GET /api/v0.1/hansard/entries/226169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 226169,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/226169/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kugusia swala la wapiga firimbi. Hao ni watu ambao wanatusaidia. Wanatuambia ufisadi uko wapi. Wanaiambia Serikali ufisadi huko wapi. Wanasema: \"Ewe Serikali, tumesikia umetangaza vita dhidi ya ufisadi! Ufisadi uko hapa! Kuja!\" Lakini ubaya ni kwamba, wanapotuambia palipo ufisadi, na ufisadi unatoa macho ya vita na kuelekea kuwapiga, sisi wenyewe hatusimami nao! Bw. Naibu Spika wa Muda, tunamkumbuka Munyakei! Ni shujaa ambaye anastahili kutuzwa na Serikali na Rais, hata kama atatuzwa baada ya kifo chake. Yeye ni mmoja wa wale waliofutwa kazi, akaishi katika taabu na hatimaye, akafa na kuiacha familia yake katika taabu kubwa. Hayati Munyakei hakuwa peke yake. Kuna wapiga firimbi wengi ambao walisema: \"Hapa kuna ufisadi! Serikali, kujeni mpigane na ufisadi huu!\" Badala ya Serikali kwenda kupigana na ufisadi huo, inaruhusu wapiga firimbi wapigwe vita. Bw. Naibu Spika wa Muda, najua kuna ufisadi uliofichuliwa katika Chuo Kikuu cha April 17, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 675 Egerton. Kulikuwa na wafanyikazi \"hewa\" - watu ambao hawamo! Lakini, kila mwisho wa mwezi, wanalipwa mshahara. Kulikuwa na watu zaidi ya 500. Kuna walimu na wafanyakazi waliohusika. Walimu hao wanatimuliwa mmoja mmoja na wenye kufanya ufisadi huo wanaendelea kujikita, kupata nguvu na hata kuongezewa madaraka. Bw. Naibu Spika wa Muda, kama hatulindi wapiga firimbi, ni afadhali tuseme ya kwamba hatuna nia ya kupigana na ufisadi. Hakuna ufisadi unaweza kupiganwa nao bila ya kuwekea wapiga firimbi ulinzi. Sasa kuna sheria ambayo ingesaidia polisi na vyombo vingine vya dola kuhakikisha ya kwamba wapiga firimbi wanapewa ulinzi wanaostahili na kuhitaji. Kwa bahati mbaya, sheria hiyo haifanyi kazi. Bw. Naibu Spika wa Muda, hapa kuna hoteli ya Grand Regency ambayo miaka mitatu iliopita waliwafukuza wapiga firimbi 11; wafanyakazi ambao walisema: \"Hapa kuna ufisadi unaoendeshwa na Kamlesh Pattni\" ambaye sasa amekuwa mhuburi mkuu. Ama ni askofu?"
}