GET /api/v0.1/hansard/entries/224564/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 224564,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/224564/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Achuka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 353,
        "legal_name": "Francis Achuka Ewoton",
        "slug": "francis-ewoton"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Yangu ni machache. Ningetaka kuomba Bunge hili lirekebishe maneno ya kuandikisha vyama vingi hapa nchini. Vyama vingi sasa vimetambaa kote nchini. Kama vile Waswahili walivyosema, wingi wa kila kitu ni sumu. Kwa hivyo, tukiendelea kuwa na vyama vingi nchini, vitatawanya wananchi. Kwa hivyo, ningeomba tujaribu kutambua vile vyama ambavyo vinaweza kuongoza nchi hii kwa utaratibu na kuifanya iwe na demokrasia ya ukweli. Ningependekeza tuwe na vyama vitatu au vinne kama vile inavyofanyika kule Amerika au Uingereza. Kule Amerika, ambapo kuna watu wengi kuliko Afrika, kuna vyama viwili tu. Kwa nini nchini Kenya ambako kuna watu wachache kuliko Amerika, tuwe na vyama zaidi ya 30? Kwa hivyo, mapendekezo yangu April 25, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 943 ni tuongee pamoja na tukate kauli kwamba tutakuwa na vyama vichache. Hii itafanya shughuli ya kuhudumia wananchi kuwa rahisi na ya haki. Jambo lingine ni kuhusu wale watu wanaowania viti vya Bunge, ambao wakikosa kuchaguliwa katika chama fulani wanahamia kwa chama kingine. Ningependekeza kwamba tuwaruhusu watu kufanya hivyo. Hiyo ni kwa sababu, kuna watu wengine ambao wanajua kwamba wanapendwa na wananchi, lakini wanakataliwa na chama chao. Ilhali, wale ambao hawapendwi na wananchi wanapendelewa na kamati ya uchaguzi. Ukikataliwa na kamati ya uchaguzi, utafanya nini? Itakubidi uhamie chama kingine. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}