GET /api/v0.1/hansard/entries/228292/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 228292,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/228292/?format=api",
"text_counter": 299,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Mr. Moroto): Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili pia nichangie Hoja hii iliyo mbele yetu. Mara nyingi sisi husema tuko pamoja kama Wakenya na kuwa ni lazima tuipende na kujivunia nchi yetu. Lakini tunastaajabu tukiangalia jinsi mambo yanavyofanyika wakati mwingine. Bw. Naibu Speika wa Muda, nashukuru kwa sababu Hoja hii inazungumzia mambo ambayo yanaweza kutujenga na kutuweka pamoja tukiyazingatia. Bw. Naibu Spika wa Muda, tukizungumza juu ya uteuzi wa Mawaziri, Mawaziri Wasaidizi na maofisa wengine wa Serikali--- Kwa mfano, kuna Hoja iliyoletwa Bungeni kuhusu uteuzi wa 414 PARLIAMENTARY DEBATES April 4, 2007 Dr. Rotich. Mpaka sasa wengi wetu tunauliza ni jambo gani lilifanyika kuhusu uteuzi huo. Tuna haki ya kupinga uteuzi mwingine, hata tukiwa wachache, mpaka tuambiwe ni jambo gani lilifanyika kuhusu uteuzi wa Dr. Rotich. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati Rais alikuwa akiwateuwa Mawaziri, Mawaziri Wasaidizi na maofisa wengine Serikalini, kuna Mpokot aliyebahatika kuteuliwa kama Chief of Protocol . Yeye ni Bw. Stephen Loyatum. Ajabu ni kwamba Waziri mmoja alimwondoa kutoka kazi hiyo na kumbadilisha na mtu wake. Lakini kwa sababu ni mtu anayetoka katika jamii iliyotengwa katika Jamhuri ya Kenya, hakuna mtu aliyejali na kuyafuata mambo hayo. Hata Rais mwenyewe hakuchukua hatua yoyote. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo, hili ni jambo ambalo tunawaambia Wakenya na Wabunge walio hapa---"
}