GET /api/v0.1/hansard/entries/22138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 22138,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/22138/?format=api",
"text_counter": 435,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante sana Bwana Naibu Spika wa Muda. Hoja hii ni ya muhimu sana haswa wakati huu Wakenya wanaposherehekea ushindi mkubwa ulioletwa na wanariadha wetu. Wanariadha hawa, haswa wa kike, wametuwezesha kuchukua nafasi ya tatu ulimwenguni. Akina mama Wakenya wamefanya kazi ya maana sana. Kazi hiyo haijawahi kufanywa miaka hii yote. Kwa siku nyingi sana, wanariadha wamekuwa waking’ang’ana wenyewe bila usaidizi. Ningependa kuchukua fursa hii kusema ya kwamba Waziri wa Maswala ya Vijana na Michezo anafaa kuhakikisha yakwamba wanariadha wanapewa usaidizi mkubwa hasa wakati wanapofanya mazoezi. Nchi nyingi duniani huwa na shule ambazo wanariadha huenda na kufuzu ili wajihusishe katika mbio na michezo kama vile ya mpira ili waweze kujiendeleza. Ukienda katika nchi kama vile Brazil, utapata kwamba wanamichezo wote wanapatiwa nafasi ya kujifunza ili waanze mapema wanapokuwa shule. Akina mama wamefanya kazi kwa bidii na ningependa kutoa pongezi hasa katika Jumba hili la kifahari na kusema kwamba wametuweka katika ramani ya ulimwengu. Ningependa haswa kumpongeza mwanariadha Vivian Cheruiyot aliyetupa medali mbili za dhahabu. Mrembo yule ametuweka mahali pengine katika hali ya michezo ulimwenguni. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono wenzangu kuwa Serikali yetu iendelee kuwasaidia wanariadha hapa nchini. Ninapendekeza Serikali iwe na hazina maalum ya kuwasaidia wanariadha ili wafaidike katika maisha yao. Si kila wakati wanapokimbia wanalipwa pesa nyingi. Kuna mbio ambapo wao hulipwa lakini mara nyingi hawapati fidia ya kutosha. Kwa hivyo, kama motisha, ni lazima Serikali yetu itenge hazina ya kuwasaidia wanariadha wetu ili waweze kutia bidii katika mashindano ya dunia. Kwa hayo machache, ninaomba kuunga mkono."
}