GET /api/v0.1/hansard/entries/22142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 22142,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/22142/?format=api",
    "text_counter": 439,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Namwamba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 108,
        "legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
        "slug": "ababu-namwamba"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ni lazima pia tuchukue hatua ya kuweza kuandaa michezo ya kimataifa kama hii. Mara ya mwisho ambapo Kenya iliandaa michezo ya adhi kuu ni mwaka wa 1987, wakati tulipoandaa michezo ya bara la Afrika. Mwaka wa 1999, tulikuwa tumepewa nafasi ya kuandaa michezo ya soka barani Afrika, lakini tukapoteza nafasi hiyo na ikapewa Afrika Kusini kwa sababu ya migororo ndani ya Serikali. Kwa hivyo, ni changamoto vilevile kwa Serikali kuonyesha heshima kwa wanaspoti wetu; inafaa tuweze pia kujitayarisha kuandaa michezo kama hii na kuwekeza katika miendo misingi."
}