GET /api/v0.1/hansard/entries/228687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 228687,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/228687/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 246,
        "legal_name": "Joseph Matano Khamisi",
        "slug": "joseph-khamisi"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hii baada ya wiki nzima ya kusimama na kukaa. Ningependa kuongea machache kuhusu Hotuba ya Rais. Hotuba yake ilitaja mambo mengi kuhusu kukua kwa uchumi na rasilimali ya nchi hii. Pia ilitaja kuhusu jitihada ya Serikali katika kuendeleza miradi ya akina mama na vijana, hisia za Serikali kuhusu sera za mwaka wa 2030 na mambo mengi kama hayo. Lakini kuna jambo moja ambalo mhe. Rais hakusema wala kutaja; ni nini Serikali imefanya kumaliza swala la ardhi na maskwota katika nchi hii? Niliamini kwamba iwapo Serikali inatoa orodha ya mafanikio yake, ni muhimu kama ingetoa orodha ya yale yote ambayo inafikiria imefanya. Kwa kuwa Rais hakusema chochote kuhusu ardhi, inadhihirika wazi kwamba Serikali haijafanya chochote kuhusu swala hili nyeti. Haya ndio masikitiko yangu. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa miaka minne tumekuwa tukikera Serikali nje na ndani ya Bunge kuhusu swala hili. Vile vile, tumepewa ahadi nyingi na Waziri wa Ardhi na pamoja Rais mwenyewe kwamba swala hili lingesuluhishwa kwa muda mfupi. Lakini inavyoonekana muda wa Serikali utamalizika bila kushughulikia swala hili. Miaka mitatu iliyopita, tuliambiwa kwamba Serikali itatoa sera za ardhi. Mpaka wa leo, hakuna sera hizo. Tuliambiwa kwamba Serikali itachukuwa hatua kutekeleza Ripoti ya Ndung'u na kuhakikisha kwamba wale waliopata mashamba kwa njia ya undanganyifu watakamtwa na kushtakiwa. Mpaka wa leo, Ripoti ya Ndung'u haijatolewa kwa wananchi. Wananchi hawajui kama Serikali inachukuwa hatua dhidi ya wale waliofanya hujuma hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, sisi wahusika katika swala hili, ambao maeneo yetu yamekumbwa na maskwota na ukosefu wa ardhi, tunaona ya kwamba Serikali imeshindwa kutatua swala hili. Ikiwa kweli Serikali imeshindwa, ni ungwana kujitokeza na kusema, \"tumeshindwa kutekeleza jambo hili."
}