GET /api/v0.1/hansard/entries/22141/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 22141,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/22141/?format=api",
"text_counter": 438,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa sababu ya Vivian Cheruiyot, Edna Kiplagat, David Rudisha, Abel Kirui, Asbel Kiprop na Ezekiel Kemboi. Wimbo wa taifa hili letu uliimbwa mara saba katika mji wa Daegu kule Korea Kusini, na bendera ya taifa hili ilipandishwa na ikapepea katika taifa hilo la ugenini. Wahenga walinena kwamba chanda chema huvikwa pete. Kwa hivyo, taifa hili halina budi ila kuvikwa pete ya dhahabu kwa kila moja wa hawa mashujaa wa Kenya, ambao wametuletea heshima kubwa na adhi nyingi kuliko yoyote ambayo tumewahi kushuhudia. Lakini tunapowasifu, ni juu yetu kutufakari na kujiuliza: Ni kwa nini hatuwekezi katika mipango yetu, muundo msingi wa kusaidia wanaspoti katika taifa hili kujiendeleza? Utaona kwamba kati ya hawa Wakenya 17 ambao wametuletea medali, wengi wanatoka katika kaunti ya Nandi, lakini ukienda katika mji wa Kapsabet, hakuna uwanja wowote ambao uko katika hali ya kuweza kuwasaidia wanaspoti. Ukitazama uwanja wa Kipchoge mjini Kapsabet, ni uwanja ambao umechakaa. Ni uwanja ambao Serikali haijaonyesha nia yoyote ya kuweza kuinua hali yake."
}