GET /api/v0.1/hansard/entries/228513/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 228513,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/228513/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Mr. H.M. Mohamed): Ahsante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hotuba ya Rais. Rais Kibaki alitaja mambo mengi muhimu katika Hotuba yake, na tunampongeza. Kwa hakika, mafanikio mengi yamepatikana katika miaka minne iliyopita. Nafikiri pia kuna mambo mengi yanayohitajika kutekelezwa. Kwa mfano, tumepata elimu ya msingi bila malipo. Watu wengi wamefurahia hatua hiyo. Wakati umefika kwa Serikali kufikiria pia elimu ya sekondari. Kuna sehemu nyingi katika nchi hii ambazo wananchi hawawezi kugharamia malipo ya sekondari. Hata ikiwa elimu ya sekondari bila malipo haitawezekana katika nchi yote, tungeanza na sehemu April 3, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 323 fulani. Tungeanza na sehemu kame ambazo zina matatizo mengi. Bw. Naibu Spika, kwa vile muda wangu ni mdogo, ningependa kugusia ufugaji. Karibu asilimia 70 ya mifugo imekufa kwa sababu ya ukame. Baada ya ukame, ugonjwa wa Rift ValleyFever pia ulizuka na kuangamiza mifugo wengi sana katika nchi hii. Kuna mambo ya kusikitisha katika nchi hii. Ugonjwa wa Rift Valley Fever ulipozuka, Wizara ya Mifugo na Ukuzaji wa Samaki haikuwa na chanjo wala madawa. Tuliambiwa hakuna dawa katika nchi nzima. Ilibidi dawa ziagizwe kutoka South Africa na Egypt. Tunashangaa Wizara hiyo ilibuniwa ya nini ikiwa haina dawa. Asilimia 30 ya mifugo iliyobaki baada ya ukame, iliangamizwa na ugonjwa huo. Uuzaji wa nyama na bidhaa zinazotokana na mifugo ulipigwa marafuku kwa muda wa miezi minne. Watu wamepata matatizo mengi sana kutokana na hatua hiyo. Hadi sasa, wafanyabiashara wa ng'ombe na mbuzi hawaruhusiwi kusafirisha mifugo mpaka Nairobi na sehemu zingine. Mfano, katika soko kubwa la mifugo la Garissa, maafisa wa mifugo wamekataa kutoa vibali vya kusafirisha mifugo. Wananchi wameambiwa waende kilomota 20 kutoka soko hiyo. Na huko hakuna maji wala nguvu za umeme. Maafisa hao wanalazimisha watu kupeleka mifugo yao huko. Ni muhimu Waziri wa Mifugo ahakikishe kwamba wananchi wamepewa vibali vya kusafirisha mifugo yao. Bw. Naibu Spika, ningependa kuzungumzia juu ya bei ya bidhaa muhimu kama sukari, unga na kadhalika. Inasikitisha sana kwa sababu bei ya sukari imefika zaidi ya Kshs100, kutoka Kshs40 miaka mitatu iliyopita. Hali hiyo imeletwa na ufisadi. Ugawaji wa sukari katika nchi hii umepewa watu wachache ambao wanaificha. Hatua hiyo imesababisha bei ya sukari kuwa juu zaidi. Pia, uagizaji wa sukari kutoka nje umepewa watu wachache. Nafikiri kuna Wizara \"inayokulia\" mambo hayo. Ningeomba Serikali iweke bei ya bidhaa muhimu. Tukiendelea hivyo, wananchi wa Kenya wataangamia! Bei ya sukari imekuwa ghali zaidi. Bw. Naibu Spika, nafikiri muda wangu umeisha. Kwa hayo machache, naunga mkono Hotuba ya Rais."
}