GET /api/v0.1/hansard/entries/226184/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 226184,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/226184/?format=api",
    "text_counter": 310,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa naongea juu ya wapiga firimbi. Nilikuwa nasema kwamba kuna wapiga firimbi 11 ambao walikuwa wameajiriwa kazi katika Hoteli ya Grand Regency ambao hatimaye ilijulikana kwamba walifutwa kazi kimakosa. Walitakikana kurudishwa kazini lakini mpaka sasa wafanyakazi hawa 11 hawajarudishwa kazini, ingawa tumepitisha sheria ambao inaruhusu Serikali kuwapa ulinzi na kuhakikisha ya kwamba wamerudi kazini kama ilivyo haki yao. Utatokwa na machozi ukifahamu ya kwamba wafanyakazi hao wamemwandikia mhe. Michuki barua wakimtaka awape ulinzi ili waweze kurudi kazini. Walipokuwa wakiandika hiyo barua, walisema ya kwamba watoto wao walikuwa wametoka shuleni kitambo kwa sababu hawana pesa za kuwalipia karo. Walisema ya kwamba wanaomba chakula chao na cha familia kila siku. Walisema ya kwamba hata nyumba wanazoishi wanakodishiwa na watu ambao wanawahurumia. Ukisoma hii barua, utatokwa na machozi. Watu hao wanaadhibiwa, wanaumia, watoto wao wanakosa mahitaji ya kila siku kwa sababu, mhe. Michuki amekosa kuwapa ulinzi. Bw. Naibu Spika wa Muda, isitoshe; Wizara ya Katiba na Haki, ya mhe. Karua, imeandika barua pia ya kutaka watu hao warudishiwe kazi lakini hawarudishiwi. Hatimaye, unauliza ni nani katika nchi hii ana nguvu za kuamuru jambo kufanyika na linafanyika? Ikiwa Wizara mbili zinaweza kushindwa kuhakikisha ya kwamba hao wafanyakazi wamerudishiwa kazi yao, unashindwa watamlilia nani. Watakwenda kwa nani ili wapate kurudishiwa kazi yao? Katika barua ambayo nina nakala zake hapa, hao wafanyakazi wanamshtaki afisa mmoja wa polisi ambaye wanasema anaitwa David Kimaiyo ambaye anasemekana ni Deputy Operations Officer ama Commissioner ambaye wanasema ya kwamba ameapa kwamba hawaturudi kazini mwao. Kama polisi wanaweza kukaidi amri ya Mawaziri wawili, unashindwa katika vita hivi ya kupigana na ufisadi, polisi wamo upande gani? Polisi anawezaje kukaidi Waziri wake na Waziri huyo asimfute kazi? Labda ndio sababu wengine wetu hatukupewa kazi za Uwaziri kamilifu kwa sababu kweli, mimi ningekuwa Waziri halafu afisa anikaidi kiasi hiki, nitamfuta kazi, liwalo liwe! Hii ni kwa sababu tungetarajia polisi wetu kuwa katika mstari wa mbele wa kupigana na ufisadi. Lakini kama wao ndio wanatetea wafisadi, kusumbua na kuhakikisha ya kwamba wapiga firimbi hawalindwi ijapokuwa kuna sheria inayowataka wafanye hivyo, basi unajua tuko taabuni. Kama polisi hawakuunga mkono vita dhidi ya ufisadi, hivi vita vitatushinda. Hatutafaulu! Polisi lazima wawe katika mstari wa mbele lakini nimeona hawamo. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaweza kuongea juu ya kwangu Subukia. Nimeona polisi wakiajiriwa ni kama wanapewa kazi na matajiri katika Subukia. Kila wakati kukiwa na ugomvi kati ya watu ambao ni wa kawaida na tajiri katika Jimbo la Subukia, utawaona polisi kuwa mbio zao ni za kwenda kuwa upande mmoja na tajiri. Mwishowe unashindwa, hao polisi hawaelewi kuwa mshahara wanaolipwa umechangiwa na kodi ya maskini pamoja na matajiri na kwamba maskini wana haki kama vile matajiri? Kama tunataka kupigana na ufisadi, basi tuwashirikishe polisi. Ikiwa polisi watakuwa ng'ambo ile nyingine, tujue ya kwamba hatufaulu katika vita hivi! Kuna polisi wengi ambao waliugua kasumba hii ya kuwa upande wa ufisadi na wangali wanaugua. Ni kama hakuna daktari wa kuwatibu. Bw. Naibu Spika wa Muda, sijui ni nani atamfikishia mhe. Michuki ujumbe wangu kwamba ni muhimu sana awapatie hawa wafanyakazi ulinzi. Hapa ninayo barua moja imeandikwa na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Nairobi ikimwamuru OCPD wa Kituo cha Polisi cha Central awape hawa wafanyakazi ulinzi lakini amri hiyo imekaidiwa. Pana mtu mwingine ambaye amepiga simu na kusema, \"Achananeni na mambo hayo.\" Ni kama tunaishi katika pori ambamo uhai wa kila mtu unategemea ukali wa meno yake na urefu wa kucha zake. Ikiwa meno yako si makali na kucha zako si ndefu, basi utaliwa mchana. Hivyo ndivyo imewafanyikia hawa niliowataja. Hiki ni kisa cha kusikitisha sana kwa sababu hata vyombo vya habari navyo vimeshindwa kulizungumzia April 17, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 677 swala hili. Kwa nini haviongei juu ya mambo kama haya? Watu wanaumia ilhali wao wanaandika maneno ambayo hayana maana, kwa mfano, mambo ya mamluki waitwao Artur na ndoa inayopangwa baina ya mmoja wao na Bi. Wangui. Kwa nini wasishughulukie mambo ambayo ni muhimu?"
}