GET /api/v0.1/hansard/entries/222987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 222987,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/222987/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii nafasi kuchangia Mswada huu kuhusu ajira. Kwa kuanza tu ningesema kwamba huu Mswada tumeusubiri kwa miaka mingi sana, kwa sababu sheria nyingi za nguvu kazi ni sheria ambazo zimekuwa za kikoloni. Ingawa Waziri amechelewa katika kuleta Mswada huu Bungeni, haidhuru ni bora kuchelewa kuliko kutokuja. Mambo haya na sheria hii inahusu haki za wafanyakazi; lakini katika mfumo wa ubepari. Kwa hivyo, kutoka mwanzoni, mimi naelewa kabisa kwamba, sio kwamba sheria hii itamkomboa mfanyakazi. Hii ni sheria ambayo itampatia mfanyakazi uwezo wa kupambania haki zake zaidi. Sheria zilizokuwa hapo mwanzoni, zile za kikoloni, zilikuwa sheria zilizotungwa makusudi kabisa na wakoloni kupambana dhidi ya mfanyakazi kabisa ili asipate uwezo wake. Bw. Naibu Spika wa Muda, Mswada huu unahusu hasa washikadau watatu; Wizara ya Leba na Ustawi wa Wafanyakazi, mwajiri na mwajiriwa. Kwa sababu sheria haitoki hewani bali inatoka katika hali halisi ya kihistoria, tukichunguza historia ya nchi yetu, ni wazi kabisa kwamba Wizara ya Leba na Ustawi wa Wafanyakazi imekuwa kama mbwa ambaye hana meno. Nakumbuka kuwa nishawahi kuuliza Swali hapa Bungeni, nikamwita Waziri wa Leba na Ustawi wa Wafanyakazi hata akaenda kuzuru Taita Sisal Estate, Mwatate. Vile vile, alienda kuzuru Salt Lick na Taita Hills Lodges na aliona gandamizo na nyanyaso ambazo ziko hapo. Lakini alipokuwa huko, ni kama kulia machozi ya mamba. Tangu atoke huko akiwa Waziri wa Leba na Ustawi wa Wafanyakazi, hakuna chochote kilichobadilika huko. Jambo hilo linahusu sehemu nyingi. Waziri wa Leba na Ustawi wa Wafanyakazi anaelewa kuhusu nyanyaso zinazoendelea dhidi ya wafanyakazi kila pahali katika nchi, lakini ni kana kwamba Serikali, ikiongozwa na Wizara ya Leba na Ustawi wa Wafanyakazi, haina nguvu zozote za kufanya chochote. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika wa Muda, ndani ya sheria hii, kama ingeweza kusaidia, ingawa najua kabisa kuwa, katika mfumo wa kibepari, Wizara ya Leba na Ustawi wa Wafanyakazi inakuwa katika upande wa wanyonyaji na wagandamizaji. Lakini kama ingekuwa--- Haidhuru, kuna nia ya kujaribu kubadilisha na kwenda mwelekeo mwingine pale tunaelekea, ambapo wafanyakazi watakuwa na nguvu katika nchi hii, Wizara ya Leba na Ustawi wa Wafanyakazi ingekuwa na meno zaidi katika nchi hii. Kwamba, hii sheria isiwe ya kulilia wafanyakazi. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukiisoma sheria hii kwa jumla, utaona kwamba sehemu nyingi ni zile za kufanya kwamba mwajiri eti anaweza kuwahurumia wafanyakazi; eti anaweza kuwahurumia na kuwasaidia wafanyakazi. Eti tunafuata--- Haidhuru, mwajiri afanye jambo fulani ambalo ni nzuri. Ni kama kumwomba mwajiri. Inajulikana kwamba mwajiri hawezi kumpa mfanyakazi nguvu pasina mfanyakazi mwenyewe kupambania haki yake. Kwa hivyo, inakuwa kwamba, katika hali kama hii yetu tuliyoko na tukiangalia historia yetu, jambo ambalo ningesisitiza zaidi, maanake tunajua kwamba kabla hatujaondoa huu mfumo wa ubepari, Wizara ya Leba na Ustawi wa Wafanyakazi itakuwa ikilia machozi ya mamba katika nchi; haiwezi kufanya chochote. 1254 PARLIAMENTARY DEBATES May 9, 2007 Kwa hivyo, nguvu nyingi zingeweza kwenda katika vyama vya wafanyakazi. Vyama vya wafanyakazi havijaimarishwa zaidi katika sheria hii. Namuomba Mheshimiwa Waziri kuwa, wakati tutakapoleta marekebisho ambayo yatatilia nguvu kabisa vyama vya wafanyakazi, ni muhimu kwamba yaungwe mkono, kama kuna nia. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu mpaka sasa, lazima sheria yenyewe izungumzie kwa undani kuhusu vyama vya wafanyakazi. Hiki chama cha wafanyakazi kinachoitwa Central Organisation of Trade Unions (COTU), mpaka sasa, wafanyakazi wengi wa nchi yetu wanalia kwamba kinawasaliti; kimenunuliwa na waajiri. Chama cha wafanyakazi ambapo ndani yake hakupatikani haki za wafanyakazi, kinawezaje kutetea wafanyakazi? Chama cha wafanyakazi ambacho kinazungumzia maslahi ya mwajiri, kinawezaje kuwatetea wafanyakazi? Kwa hivyo, lazima sheria hii izungumzie kuhusu wafanyakazi."
}