GET /api/v0.1/hansard/entries/227943/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 227943,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/227943/?format=api",
"text_counter": 320,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. M.Y. Haji",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ninasimama hapa kuunga mkono Hoja hii. Bunge ni pahali ambapo wananchi wa Kenya walituchagua kuja kwa sababu walijua sisi tunaweza kuwaongoza. Hoja hii ni juu ya maisha ya binadamu. Hoja hii inahusu maisha ya watu ambao tunawakilisha hapa Bungeni. Kwa hivyo, halitakuwa jambo nzuri kwa sisi kulaumiana au kutukanana. Ni lazima tuonyeshe ukakamavu kuwa sisi tunafaa kuongoza na kwamba yale mambo ambayo tutazungumza hapa yataleta suluhisho kwa matatizo katika Wilaya ya Mt. Elgon. Bw. Naibu Spika, ni kawaida kwa wazee au watu wowote likitokea jambo kama hili kuulizana swali. Tumesikia ya kwamba haya matatizo yalianza mwezi wa nane, mwaka jana. Mpaka leo ni karibu miezi minane. Kwa nini matatizo haya hayakutatuliwa kwa wakati uliofaa? Tunajua ya kwamba hata vita vya Marekani na Iraq havikuchukua miezi minane. Ni ajabu ya kwamba wilaya ndogo kama ya Mt. Elgon, watu wanazozana na wanauana kwa muda mrefu. Ni kwa sababu hii Hoja kama hii imeletwa ili tujadiliane na tuone njia ambayo tunaweza kutatua haya April 4, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 359 matatizo. Bw. Naibu Spika, ni aibu kwa nchi yetu kusikia ya kwamba kuna kikundi cha watu ambao wanajiita Sabaot People's Land Force. Sisi tunajua ya kwamba kuna Serikali na ni kosa la jinai kwa kikundi cha watu fulani kujitwika silaha na kusema wazi wazi kwa runinga kuwa wako tayari kutetea ardhi yao. Hata wanavaa mavazi rasmi. Hii inaonyesha ya kwamba kuna hatari na ikiwa hatutachukua hatua mwafaka, basi nchi hii inaweza kuwa na matatizo. Bw. Naibu Spika, nilikuwa Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa kwa muda mrefu. Kwa hivyo, ninajua matatizo ya Wilaya ya Mt. Elgon vizuri na vile yalivyoanza. Ninafurahi kusema ya kwamba wakati huo ambapo mashamba haya yaligawanyiwa watu, watu wa wilaya hiyo walikuwa na uhusiano mzuri kati yao. Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya miaka kumi watu hawa wanazozana juu ya mashamba katika sehemu hiyo. Jambo lingine ambalo linafanya matatizo haya kuwa magumu, ni kwa sababu si kawaida ya watu wa jamii moja kuuana juu ya jambo kama hili. Kwa hivyo, Serikali ni lazima iingilie haya matatizo kwa nguvu zaidi kuliko wanavyofanya sasa. Suluhisho si kupeleka askari wengi katika wilaya hiyo. Tunaambiwa ya kwamba askari hao wanachoma nyumba na kuwabaka wanawake. Mimi kama mkuu wa mkoa na Waziri wa zamani, ninaishauri Serikali hii iwapeleke ma-DO 15 katika Wilaya ya Mt. Elgon. Ninapendekeza pia wilaya hiyo igawanywe katika sehemu 15. Halafu kila sehemu iwe na askari wa utawala na wala si vikosi vya GSU ama Jeshi la Nchi Kavu. Wao wachunguze chanzo cha matatizo haya. Tunajua ya kwamba wakuu wa wilaya wana lugha ya kuweza kuzungumza na kuwatuliza watu. Pia wana mbinu ya kupata mashauri kutoka kwa wazee na vijana ili tuweze kusuluhisha jambo hilo. Haifai kuwapeleka askari wengi kwa sababu si watu wa nchi zingine ambao wana sababisha vita. Askari wa kikosi cha GSU na Jeshi la Nchi Kavu wanahitajika sana kulinda usalama mipakani. Kwa mfano, Wilaya ya Marsabit watu wetu wanauwawa na majangili kutoka nchi jirani. Tunafaa kupeleka kikosi cha GSU na Jeshi la Nchi Kavu katika wilaya hiyo kulinda mpaka wetu. Lakini jambo la ndani kama matatizo haya, yanaweza kutatuliwa kwa njia ya kikazi bila kutumia nguvu yoyote. Bw. Naibu Spika, chanzo cha matatizo haya kinaweza kuwa ni siasa. Hata hivyo, siasa haiwezi kuwa suluhisho---"
}