GET /api/v0.1/hansard/entries/224067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 224067,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/224067/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza hapa Kenya mwaka wa 1992, imechukua muda mrefu sana kuleta Mswada kama huu hapa Bungeni, ili tuwe na sheria ya kurekebisha maswala ya vyama vya kisiasa. Kwa hivyo, ningependa kumpongeza Waziri Martha Karua kwa kufanya kazi hii ambayo tulikuwa tunaingoja kwa muda mrefu. Lakini, kuna mambo mengi ambayo lazima yaangaliwe. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa heshima yako, ningependa kukubaliana na wenzangu wote waliochangia Mswada huu. Ningependa tu kutaja mambo mawili au matatu. Tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza, tumekuwa na tabia ya ajabu - udoezi wa kisiasi! Tukidoeadoea namna hiyo, vyama hivi havitaweza kutegemewa. Hatutaendelea na mfumo huu kwa muda mrefu. Bila sheria hii, mfumo wa vyama vingi unaweza kupotea. Kwa hivyo, jambo hilo la udoezi ni lazima likomeshwe kwenye sheria hii mpya. Nafikiria tukianzisha hiyo sheria, itakuwa ni rahisi kukomesha tabia hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, ningependa kuzungumzia juu ya mfuko huo wa fedha ambao utasaidia vyama vya kisiasa. Ni rahisi kwa watu kusema kwamba akina mama wawekwe kwenye vyama kuanzia mashinani. Lakini, tayari, akina baba wanaibuka na hasira kwa sababu wameshatumia kura za akina mama kufika hapa. Kwa hivyo, akina mama hawana faida yoyote. Ningependa kusema sioni ni kwa nini wanaume wanakuwa na wasiwasi. Sio rahisi kwa wanaume April 26, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1009 kufika hapa bila kura za akina mama. Kwa hivyo, tusiwatumie akina mama kwa ubwete. Tufike hapa bure halafu, tukishafika hapa, tuamue kuwa hatuwahitaji akina mama. Kuna umuhimu wa akina mama kuwekwa katika mashina ya vyama. Hata kitaifa, akina mama inapaswa wapewe asilimia 30 ya nafasi za kazi. Mhe. Rais alitaja mwezi wa Oktoba mwaka jana kwamba akina mama wahusishwe katika kila kitu kwa asilimia 30. Akina mama wahusiswe sio tu katika kazi za kuajiriwa na vyama, bali kwenye shughuli zote zinazotekelezwa nchini. Vile vile, licha ya kupendekeza kuwa akina mama wahusishwe kuanzia mashinani, ni lazima pia tuweke asilimia ya kura ambazo vyama vitatakiwa kupata ili vinufaike na mfuko huo. Pendekezo langu lingekuwa asilimia 15 ya fedha hizo ziwekwe kando ili tuhakikishe akina mama wamehusishwa kutoka mashinani hadi kitaifa. Hilo litakuwa jambo la muhimu. Vile vile, tungepende ile tume ya uamuzi kuhusu vyama vya kisiasa pia ihusishe akina mama. Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii."
}