GET /api/v0.1/hansard/entries/228305/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 228305,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/228305/?format=api",
"text_counter": 312,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Mr. Moroto): Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwa kweli, tumepiga hatua kama Wakenya na kwa kiwango fulani, Serikali imejaribu sana. Lakini, kuna mambo mengine ambayo yanaudhi zaidi na yanaweza kuchafua hata yale mazuri ambayo Serikali imefanya, kama yale tuliyogusia wakati huu. Nilikuwa najiuliza swali fulani. Wakati niliona kikundi cha dada zetu wa FIDA walipoketi na kutoa jina la mmoja wao hali kuwa tunajua kwamba kuna madada wengi ambao wanaweza kufanya kazi hiyo, kwa mfano, yule mwenyekiti wa Maendeleo ya Wanawake wa Jamhuri ya Kenya, kwa muda kidogo alioshikilia jukumu hiyo, kuna mabadiliko makubwa! Hakuna mtu atakayekuja kusema: Okay, wacha April 4, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 415 tumshukuru dada huyu kwa sababu anatoka kona nyingine ya nchi, ambayo watu wanaona kuwa sio mtu wa maana. Wazo ninalotaka kusisitiza zaidi ni kwamba kuanzia sasa, kila mtu lazima aangalie mahali anapokanyaga ili isije ikawa kwamba, wakati unapopiga hatua ukifikiri kuwa unapiga hatua, kuna watu wengine ambao wanaweka visiki kwenye njia yako. Hatutaki madharau. Tunaheshimiana na tunajua ni nani anaweka mali na ni nani anaweza kufanya jambo fulani. Namshukuru sana Mbunge wa Molo kwa jambo alilogusia na kusisitiza sana. Hata ameanza kuuliza na kuisihi jamii fulani ambao wanafikiria kuwa wao ndio bora peke yao katika Jamhuri ya Kenya kuliko wengine. Wakenya wanaangalia, na hatutaki watu wachache; tunajua kwamba sio wengi au wote ambao wanaharibu. Kuna wale ambao wanafanya---"
}