GET /api/v0.1/hansard/entries/228691/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 228691,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/228691/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 246,
        "legal_name": "Joseph Matano Khamisi",
        "slug": "joseph-khamisi"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, hivi majuzi, Rais alizuru Mkoa wa Pwani tena na matumaini yetu yalikuwa kwamba atatupatia ahadi ambazo tungefurahia. Lakini alikuja Mkoa wa Pwani na akarudi Nairobi na hakuna chochote tulichopata. Kwa hivyo, ni muhimu kwa Serikali, katika utekelezaji wa ahadi ilizotoa wakati ilipokuwa inataka mamlaka, itimize jambo hilo kabla ya kuondoka katika utawala mwisho wa mwaka huu. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumeambiwa katika Hotuba ya Rais kwamba, sekta ya utalii imeipatia nchi hii Kshs56 bilioni. Mimi kama mtu anayetoka Mkoa wa Pwani, ambako asilimia 60 ya mapato ya utalii yanatoka, hatujaziona hizi Kshs56 bilioni ambazo tunaambiwa. Tunataka Serikali ituambie bilioni hizo ziko wapi, ikiwa haziwezi kuonekana katika maeneo ambayo yanazalisha utalii. Hii ndiyo sababu naunga mkono yale yaliyosemwa hapa na wenzangu kwamba, suluhisho ni kuwepo na Serikali ya majimbo, ambapo baadhi ya mapato hayo yataachwa katika sehemu zinazozalisha mali. Tumeambiwa kwamba Kshs8 bilioni zimetumiwa kumaliza miradi fulani Mkoani Pwani. Tunataka Serikali itupatie orodha ya miradi iliyotumia hizo fedha. Kwa sababu mimi ninao mradi March 29, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 267 ambao haujamalizwa kama ilivyoahidiwa na Serikali; mradi wa Korosho. Kama hizo Kshs8 bilioni zingetolewa na baadhi yake tukaziona katika kufunguliwa kwa mtambo wa korosho, tungeweza kuamini kwamba hizo pesa zimeingizwa katika sehemu ya pwani. Hivi sasa, huo ni uzushi mtupu! Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna ahadi nyingine ambayo Waziri wa Fedha alitoa katika Ukumbi huu wa Bunge wakati wa Bajeti. Alisema kwamba, bandari ya Mombasa itafunguliwa kwa masaa 24 kwa siku ili kuweza kuondoa msongamano wa bidhaa na vile vile kutoa nafasi za kazi kwa wananchi. Mwaka mzima umepita na bandari ya Mombasa haijafunguliwa masaa 24 kama vile Waziri wa Fedha alivyoahidi. Hii ni moja ya ahadi nyingi za uongo ambazo zimetolewa na Serikali. Bw. Naibu wa Spika wa Muda, ningependa kuzungumza kuhusu pesa ambazo Serikali inasema inatoa kusaidia makundi ya akina mama au maendeleo ya akina mama. Ningependa kuipongeza Serikali kwa kuchukua hatua hiyo, lakini ningependa kuikumbusha pia kwamba kuna walemavu wengi katika nchi hii ambao wangependa kupata hazina kama hiyo, ili nao pia wapate kujumuika kama wananchi wengine. Kuhusu usalama, ni jambo la kusikitisha kwamba Serikali inaweza kuondoa wananchi kutoka nchi hii na kuwahamisha na kuwapeleka katika nchi za nje. Mfano ni kile kikundi kilichopelekwa Somalia na yule mtu aliyetolewa hapa na kupelekwa Cuba. Serikali hii ingekuwa ya busara ingewaeleza wananchi wa Kenya ni kwa nini raia wa Kenya wanahamishwa kutoka hapa na kupelekwa katika maeneo ya bara ambako ni nchi za kigeni kwao. Vile vile, kuna mtu ambaye anaitwa Felicien Kabuga. Kila siku tunaambiwa kwamba anatafutwa na Serikali na fidia kubwa imetolewa kwa yule mtu ambaye anaweza kumpata, na hali tunajua na kuambiwa kwamba mtu huyo huenda amefichwa katika nchi hii. Miezi miwili iliyopita kulikuwa na msako katika sehemu ninakotoka ikidaiwa kwamba Bw. Kabuga alikuwa amejificha katika eneo langu la uwakilishi la Bahari. Polisi walikuja wakavamia eneo lile na Kabuga hakupatikana. Tunaambiwa kwamba siku hizi anavaa kanzu na vitoroboshi. Ikiwa Serikali ina uwezo na nguvu za kupigana na uhalifu, inakuwaje kwamba ni rahisi kupata magaidi wa Kenya na ni vigumu kupata gaidi ambaye anatoka katika nchi nyingine, ambaye anaishi katika nchi hii? Serikali ina wajibu wa kuwaeleza wananchi kuhusu jambo hilo. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna hili swala la Katiba. Ninamshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kukutana na kundi la chama cha ODM-K hivi leo na vile vile kukubali kujumlisha kundi la wale wasiomo ndani ya Serikali katika mazungumzo ya kuangalia jinsi gani tunavyoweza kupata mabadiliko haba ya Katiba kabla ya uchaguzi wa mwaka huu. Ninavyoona ni kwamba, Serikali haina njia nyingine isipokuwa kukubali matakwa ya wananchi, ambayo ni kuleta mabadiliko ya kuweza kuweka sawa hali ya uchaguzi wakati utakapotokea. Mwisho kabisa, ningependa pia kuzungumza juu ya ukosefu wa maafisa katika miradi inayojengwa na CDF, waalimu na madaktari katika hospitali zetu. Wakati huu hospitali na shule nyingi zinajengwa na Serikali haiko tayari kutoa wafanyakazi katika sehemu hizo. Kwa hivyo, ningeiomba Serikali kutia bidii ili kwamba miradi hiyo itakapomalizika, watu waatandikwe kazi mara moja. Kwa hayo machache, ningependa kuunga mkono Hotuba ya Rais."
}