HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 228507,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/228507/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Dzoro",
"speaker_title": "The Minister for Tourism and Wildlife",
"speaker": {
"id": 247,
"legal_name": "Morris Mwachondo Dzoro",
"slug": "morris-dzoro"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Nami ningependa kusema kwamba ninaunga mkono Hoja juu ya Hotuba ya Rais kwa sababu, kufikia sasa, kuna mambo mengi ambayo tumeona yakiendelea. Sasa tuko huru kuzungumza tunavyotaka, na magazeti kuchapisha habari wanazotaka bila wasiwasi. Hali hiyo ya uhuru iko katika hali inayotakikana. Uhuru wa kuabudu uko katika hali ambayo ni ya maana sana katika taifa letu la Kenya. Ni kwa sababu hiyo nchi nyingine zimeweza kujua kwamba demokrasia inadumishwa katika nchi hii. Ningetaka tu kuongeza kwamba, tupoufurahia uhuru huo, ni lazima kuweko na utaratibu utakaotuwezesha sisi, kama wanasiasa pamoja na vyombo vya habari, kusawazisha hali katika shughuli zetu za kila siku. Tumeona mambo mengi yakibadilika, kwa mfano kuhusiana na uchumi. Ingawaje mwenzangu aliyetangulia kuzungumza alisema kwamba uchumi umekua kwa kiwango kidogo tu, ningependa kusema kwamba, kama isemwavyo, haba na haba hujaza kibaba, na kwamba hakuna safari ndefu isiyokua na hatua. Kwa kweli, tumepiga hatua. Sisi, kama viongozi na wakaaji katika nchi hii ya Kenya, tunastahili kuishukuru Serikali kwa yale machache yanayotendeka, tukiamini kwamba makubwa pia tutayapata. Tunapoona kwamba kuna maendeleo lakini hatuyatambui, na badala yake tunatamani makubwa tusiyonayo, tutakuwa tunakosa. Inafaa tushukuru kwa kile tulichonacho, tukiamini kwamba tutapata maendeleo zaidi. Uchumi umekua, na hiyo si siri. Kila mmoja ameliona jambo, na anaweza kulifurahia. Bw. Naibu Spika, ningependa kupendekeza kwamba kadri uchumi unavyokua - ni matarajio yangu kwamba utaendelea kukua zaidi - liwe jukumu la kila mwekezeji anayetaka kuanzisha viwanda afanye hivyo katika sehemu nyingine nchini badala katika miji mikuu. Sasa, umeme unapatikana katika kila sehemu humu nchini. Sehemu nyingi humu nchini zinasambaziwa umeme. Maji pia yanasambazwa kila mahali. Kwa hivyo, ningependa kupendekeza, kama walivyofanya baadhi ya Wabunge wenzangu, kwamba wale wanaotaka kuanzisha viwanda humu nchini wasifanye hivyo tu katika miji mikubwa bali pia katika miji midogo. Kufanya hivyo kutatusaidia. Viwanda vikianzishwa katika miji midogo, vijana wetu waliohitimu katika nyanja mbali mbali, wanapotafuta kazi, badala ya kwenda katika miji mikubwa, ambako itawabidi wakodishe nyumba ambazo watalipia kodi mbali na kununua chakula, wataweza kupata kazi katika vijiji na kulala nyumbani kwao huku pia wakifanya shughuli za kilimo. Kwa hivyo, hali ya maisha itaboreshwa zaidi kwa njia hiyo. Kama inavyosemwa, utalii umeendelea. Lakini, ningependa kuwafahamisha Wakenya kwamba katika dunia nzima, utalii ni sekta ambayo inaweza kupanua uchumi, si wa Serikali ama nchi tu bali pia ule wa watu binafsi. Ndio maana tumeamua kwenda katika kila sehemu nchini kuona yaliyopo ili tusambaze shughuli za utalii kote nchini. Hatutaki shughuli za kitalii ziwe tu 320 PARLIAMENTARY DEBATES April 3, 2007 katika sehemu fulani. Tunataka kila mahali humu nchini pawe mahali ambapo watalii wanaweza kutembelea. Hivyo ni kusema kwamba wakaaji wa Kenya wanapofikiria kujenga hoteli, wafikirie kufanya hivyo katika miji tofauti tofauti. Watalii wako tayari kuitembelea miji hiyo, haswa wakati huu ambapo tumesema kwamba tutaenda katika sehemu kadha wa kadha kutengeneza ratiba ya vivuta watalii. Tungependa watu wajitokeze na waingilie biashara ya utalii kwa upande wa mahoteli na mambo ya kitamaduni. Ninaamini kwamba kwa njia hiyo, watu watajifundisha mengi na uchumi miongoni mwa watu binafsi utaimarika. Bw. Naibu Spika, tunahitaji kutilia mkazo mambo ya kilimo, haswa wakati huu uchumi unapoimarika. Ni lazima wakulima wapewe kipaumbele. Njia zote zitumiwe ili ukulima bora uweze kufanyika katika sehemu za mashinani, na wale wakulima waliojitolea wapewe vifaa na mbinu ambazo zitawawezesha kujitengenezea si vyakula tu bali pia vitu watakavyouza na kupata hela. Tukifanya hivyo, tutadumisha uchumi. Uchumi unapoimarika, inatakikana hali hiyo ionekane hata kule mashinani. Ni muhimu kumtambua mwananchi wa kule mashinani, na kufahamu kwamba naye anastahili kuuchangia uchumi wetu na aweze kupata faida kutokana na mchango wake. Watu wengi wanaotakiwa kufahamu jinsi uchumi wetu unavyoimarika wako kule mashambani. Wengi wa Wakenya hawaishi mijini, bali huishi mashambani. Kwa hivyo, tunapofikiria kuhusu mwelekeo unaofaa kuchukuliwa na nchi hii, ni lazima watu hao wapewe kipaumbele, na haswa zile kazi wanazofanya. Kazi muhimu zaidi ya watu wa mashambani ni kilimo. Kama nilivyosema, inafaa wawekezaji waanzishe viwanda katika sehemu za mashambani, na maswala ya kilimo yapewe kipaumbele. Pia ni vizuri tuweze kuzitumia raslimali tulizonazo kunyunyizia maji mimea yetu, haswa mboga, ili ukulima usiwe wa kuzalisha chakula tu bali pia uwe kama biashara ambayo italeta hela zitakazowasaidia wakulima wetu katika maisha yao na maisha ya jamii zao. Bw. Naibu Spika, nimefurahi kwamba tumepata elimu ya msingi bila malipo, ambayo imesaidia sana watoto ambao hawangeweza kupata karo. Kwa kweli, kuna uhaba wa walimu, lakini ni jambo la kufurahisha kusikia kwamba walimu zaidi wataajiriwa. Ni lazima jambo hili litiliwe mkazo ili elimu hii iwe ya faida, na watoto wengi waweze kuelimika. Zaidi ya yote, tunafaa kufikiria vile tutaweza kupata elimu bila malipo kwa shule za upili, kwa sababu kuna watoto wengi ambao wamekosa karo na hawawezi kuendelea na masomo yao. Unakumbuka kwamba kuna Hoja ambayo tulipitisha hapa ili kuwawezesha wanafunzi ambao wamefanya mtihani wa Kidato cha Nne na hawajamaliza kulipa karo, kupata hati zao bila wasiwasi."
}