GET /api/v0.1/hansard/entries/228500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 228500,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/228500/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Achuka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 353,
        "legal_name": "Francis Achuka Ewoton",
        "slug": "francis-ewoton"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hotuba ya Rais. Hotuba hii ilikuwa na mpango mzuri sana na ikiwa yale aliyoyasema yatatekelezwa, nchi hii itaendelea mbele. Katika Hotuba ya kwanza ya Rais mwaka wa 2003, mimi sikukubaliana nayo kwa sababu mara nyingi tunasomewa Hotuba nzuri ya Rais na baadaye hakuna vitendo. Lakini leo ninaunga Hotuba ya Rais mkono kwa sababu baada ya Hotuba ya 2003 mimi nimeridhika na vitendo vyake na mipango yake katika nchi hii. Kwa muda wa miaka michache; minne sasa, tumeona maendeleo. Nchii hii imekuwa na maendeleo mengi. Maendeleo yamefanyika kila mahali; kila eneo la uwakilishi bungeni na katika kila kijiji. Ni lazima tuseme ukweli ukifanyika. Hakuna haja tukatae vitendo ambavyo vinafanyika mbele yetu. Mtanisamehe kwa sababu nina homa. Bw. Naibu Spika wa Muda, tangu tuliponyakua Uhuru, sisi bado hatujaona maendeleo ambayo yamefanyika Turkana kwa wakati huu. Kwa muda mfupi wa miaka mitatu, katika kila eneo la Ubunge kuna miradi mingi ambayo inafanyika kupitia kwa LATF, CDF na idara za Serikali. Miradi kama hiyo haikufanyika hapo mbeleni, lakini inafanyika sasa wakati wa Serikali ya Rais Kibaki. Ni lazima tutambue kwamba Rais Kibaki ni mtu aliye na ujuzi wa kazi. Yeye si mtu ambaye anaweza kufundishwa jinsi ya kuongoza nchi hii, kwa sababu yeye alishiriki katika vita vya Uhuru, amekuwa Mbunge, Waziri na hata Makamu wa Rais kwa miaka kumi. Ni lazima tutambue kwamba yeye ataendelea kuongoza nchi hii na kuleta maendeleo zaidi. Sioni ni kwa nini tunakataa kutambua ukweli au kukubali vitendo vinavyodhihirisha ukweli. Yale mengine ambayo yanaendelea hapa si ukweli na si demokrasia. Kitu kinachoendelea hapa ni kujitakia makuu. Ni ukabila mtupu. Wakati huu tunachosikia katika kila kituo cha habari ni kila mtu kujitakia makuu na kueneza ukabila. Wakati huu, kila kabila linataka kuchagua Rais wake. Hiyo itawezekana kweli? Tukiendelea hivyo, Kenya itakuwa ya makabila au ya watu wote? Bw. Naibu Spika wa Muda, ningewaomba Wabunge wenzangu, na Wakenya wote kwa jumla, watambue ukweli; wawe wazalendo na tutambue ile kazi ambayo Serikali inafanya kwa wakati huu. Hakuna maana sisi tukatize maendeleo ambayo yamepangwa kuijenga nchi hii. 312 PARLIAMENTARY DEBATES April 3, 2007 Ninaamini kwamba tukimpatia Rais Kibaki kipindi kingine cha miaka mitano huo hautakuwa muda mrefu. Kwa nini tumnyime miaka mitano? Tumpatie yeye nafasi aongoze kwa miaka mingine mitano, kwa sababu tunaona ishara ya maendeleo ambayo amepanga kutekeleza, ambayo yataifaidi nchi hii. Tukimkatiza wakati huu, tutarudi nyuma na kuanza kutafuta tena jinsi ya kwenda mbele. Kwa hivyo, hakuna maana ya Rais kustaafu baada ya miaka mitano peke yake na hali anafanya kazi nzuri. Jambo la maana ni kutambua kwamba sisi ni Wakenya na tumheshimu kiongozi wetu ambaye tuko naye wakati huu. Hii ni kwa sababu sisi sote, makabila 42, ni kitu kimoja. Yule mmoja atakayechaguliwa kuwa kiongozi, awe Turkana au Msomali, inafaa tumuunge mkono. Tukifanya hivyo, tutapata baraka na kufanya maendeleo ya kweli. Kutambua na kumheshimu kiongozi ambaye yuko wakati huu, ambaye alipata uongozi kimiujiza--- Watu wengine hawakumtarajia apate uongozi, lakini kwa miujiza ambayo ilifanywa na Mungu kupitia kwa wananchi, alishinda urais. Kwa hivyo, yeye yuko na baraka. Tukiheshimu uongozi wake na kumuunga mkono, tutapata baraka, amani na maendeleo. Jambo tunalopaswa kutambua ni hili; Serikali imepiga hatua kubwa kimaendeleo. Ni lazima tukubali hilo. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo ambalo ningeomba Serikali irekebishe ni usalama. Hii ni kwa sababu usalama ni jambo kubwa. Tunatka kila kijiji kipate usalama wa kutosha. Hawa askari wa kibinafsi wanatakikana kufunzwa vizuri na kupewa bunduki, kwa sababu majambazi wanatatiza wananchi katika kila kijiji. Wanaenda kwa vijiji na kufanya vile wanavyotaka bila hatua yoyote kuchukuliwa ya kuokoa wale wanaoishi huko. Kwa hivyo, ni vizuri sisi tuige ile mpango iliyoko katika nchi nyingine kama vile Uganda. Kule wameweka vigilantes kila mahali na wanawapatia bunduki. Serikali ikifanya mpango bora wa kuwafunza askari wa kibinafsi na pia kuwapa silaha, tutaimarisha usalama. Hata wale askari wa kuchunga benki ni lazima wapewe bunduki. Usalama ni muhimu sana ndani na nje ya mabenki. Jambo la pili ambalo ningeomba Serikali iangalie kwa makini ni hali ya barabara. Ninajua kwamba Serikali ina mipango ya kurekebisha barabara, lakini inafanya hivyo pole pole. Ni vizuri kama Serikali ingelitilia jambo hili maanani zaidi. Kwa mfano, kama kampuni fulani imepewa kandarasi ya kutengeneza barabara, isiwe tu ni kampuni moja. Ni vizuri kandarasi zitolewe kwa kampuni tofauti tofauti. Kwa mfano, kampuni moja ipewe kandarasi ya kurekebisha barabara kutoka Nairobi hadi Naivasha, na nyingine iendelee na kazi hiyo kutoka hapo hadi Nakuru. Ikipangwa hivyo, barabara nyingi zitarekebishwa. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}