GET /api/v0.1/hansard/entries/22140/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 22140,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/22140/?format=api",
    "text_counter": 437,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, timu ya Gor Mahia ilishinda kombe la Barani Afrika la kandanda mwaka wa 1987. Ushindi huu ulitokea baada ya wao kujaribu miaka nenda miaka rudi. Hata hivyo, wakati timu hiyo iliporejea hapa nyumbani haikutambuliwa wala kutunukiwa heshima yoyote. Hata leo timu hiyo haijawahi kutambuliwa kwa ushindi huo. Kenya ina wachezaji wengi wanaotuletea heshima na sifa duniani. Nchi ya Uganda ilikuwa na mkimbiaji mmoja tu kwa jina la John Nakibwa ambaye alishinda medali moja. Leo hii ukienda Uganda utaona barabara inayojulikana kwa jina lake. Sisi Wakenya tuna shida moja ya kukosa kujitambua na kujiamini. Ingelikuwa ni nchi zingine zilizopata medali kama Kenya kule Daegu, sifa zao zingeenea kote ulimwenguni. Je, ni njia gani mwafaka ya kuweza kuwasaidia wanariadha wetu? Pendekezo langu ni kuwa ikiwa mtu amefaulu katika mbio au mchezo wote ule, atambuliwe na kupewa kazi katika wizara zetu. Hii ni njia mojawapo ya kuwatia shime wanariadha wetu. Ikiwa wanafanya kazi katika kikosi cha polisi au jeshi letu, basi wapewe madaraka ya juu na tuimarisha mishahara yao. Jambo la tatu ni sisi kuwatambua watu wote waliyoiletea nchi hii sifa katika miaka iliyopita. Watu hawa wanastahili pensheni ya kutosha ili wajikimu maishani. Ni lazima tuwape bima ya kuwagharimia matibabu na mahitaji mengine maishani. Hii ni kwa sababu hawa ni mashujaa wetu waliovuma na kuiletea sifa nchi hii wakiwa vijana. Nchi hii ni tajiri sana ikiwa inaweza kutumia pesa na rasilmali zake vilivyo. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}