuelewa ujamaa wa Afrika Mashariki ni nini. Mipaka hii ambayo tuliwekewa na Wakoloni inaleta vikwazo. Kuna vita kati ya makabila kutoka nchi jirani. Tutawapatanisha hawa watu namna gani, kama sisi wenyewe hatuwezi kusimamia hizi sheria, na kusema tumepanga kama Wabunge wa Kenya sheria iidhinishwe na Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi? Hayo mambo ndiyo yataweza kuwa ya maana kuliko kusema kwamba kilichofanywa na Cabinet ndicho uamuzi wa mwisho. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}