GET /api/v0.1/hansard/entries/226770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 226770,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/226770/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, asante sana kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja hii muhimu sana kuhusu kilimo cha korosho na vita dhidi ya ufisadi. Ninasimama kuunga mkono kabisa Hoja hii. Hii ni kwa sababu baadhi ya watu wangu wa Eneo la Uwakilishi Bungeni la Wundanyi walifanya kazi katika kiwanda hicho kabla hakijanunuliwa na watu binafsi. Wengi wao wanaishi maisha ya shida katika mji wa Kilifi. Bw. Naibu Spika, tukiwa katika Bunge hili hatuwezi kujua ni upande gani wa Serikali au Upinzani. Hii ni kwa sababu hata Mawaziri na Wasaidizi wao hulalamika na kunung'unika kama sisi wa Upinzani. Ikiwa Serikali inaona kuna umuhimu wa kufufua kiwanda hicho, basi kwa nini wasifanye hivyo? Hiyo hatua wangekuwa wameichukua kitambo; sio kungojea hadi Hoja iwasilishwe hapa Bungeni. Haifai wao kulalamika kama sisi wa upande wa Upinzani. Ikiwa Serikali imeamua kuuangamiza ufisadi, basi yafaa ichukue hatua mwafaka kwa sababu tuna polisi wa kutosha na pia tuna tume ya kupambana na Ufisadi. Hatuwezi kuisamehe Serikali kwa jambo kama hili kwa sababu tumewapa mamlaka ya kutuongoza. Wanamngojea nani achukue mamlaka April 11, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 515 ili apambane na ufisadi au afufue kiwanda cha Kilifi? Haifai kungojea Hoja kama hii iwasilishwe hapa Bungeni ili wachukue hatua. Tunajua Serikali hii hata kama tutapitisha Hoja hii hakuna hatua watakayochukua. Ni kweli Hoja hii itapitishwa ikiwa na marekebisho yaliyopendekezwa na mhe. Mwenje ya kuwahusisha Wabunge wa pande zote mbili za Bunge hili na pia kuwazingatia washika dau wa korosho. Ukiangalia orodha ya wale waliopendekezwa ni wawili tu ambao ni washika dau wa korosho. Ningependa waongezwe zaidi ili pande zote zihusike. Hata hivyo, wale waheshimiwa Wabunge walioko upande wa Serikali hawafai kulalamika, kwa sababu wanaweza kuchukua hatua mara moja. Sio lazima wangojee Hoja iletwe hapa Bungeni. Wamepewa nafasi na uwezo mkubwa na wananchi wa Kenya. Tendeni badala ya kulalamika! Bw. Naibu Spika, nchi za Magharibi zinatuambia kwamba mashirika ya umma hayawezi kufanya kazi kwa sababu hayawezi kuongozwa vizuri kutokana na ufisadi. Ikiwa tutafanya uchunguzi katika haya mashirika ya umma, kwa mfano, kiwanda hiki cha korosho cha Kilifi ili tujue jinsi kiliporwa na kuangushwa, tutagundua kwamba mashirika haya yanaweza kufanya kazi yanavyopaswa ikiwa wale watu ambao ni wezi watachukuliwa hatua zinazowezekana. Kiwanda hiki cha korosho cha kilifi hakikuanguka kwa sababu kilikuwa cha umma. Kilianguka kwa sababu kiliendeshwa vibaya na pia kulikuwa na ufisadi mwingi ndani yake. Kwa hivyo, tukifanya uchunguzi na kupata uhakika jinsi kiwanda hiki kilianguka na kuwachukulia waliohusika hatua za kisheria, itatusaidia katika lengo letu la kuyafufua mashirika yote ya umma ambayo yameanguka katika sekta mbali mbali. Hatua hii pia itatusaidia kuyaendeleza yale ambayo yanafanya kazi kwa sasa. Umuhimu wa kilimo cha korosho hauwezi kusisitizwa kwani unajulikana wazi. Korosho ina soko kubwa sana duniani. Kilimo hiki kikifufuliwa, kinaweza kuchangia katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu. Katika ndege nyingi za usafiri wa umma kuna korosho. Hata ulaya kuna bidhaa nyingi ambazo zinatokana na korosho. Katika sehemu yangu ya uakilishi Bungeni ya Wundanyi, tayari kuna harakati za kufufua kilimo cha korosho. Watu wengi sana wanapanda korosho katika sehemu hiyo. Kwa hivyo, kufufuliwa kwa kiwanda cha korosho cha Kilifi kutasaidia sana kuendeleza kilimo cha korosho. Hata hivyo, wananchi wangependa waondolewe hiyo hofu kwamba kiwanda hicho cha korosho kitaporwa tena baada ya kufufuliwa. Kuna watu ambao wametajirika kwa sababu ya kuangusha mashirika ya umma kama lile la kiwanda cha korosho cha Kilifi ilhali hawajachukuliwa hatua yoyote. Jambo hili linawatia hofu wakulima wa korosho na mimea mbali mbali. Singependa kuzungumza mengi zaidi, lakini kwa ujumla ni wazi kwamba Serikali lazima iunge mkono Hoja hii. Nakubaliana na marekebisho ambayo yamependekezwa na mhe. Mwenje, lakini ni jukumu la Serikali kuiunga mkono Hoja hii. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}